Tafuta

Shughuli za mapokezi ya wakimbizi katika viwanja vya ndege Shughuli za mapokezi ya wakimbizi katika viwanja vya ndege 

Afghanistan:Jitihada za kuokoa watoto kwa kukaribishwa Italia

Kuanzia tarehe 27 Agosti 2021 hadi mwisho wa safari ya ndege za huduma za msaada wa kibinadamu kati ya Afghanistan na Italia,timu ya ‘Save the Children’, na Chama cha ‘CivicoZero’ Roma wanafanya kazi bila kuchoka katika Kituo cha 5 cha uwanja wa ndege wa Fiumicino,kushiriki shughuli za mapokezi ya wakimbizi wapya 800 na kusaidia familia 37 na watoto 14 wasiondikizwa.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Jitihada za kuingilia kati katika kupokea wakimbizi, zimehitimishwa katika uwanja wa ndege wa Fiumicino, Roma ,Italia ambapo shirika la saidia watoto ‘Save the Children’, wamekuwa bega kwa bega katika shughuli za mapokezi ya wakimbizi wapatao 800 na kuhakikisha uingiliaji binafsi wa familia 37 na watoto 14 wasiosindikizwa na ndugu au jamaa.  Imefunguliwa meza ya kusikiliza kwa ajili ya usaidizi na wapatanishi wa kiutamaduni katika lugha za Kifarsi, Kipashtu na Kidari kwa msaada wa haraka kwa ajili ya watoto na familia wakiwasiliana na vyama na mashirika mahalia. Mpango unahitajika kwa ujumuishaji wa kijamii na kazi, ujumuishaji wa watoto kwa wakati unaofaa na kukaribishwa hata kwa wale wanaofika kupitia njia ya kibalkan.

Kuanzia tarehe 27 Agosti 2021 hadi mwisho wa safari ya ndege za huduma za msaada wa kibinadamu kati ya Afghanistan na Italia, timu ya ‘Save the Children’, shirika la kimataifa ambalo limekuwa likipambana zaidi ya miaka 100 kuokoa watoto walio hatarini na kuwahakikishia maisha ya baadaye, na Chama cha  ‘CivicoZero’ Roma wanafanya kazi bila kuchoka katika Kituo cha 5 cha uwanja wa ndege wa Fiumicino, kushiriki katika shughuli za mapokezi ya wakimbizi wapya 800 wa Afghanistan na kusaidia familia 37 na watoto 14 wasiondikizwa. Wahudumu na wapatanishi wa kiutamaduni wa shirika la Save the Children na CivicoZero Roma walisaidia familia katika awamu za mapokezi, kupata habari za kwanza na mwelekeo, usambazaji na uhamisho wa watu kufika hadi kuondoka jijini Kabul. Jitihada hii kwa namna moja nyeti sana, sio tu kwa ajili ya mkusanyiko mkubwa wa watu kwenye Kituo, lakini zaidi ya yote kwa hali ya kihemko ya watu ambao wamefika tu nchini Italia, hasa waliotikiswa na hali za kutoroka kutoka nchi yao, kwa kutokuwa na uhakika juu ya baadaye na hofu ya hatima ya wapendwa waliobaki Afghanistan. Kwa wengine, hata hofu ya kile walichokipata moja kwa moja kufuatia shambulio la karibu na uwanja wa ndege.

Uingiliaji huo ulifanywa ndani ya mfumo wa Mkataba wa Makubaliano kati ya “Save the Children” na  Zima Moto ya  Mkoa wa Lazio, unaofanya kazi tangu nyakati za tetemeko la ardhi katikati mwa Italia, na sasa inaendelea, kila wakati kwa kushirikiana na Wakala na CivicoZero Roma, pamoja na uanzishaji wa timu ya simu za mikono kwa ajili ya maombi maalum ya msaada kwa watu waliokaribishwa kwenye hoteli kwa kipindi cha karantini kwa sababu ya Uviko 19. Uingiliaji katika awamu ya kwanza ya mapokezi ni mwanzo tu wa njia ya msaada wa muda mrefu ambayo lazima ihakikishwe kwa wanawake, wanaume na watoto ambao wameweza kufikia nchi yetu wakikimbia unyama na vurugu. Kwa kila familia sasa ni muhimu kukuza mpango wa binafsi wa ujumuishaji wa kijamii na kazi. Kwa wavulana na wasichana, hasa walioathiriwa na janga hili, ni muhimu kuhakikisha kuanza tena kwa shughuli za shule, kuandaa shule za kutosha kwa kuingizwa kwao na kukuza uhusiano na wenzao.  Usaidizi wa kisaikolojia unaoendelea pia ni muhimu kwa hali za mazingira magumu, pia kwa sababu ya jeraha kubwa lililopatikana. Na ni muhimu kujiandaa kuwakaribisha wale wanaofika Ulaya kupitia njia ya Kibalkan, mara nyingi hupata vurugu nyingine” kwa mujibu wa Raffaela Milano, Mkurugenzi wa Programu za ‘Save the Children’, nchini Italia na Ulaya.

Kwa kiwango cha kitaifa, kujibu ombi kutoka kwa watoto walio na upweke na familia ambao wamewasili nchini Italia, Save the Children imezindua huduma ya majibu (helpdesk yaan meza ya msaada) ambayo inaweza kuhamasishwa katika serikali za mitaa, huduma za kijamii na afya, vituo vya mapokezi, na pia moja kwa moja na familia zilizokuja Italia. Kwa uhakika huduma hutoa ya upatanishi wa lugha ya kiutamaduni kupitia mtandaoni moja kwa moja katika lugha za Kifarsi, Kpashtu na Kidari, mwongozo na msaada wa kisheria, msaada wa kisaikolojia na kihemko baada ya tukio la kutisha, utambulisho na uwezekano wa kuchukua jukumu la hali hatari zaidi, msaada katika taratibu za kuunganisha tena, kutuma msaada wa vifaa na timu kwenye ikiwa inahitajika

01 September 2021, 15:32