Tafuta

2021.07.28:Bi Amina J.Mohammed,naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Mkutano wa UN juu ya mifumo ya chakula uliofanyika jijini Roma kwa siku tatu 2021.07.28:Bi Amina J.Mohammed,naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Mkutano wa UN juu ya mifumo ya chakula uliofanyika jijini Roma kwa siku tatu 

Mkutano wa UN juu ya mifumo ya chakula wahitimishwa,lakini kazi inaendelea

Bado kuna mengi ya kufanya ili kutimiza na kutambua mapenzi ya Umoja wa Mataifa ya kubadilisha mfumo wa kilimo wa sasa ili kulisha ulimwengu.Bi Amina J.Mohammed,naibu katibu mkuu wa UN,wakati wa hotuba yake ya mwisho ya siku tatu za kukabiliana kwa pamoja jijini Roma,ana uhakika juu ya hili."Tunaweza kuona glasi ikiwa imejaa zaidi au kidogo,lakini katika miaka michache ijayo bado lazima tuijaze".

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mkutano  wa utangulizi wa Umoja wa Mataifa juu ya mifumo ya chakula umemalizika, lakini kazi iko mbele ambayo itaendelea ya Mkutano katika wiki zijazo za mwezi Septemba huko New York, Marekani ili kutimiza matakwa, nia na kujitolea iliyooneshwa wakati wa siku hizi tatu ambazo hitaji la kazi kadhaa za pamoja kuhusu mipango ya viwango vya kuleta mabadiliko ya uzalishaji na uuzaji wa chakula na kwa  maana hiyo kuweza kufikia lengo la kutokuwa  njaa kama waitavyo “njaa zero”. Kazi ya Mkutano iliyofanyika itakusanywa katika hati na itakuwa mahali pa kuanzia kwa kuweza kulinganisha zaidi wakati wa makabiliano.

Bi Amina J. Mohammed anayo matumaini

“Maono haya yalikuwa ya ujasiri na kazi ilikuwa nyingi ili kufanikisha mkutano huu wa mapema. Ninaondoka Roma nikiwa nimejaa matumaini, alisema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed wakati wa kutoa hotuba yake ya kumalizia mchana tarehe 28 Julai 2021. Akiendelea  Bi Amina alisisitiza kuwa: “Ni kwa kufanya kazi pamoja kwa njia ya  mshikamano tunaweza kuwa na sayari yenye mafanikio”, na  kuzindua  ujumbe maalum kwa watu wa kiasilia ili waweza kuwa wahusika wakuu wa mabadiliko na kurudia umuhimu wa kukuza na kuthamanisha wakulima wadogo. Kila mtu lazima awe katika “chumba” kimoja, alithibitisha na kwamba, tunaweza kutokubaliana, lakini lazima tushirikiane ili kila mtu apate chakula cha kutosha.

MKUTANO WA UN KUHUSU MIFUMO YA CHAKULA
MKUTANO WA UN KUHUSU MIFUMO YA CHAKULA

Bi Amina alisema kuwa: “Mifumo ya chakula ni eneo la kipaumbele kwa kufanya uwekezaji wa mabadiliko na kutusaidia kufanya mabadiliko ambayo yanahitajika. Inahitajika kuanzisha miungano mpya na miungano na kupata ufadhili zaidi”. Naibu katibu mkuu aliwashukuru wale wote waliohudhuria mkutano huo wa utangulizi  ambao umewaona  watu 500 waliohudhuria pamoja na viongozi ambao, alisema, haikuwa rahisi kufikia wakati huu wa shida maalum ya ulimwengu, na uhusiano wa watu 20,000 waliokuwa wanafuatilia mtandaoni ulimwenguni. Hatimaye  shukrani zake maalum zilikwenda kwa serikali ya Italia ambayo iliandaa na kukaribisha tukio hili jijini  Roma.

30 July 2021, 14:44