Tafuta

Mlima wa Kilimanjaro Tanzania ni mrefu zaidi kati ya milima ya Afrika. Mlima wa Kilimanjaro Tanzania ni mrefu zaidi kati ya milima ya Afrika. 

Tanzania:wapanda milima 34 waanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro

Kundi linalojumuisha watu 34 kutoka katika nyanja mbalimbali kama vile za biashara,serikali,wanamichezo mashuhuri ,madaktari na wawakilishi wa vijana wameanza kupanda mlima Kilimanjaro nchini Tanzania tarehe 19 na watawasili kwenye kilele cha mlima huo tarehe 24 Oktoba ambayo ni Siku ya Umoja wa Mataifa.Lengo kuu ni kuhamasisha upatikanaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa wote.

Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 19 Oktoba Wapanda mlima 34 wameanza safari ya kupanda mlima mrefu zaidi barani Afrika wa Kilimanjaro nchini Tanzania kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kuhamasisha upatikanaji wa chanjo ya UVIKO-19 (COVID-19) kwa wote. Kundi hilo linalojumuisha watu kutoka katika nyanja mbali mbali kama vile za biashara, serikali, wanamichezo mashuhuri na wawakilishi wa vijana na  ambalo linatarajiwa kuwasili kwenye kilele cha mlima huo mnamo tarehe 24 Oktoba 2021 ambayo ni  Siku ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake mnamo 1945, sambamba na hiyo mnamo 1970 mkakati wa kimataifa wa maendeleo na vile  vile tarehe hiyo ni kuhusu habari za maendeleo iliyoanzishwa mnamo 1972 na Mkutano huko mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Mlima Kilimanjaro Tanzania na Wanyama
Mlima Kilimanjaro Tanzania na Wanyama

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, wapanda mlima hao kupitia mradi wa Kilimanjaro (Initiative,KI) wanabainisha kuwa wanawakilisha tamaduni, uchumi, mazingira na mabara tofauti wakiwemo vijana 10 wanaowakilisha kutoka miradi tofauti ya kijamii nchini Tanzania na shule za Tanzania na Kenya  pia wanawake wanariadha mashuhuru wa mbio za milimani, viongozi wa kisiasa, maafisa wa Umoja wa Mataifa, madaktari, wanasayansi na wawakilishi wa vijana.

Lengo lao kubwa la kupanda mlima Kilimanjaro ni kuelimisha kuhusu haja ya haraka ya kuwa na usawa wa usambazaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19. Fedha zitakazopatikana wakati wa kupanda mlima zitakwenda kwenye  mfuko wa Muungano wa Afrika AU wa kupambana na UVIKO-19 na kampeni ya Go Give One  nena utoe moja, inayosimamiwa na shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO.

Hata kwa upande wa WHO fedha zitatumika kutoa chanjo za UVIKO-19, wakati kipaumbe kikitolewa kwa  wale wanaohitaji zaidi katika nchi ambazo haziwezi kumudu chanjo hiyo.  Tim Challen, mwanzilishi wa  Shirika lisilo la Kiselikali (NGO) la  Kilimanjaro(Innitiative (KI) iliyoandaa upandaji mlima huo au The Big Climb akimkunuu mkurugenzi mkuu wa  Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Dk. Tedros Ghebreyesus amesema  kuwa kuelimisha kuhusu changamoto ya kutokuwepo haki ya upatikanaji wa chanjo ni muhimu ili kutafuta pamoha suluhusho lenye usawa. Lazima kuwpo ushirikiano kama familia ya kimataifa ili kupambana na UVIKO-19.  Upandaji wa Mlima mkubwa (The Big Climb) unawakilisha mchango wao katika juhudi hizi za pamoja.

Madaktari wengine  3 katika kundi hilo ni kutoka India, Marekani na kundi la utafiti la ISGlobal wanashiriki katika kampeni hiyo sanjari na mwanariadha Mira Rai kutoka Nepal ambaye ni balozi mwema wa Umoja wa Mataifa wa ushirikiano wa milima na Akinyi Obama-Manners akiwakilisha vijana kutoka kwa niaba ya  Auma Obama Sauti Kuu nchini Kenya.  Wadau wengine wakubwa katika kampeni hii ni FAO mountain partnership, mfuko wa Benki ya Umoja wa Mataifa UNFCU, kituo cha Afrika cha kuzuia na kudhibiti magonjwa (CDC), Muungano wa chanjo duniani GAVI, AU, mradi wa wanawake  kuhusu akili na mchezo “Women’s Brain na Sport” and Mpango wa  Msaada kimataifa (SI).

Mlima Kilimanjaro Tanzania na Wanyama
Mlima Kilimanjaro Tanzania na Wanyama
19 October 2021, 16:40