Tafuta

Mkutano wa kidiplomasia kuhusu msaada wa mgogoro nchini Afghanistan huko Geneva, Uswiss. Mkutano wa kidiplomasia kuhusu msaada wa mgogoro nchini Afghanistan huko Geneva, Uswiss. 

Mkutano wa UN kuchangisha fedha kwa ajili ya Afghanistan!

Hata hivyo Umoja wa Mataifa unatoa taadhari kuwa huenda kukawa na mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo kufuatia Taliban kuchukua madaraka: Kwa maana hiyo kuna hofu ya mauaji na vurugu katika kulipiza kisasi licha ya ahadi za msamaha nchini Afghanistan.Wakati huo huo unafanyika mkutano kuchangisha fedha kwa ajili ya mgogoro.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Umoja wa Mataifa umefanya kongamano la kuchangisha fedha mjini Geneva mwezi Septemba   kwa ajili ya juhudi zake za kuchangisha zaidi ya dola milioni 600 kwa ajili ya Afghanistan. Hata hivyo Umoja wa Mataifa unatoa taadhari kuwa huenda kukawa na mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo kufuatia Taliban kuchukua madaraka. Kongamano hilo litahudhuriwa na maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Katibu Mkuu Bwana Antonio Guterres na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas. Hata kabla Taliban kuuteka mji wa Kabul mwezi uliopita, nusu ya idadi ya watu nchini Afghanistan au watu milioni 18 walikuwa wanategemea misaada. Umoja wa Mataifa unatahadharisha kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na ukame na uhaba wa fedha na chakula. Mataifa mengi ya kigeni yamesitisha upatikanaji wa misaada ya kifedha kwa ajili ya Afghanistan kufuatia Taliban kuchukua madaraka jambo lililouwekea shinikizo kubwa Umoja wa Mataifa.

Mazungumzo na Taliban na utunzaji wa misaada kwa Afghanistan unahitajikia ili kuepusha mtikisiko wa uchumi ambao unaweza kusababisha mamilioni ya vifo. Huu ndio mwito uliotolewa na Katibu Mkuu wa UN, Bwana Antonio Guterres, katika mahojiano na Gazeti la Ufaransa, wakati Baraza la Usalama likiendelea. “Kwa kuwa hali hiyo haitabiriki tunahitaji kushiriki katika mazungumzo ili Afghanistan kisiwe kituo cha ugaidi na haki zilizopatikana na wanawake zisipotee daima. Kwa sasa ni urusi inaendelea mhakato wa kuhamisha raia wa nchi karibu robo tatu lakini ambayo haitashiriki sherehe ya kuapishwa kwa serikali mpya ya Afghanistan. “Wengi wametuomba  tusaidie kuwaondoa raia wa nchi za kigeni au hata Wafghanistan kutoka eneo la nchi hiyo,  lakini hatufanyi hivyo chini ya meza, tunajadiliana ili kufikia makubaliano na Taliban juu ya baadhi ya makundi ya raia” alisema rais Putin.

Nchini Uturuki pia inazindua tena mada ya mazungumzo: “Tunaamini kuwa kushirikiana polepole na Taliban ndio njia sahihi. Tunahitaji mazungumzo nao ili kuona ikiwa wanatimiza ahadi zao”. Lazima wapate imani yetu kwa kugeuza maneno yao kuwa matendo. Kwa naama hivyo mwakilishi wa kudumu wa Uturuki kwa Umoja wa Mataifa  UN, akiongea katika kikao kilichohusu Afghanistan katika Baraza la Usalama. Serikali ya mpito inajua vizuri kwamba itawajibika kwa ukukaji wa haki za binadamu, hasa ikiwa zinakiuka haki za wanawake na wasichana. Tunahitaji kufuatilia kwa karibu maendeleo katika muktadha huu, ameongeza mwakilishi wa Ankara.

13 September 2021, 15:17