Tafuta

Earth Overshoot Day: Siku ya kuzidiwa kiasi kikubwa cha matumizi ya maliasili ya sayari. Earth Overshoot Day: Siku ya kuzidiwa kiasi kikubwa cha matumizi ya maliasili ya sayari. 

Imeanza kampeni ya siku 100 ya uwezekano kabla ya mkutano wa Cop26

Tarehe 29 Julai ni siku ya Earth Overshoot kwa ngazi ya kimataifa ambayo imewahi kulinganisha na mwaka jana.Ni siku inayofafanua juu ya matumizi mabaya ya maliasili tuliyopewa.Matumizi ya ardhi na usimamizi wa ardhi huwa na athari kubwa ya maliasili pamoja na maji,udongo,virutubishi,mimea na wanyama.Tangu leo kampeni imeanzishwa ya siku 100 kabla ya mkutano wa Cop26

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Leo tarehe 29 Julai ni Siku ya “Overshoot day, siku ya kuelemewa na uzito wa matumizi mabaya ya rasilimali ya sayari kwa ngazi ya kimataifa ambapo mwaka huu imewahi kufanyika ukilinganisha na mwaka jana iliyofanyika tarehe 22 Agosti kwa sababu ya kuharishwa kutokana na janga la Covid-19.  Kwa mfano, mnamo 1970, siku hiyo iliangukia tarehe 29 Desemba. Kwa njia hiyo Sayari, kama ilivyokuwa ikitokea katika miongo ya hivi karibuni, tangu kesho inaingia kwenye mkopo wa rasilimali za mwaka uliofuata, ikionesha kuwa inazitumiwa vibaya. Kwa mfano vyanzo vya maji katika eneo ambalo limekatwa miti au kuna mmomonyoko vitakuwa na tofauti wa ubora wa maji kuliko katika maeneo ambayo yana miti.

Sisi sote tunaishi, watu binafsi na jamii, kana kwamba tunayo Dunia na nusu kidogo, anakumbusha mfikiriaji katika Jumba la Mawazo la Mfumo wa Ulimwenguni huko Marekani. Miongoni mwa sababu kuu ni kuongezeka kwa alama za kiekolojia (ambazo huhesabu ni ngapi na rasilimali gani ambazo kila mtu hutumia) na ukataji hovyo wa miti. Kulingana na makadirio mengine, tanki la kufikiria linakumbusha, kuwa ili kuahirisha tarehe hiyo, kupunguza nusu ya uzalishaji wa kaboni ulimwenguni, inahitaji kubadilisha Siku ya Overshoot ya Dunia kwa siku 93, au zaidi ya miezi mitatu.

Katika hafla ya Siku ya matumizi mabaya na makubwa ya rasilimaliza za Sayari, kampeni ya Siku 100 za uwezekano zimezinduliwa huko Marekani kwa kuzingatiwa kuwa kuna siku 100 kabla ya kuanza mkutano wa Cop26, ambao ni mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika huko Glasgow kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi 12 Novemba ijayo.

Kwa mujibu wa Diwani Susan Aitken, kiongozi wa Halmashauri ya Jiji la Glasgow, kwa niaba ya Mtandao wa Nyayo za Ulimwenguni na Wakala wa Ulinzi wa Mazingira wa Scotland amejikita kuelezea maandalizi hayo. Hapa kuna mlolongo mrefu kutoka mwaka 1970 hadi 2021. Kwa macho ambayo yanatazama mji wa Glasgow kwa ajili ya mkutano wa  Cop26 wa mwaka huu, Mkutano wa Dunia unao husu Mabadiliko ya Tabianchi, Bi Aitken ameelezea kuwa “Tuna nafasi hapa Glasgow kuonesha ulimwengu kile tunachofanya kwa kuungana pamoja, kama mji kuonesha mabadiliko ya kweli, kukabiliana na hali ya hewa na dharura ya ikolojia. Wacha tuweke sayari yetu kwanza na tufanye”.

29 July 2021, 15:16