Tafuta

Katika Mkutano wa COP26 huko  Glasgow wapo hata watu wa Asilia Katika Mkutano wa COP26 huko Glasgow wapo hata watu wa Asilia 

Kutoka COP26:kusimamisha ukataji hovyo wa miti kufikia 2030

Katika mkutano wa COP26 unaoendelea hupo uamuzi muhimu wa kulinda na kurejesha mapafu ya kijani ya sayari.Zaidi ya nchi 100 zimejiandikisha kwa kutaka kuongeza kiasi cha euro bilioni 19.2.Huo mo muungano kwa kutaka kuokoa Msitu wa Mvua.Damira ni kutaka sasa kufanya jitihada ni kuhama kutoka katika matamko hadi kufikia matendo halisi.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Tamko la pamoja la thamani ya kihistoria, ni lile linalojitokeza katika siku ya pili ya kazi huko Glasgow nchini Scotland na ambalo linahusu dhamira ya kulinda urithi wa misitu duniani dhidi ya unyonyaji kiholela ifikapo 2030. Zaidi ya viongozi mia moja wa dunia, ambao wanaongoza nchi zilizo na misitu takriban asilimia 86% duniani, wameahidi kukomesha ukataji hovyo wa miti kwa kuweka mezani ahadi za kifedha, zikiwemo hata za binafsi, kwa kiasi cha euro bilioni 19.2. Makubaliano hayo pia yanajumuisha hatua za pamoja za urejeshaji wa mifumo ya ikolojia iliyojaribiwa vikali na ukataji miti hovyo na kwa usaidizi wa kifedha wa ajili ya  jumuiya asilia ambazo ni sehemu yake.

Miongoni mwa waliotia saini pia ni nchi ya Brazil, Urusi, China, Colombia, Indonesia, Australia, Costa Rica. Umoja wa Ulaya umejitolea kwa mabilioni na kwa ahadi ya udhibiti wa kukabiliana na ukataji hovyo wa miti, rais wa Marekani, Joe Biden, ametangaza kuwa ataliomba Bunge lake kutenga bilioni tisa ifikapo 2030. Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amefafanua makubaliano ya kukataza ukataji miti hovyo kuwa ya msingi kwa lengo la jumla ya kupunguza ongezeko la joto hadi nyuzi joto 1.5, ambalo ni kubwa zaidi kulingana na Mkataba wa Paris. Ahadi hiyo pia inajumuisha upandaji wa miti mipya isiyopungua trilioni moja, tena ifikapo mwaka 2030, ambayo ni muhimu kwa kunyonya hewa ya ukaa, na kukomesha mabadiliko ya tabianchi. Serikali za nchi 28 pia zitajitahidi kuondoa ukataji miti hovyo kutoka kwa biashara ya kimataifa ya chakula na mazao mengine ya kilimo kama vile mawese, soya na kakao.

Kuridhika lakini pia na tahadhari zimeoneshwa na wachunguzi waliopo huko Glasgow. Miongoni mwao ni Federica Bietta, Mkurugenzi Mkuu wa Muungano wa Msitu wa Mvua, (NGO) ambalo ni shirika lisilo la kiserikali linalojitolea pamoja na serikali, jumuiya na watu wa nchi za tropiki kusimamia kwa uwajibikaji misitu yao ya mvua. Kwa mujibu wake amesema: "Kwa hakika tunakaribisha kauli yoyote inayoletwa kuhusiana na misitu mbele baada ya kusahaulika kwa miaka hii ambayo iliaminika kuwa teknolojia iliokoa dunia. Lakini ikiwa hiyo inatosha, sijui. Tumekuwa tukilifanyia kazi suala hili kwa miaka mingi na tunaogopa kwamba hii ni moja ya matamko mengi ambayo hayatatimia. Ahadi iliyotolewa, tamko la wazi, dola bilioni 12 mezani lakini bila mwelekeo wazi wa jinsi ya kuzitumia, kwa njia gani. Hivyo ni wajibu wetu sasa kufanya kazi kwa bidii kwa maana hii".

03 November 2021, 15:35