Tafuta

Kwa mujibu wa UNICEF watoto 260elfu wa Haiti hadi sasa wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na tetemeko la Ardhi lililokumba kisiwa hiki na kuacha madhara makubwa. Kwa mujibu wa UNICEF watoto 260elfu wa Haiti hadi sasa wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na tetemeko la Ardhi lililokumba kisiwa hiki na kuacha madhara makubwa. 

Haiti/UNICEF:baada ya mwezi watoto 260,000 wanahitaji msaada

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Umoja wa mataifa la kusaidia watoto UNICEF linasema kuwa baada ya mwezi mmoja,watoto 260Elfu bado wanahitaji msaada wa kibinadaamu.Ili kufikia lengo la kusaidia UNICEF imezindua ombi la dola 73.3 milioni ili kujibu mahitaji ya afya,elimu,maji,usafi wa mazingira,lishe na ulinzi wa watoto kwa miezi sita ijayo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika taarifa yake iliyotelewa tarehe 15 Septemba 2021, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limebainisha kuwa baada ya mwezi mmoja tangu kutokea tetemeko la Ardhi kali  huko Haiti Kusini Magharibi, idadi kubwa ya watu 650 elfu na  miongoni mwao  watoto 260 elfu bado wanahitaji msaada wa kibinadamu. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kanda ya UNICEF wa Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien, Bwana Jean Gough, amebainisha kuwa, watoto wa Haiti bado wanapambana katika kukubali matokeo ya tetemeko la ardhi lililopelekea kuanguka kwa nyumba zao, shule zao, miundo ya kiafya na jumuiya nzima.

Huduma za afya bado zimevurugika kusini magharibi mwa Haiti. Majengo mengi ya hospitali yameharibiwa au kuanguka kabisa. Familia nyingi zilizo na watoto zinaogopa kwenda kwenye vituo vichache vya afya vilivyoachwa vimesimama. Upatikanaji mdogo wa maji safi na huduma msingi za afya zinaweka maisha ya vijana hatarini. Mifumo ya afya inajitahidi hata hivyo kukidhi mahitaji, na watu 12,000 waliojeruhiwa na inakadiriwa vituo vya afya 82 vimeharibiwa au kufutwa kabisa katika idara zilizoathirika zaidi. Hata baada ya mwezi, jumuiya nyingine za vijijini bado haziwezi kupata vituo vya afya vinavyofanya kazi kwa sababu ya miundombinu iliyoharibiwa. Uwezo mdogo wa usafi huko hatarini  kama maambukizi ya majeraha na hatari ya pepopunda. Ukosefu wa huduma za kawaida za kiafya zimeongeza hatari ya vifo vya akina mama na watoto wachanga, kwani wodi nyingi za akina mama na upasuaji hazifikishi vifaa na vigezo vya kujifungua salama. Uwezo wa mamlaka ya afya kuzuia, kutambua na kutibu utapiamlo pia ulidhoofishwa na tetemeko la ardhi.

Maisha huko Haiti baada ya Tetemeko kali
Maisha huko Haiti baada ya Tetemeko kali

Kwa kujibu mahitaji haya yaliyoongezeka, UNICEF inafanya kazi na washirika kutoa dawa muhimu, vifaa vya matibabu na msaada wa lishe, ili kusaidia kuanza tena kwa huduma za afya katika vituo vya afya vilivyoharibiwa au ambavyo vimeanguka kabisa na kuimarisha usimamizi wake. UNICEF imezipatia hata hivyo timu 24 za kliniki vifaa muhimu vya matibabu na dawa ili kutoa huduma za afya na lishe,  ikiwa ni pamoja na kutambua na matibabu ya utapiamlo wa kukithiri  katika manispaa za mbali. Ikiwa familia zilizo na watoto haziwezi kupata vituo vya afya baada ya tetemeko la ardhi, ni muhimu kuleta huduma za afya zinazo okoa maisha kwao ili waweze kuzuia vifo vya watoto, kwa maelezo ya Bwana Gough. UNICEF kwa sasa inajitahidi kuanzisha hata kliniki nyingi zinazotembea katika maeneo ili kuwafanya watoto wawe na afya. Pamoja na maelfu ya familia na watoto wanaohitaji huduma ya matibabu haraka, na kwa maana hiyo hawawezi kusubiri vituo vya afya kujengwa upya.

Maisha huko Haiti baada ya Tetemeko kali
Maisha huko Haiti baada ya Tetemeko kali

Kuhusiana na afya ya mama na mtoto, UNICEF inatoa kipaumbele kwa kuendelea kutoa huduma msingi ya afya kwa watoto na wanawake, kwa kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Afya na Shirika la Afya Ulimwenguni. Katika kipindi cha miezi sita ijayo, UNICEF itasaidia utoaji wa huduma muhimu za afya na lishe, kwa lengo la kufikia watoto na wanawake 251,000, pamoja na kutoa msaada muhimu kutibu magonjwa ya kawaida kwa watoto. Njia nyingine za kiafya ambazo zitapanuliwa kwa kiwango ni pamoja na upanuzi wa chanjo ya kawaida kwa watoto 35,000, utambuzi na utunzaji wa watoto walioathiriwa na utapiamlo sugu;  mipango ya kusaidia kulisha watoto wachanga na watoto wadogo, virutubisho vya ujumuishaji kuzuia utapiamlo na utoaji wa huduma kwa akina mama, watoto wachanga na watoto.

Maisha huko Haiti baada ya Tetemeko kali
Maisha huko Haiti baada ya Tetemeko kali

UNICEF pia itasaidia ujenzi na ukarabati wa hospitali 30 na vituo vya huduma msingi vilivyoharibiwa, na pia mafunzo ya wafanyakazi 3,000 wa vituo vya afya na wafanyakazi wa afya katika kudhibiti na kuzuia, pamoja na kuendelea kwa hatua za kuzuia dhidi ya UVIKO-19 na usambazaji wa vifaa vya kujizuia binafsi.  Na ili kufanya hivyo hata hivyo UNICEF imezindua ombi la dola za kimarekani milioni  73.3 kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi,  kwa kulenga kutoa msaada wa haraka katika maeneo ya afya, elimu, maji na usafi wa mazingira, lishe na ulinzi wa watoto, pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, katika miezi sita ijayo. Hadi sasa ni chini ya 11% ya fedha hizi tu zimepokelewa.

Maisha huko Haiti baada ya Tetemeko kali
Maisha huko Haiti baada ya Tetemeko kali
15 September 2021, 15:40