Tafuta

Kuhamishwa kwa wakimbizi wa Afghanistan wakiwa katika ndege ya Ujerumani. Kuhamishwa kwa wakimbizi wa Afghanistan wakiwa katika ndege ya Ujerumani. 

Afghanistan:Ahadi ya Watalebani kulinda hadhi ya wanawake

Kundi la Taliban limesema linataka amani na limeahidi kuwa halitalipiza kisasi dhidi ya maadui zao wa zamani.Kundi hilo pia limesema litaheshimu haki za wanawake kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu.Takwimu za waathiriwa wa tetemeko huko Haiti linazidi 1900,wakati mvua kubwa inanyesha katika pwani ya Haiti iliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Watalebani wamekutana na vyombo vya habari na kusema kuwa hawataki kuona Afghanistan wanaingia katika kambi ya mapambano na kuahidi kuwa halitalipiza kisasi dhidi ya maadui zao wa zamani. Kundi hilo pia limesema litaheshimu haki za wanawake kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu. Nchini China, Urusi na Uturuki wanazungumza nchi hiyo kwa uchaya. Rais wa Marekani, Bwana Biden na Jonson wanakubaliana kwa mkutano wa G7 kwa njia ya mtandao wiki ijayo, wakati Nato inatishia kutoa jibu zito, ikiwa ahadi zilizotolewa na watalebani hazitaheshimiwa. Hata hivyo wanaendelea kuhamisha maelfu ya watu wa Afghanistan kwa upande wa nchi hiyo Magharibi na mjadala mkubwa kuhusu wimbi la wakimbizi hao linaendelea.

Na Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa mataifa kusimamisha mpango wa kuwarudisha makwao raia wa Afghanistan baada ya kundi la Taliban kuchukua madaraka na kusababisha hali ya wasiwasi. Shirika la kushughulikia wakimbizi la UNHCR limezishauri nchi kutowarudisha kwao raia wa Afghanistan, wakiwemo raia wa taifa hilo ambao maombi yao ya kutaka hifadhi yamekataliwa.Msemaji wa UNHCR Shabia Mantoo amewaambia waandishi habari mjini Geneva kuwa, kufuatia kudodora kwa usalama na mzozo mbaya wa kibinadamu nchini Afghanistan, UNHCR imeyahimiza mataifa kusimamisha mipango ya kuwarudisha makwao raia wa Afghanistan.Mantoo amekaribisha hatua ya baadhi ya mataifa ya Ulaya yaliyosimamisha mpango wa kuwarudisha kwa nguvu raia wa Afghanistan, na kuonyesha matumaini kuwa mataifa mengine pia yataiga. Msemaji huyo wa UNHCR amesema hata kabla ya kuanza kwa machafuko ya hivi karibuni, zaidi ya Waafghani 550,000 wamepoteza makaazi yao kutokana na mizozo na ukosefu wa usalama kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu

Mvua za sasa kutokana na kimbungna Grace: Takwimu za waathiriwa wa tetemeko linazidi 1900, wakati mvua kubwa inanyesha katika pwani ya Haiti iliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha vifo vingi zaidi namna hiyo. Idara ya hali ya hewa ya Marekani imesema kuwa kimbunga Grace ambacho kimesababisha mvua hiyo, kinaripotiwa kuelekea Jamaica. Idara hiyo imetahadharisha juu ya kutokea mafuriko na maporomoko ya ardhi katika sehemu ya kisiwa cha Hispania, sehemu iliyopo Haiti na Jamhuri ya Dominica. Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi la hivi karibuni imefikia 1,419 wakati wengine 6,900 wamejeruhiwa katika dhoruba hiyo. Unicef inazungumzia juu ya nusu milioni ya watoto ambao wako hatarini.

Niger: Mauajia ya kinyama kwa raia nchini Niger Magharibi yanashughulia na kundi la kijihadi. Karibia watu 37 ya watu, miongoni mwao kuna watoto 14 na wanawake 4 katika kijiji cha Darey, sio mbali na Mali. Inakabiliwa waathiriwa wote katika mkoa huo  ni zaidi 450 tangu mwanzo wa mwaka.

Shirika la Wakimbizi UNHCR linatoa taarifa kuwa watu 46 kutoka Afrika magharibi wamekufa baharini wakati wanatafuta kuifikia Ulaya wakiwa katika mtumbwi baada ya siku kumi na tano kabla ya kuwaokoa huko Mauritania na manusura saba tu.

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC imesifu nchi ya Zambia kwa makabidhiano ya amani ya madaraka baada ya kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Alhamisi 12 Agosti iliyopita. Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amesema kuwa Zambia inastahili sifa na kuwa taifa la kuiga mfano. Chakwera, Ameiambia jumuiya ya SADC kuwa amani na usalama katika kanda hiyo ya kusini mwa Afrika inategemea kuheshimiwa kwa mifumo ya demokrasia na haki za binadamu. Rais Mteule Hakainde Hichilema alitangazwa mshindi Jumatatu 16 Agosti baada ya kumshinda Rais Edgar Lungu, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka sita.

18 August 2021, 14:37