Tafuta

Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani UNWTO: Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Utalii Kanda ya Afrika kwa mwaka 2022. Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani UNWTO: Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Utalii Kanda ya Afrika kwa mwaka 2022. 

Tanzania Mwenyeji wa Mkutano wa Utalii Kanda ya Afrika 2022

UNWTO, limeridhia ombi la Tanzania la kuwa ni mwenyeji wa mkutano wa Mwaka 2022 wa masuala ya utalii Kanda ya Bara la Afrika. Hatua hiyo inakuja kufuatia kikao kilichofanyika pembeni baina ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro na Zurab Pololikashvil Katibu mkuu wa UNWTO, katika Mkutano wa Kimataifa wa Utalii Kanda ya Afrika. UVIKO-19 umetikisa utalii.

Na Mwandishi Maalum Windhoek, - Namibia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO), limeridhia ombi la Tanzania la kuwa ni mwenyeji wa mkutano wa Mwaka 2022 wa masuala ya utalii Kanda ya Bara la Afrika. Hatua hiyo inakuja kufuatia kikao kilichofanyika pembeni baina ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro na Zurab Pololikashvil Katibu mkuu wa UNWTO, katika Mkutano wa Kimataifa wa Utalii Kanda ya Afrika. Mkutano huu umefanyika hivi karibuni Jijini Windhoek nchini Namibia. Katibu mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani amekubali yeye binafsi kutembelea Tanzania kwa ajili ya kukutana na hatimaye, kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Kitaifa pamoja na wadau wa utalii nchini Tanzania baada ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 kutikisa kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii duniani.

Katika mkutano huu, ujumbe wa Tanzania umeweza kukutana na wadau mbalimbali wa utalii na hivyo kushirikisha fursa, changamoto na matarajio ya Tanzania katika sekta ya utalii kwa siku za usoni. Imekuwa ni fursa kwa Tanzania kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania. Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO), limekubali ombi la Tanzania na kuiingiza kwenye Mradi wa Utalii wa Umoja wa Mataifa. Nchi nyingine katika mpango huu ni Namibia na Cape Verde, ambazo zimekuwemo kwenye mpango huu kwa muda mrefu. Hii ni nafasi kwa sekta ya utalii nchini Tanzania kutoa fursa za ajira kwa vijana. Huu ni mkutano ambao umewakutanisha Mawaziri kumi na tano wa Utalii kutoka nchi kumi na tano za Bara la Afrika. Ugonjwa wa UVIKO-19 umekuwa ni tishio kubwa sana katika sekta ya utalii. Imekuwa ni nafasi kwa wajumbe kushirikishana hatua za mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19. Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania amesema kwamba, Tanzania mwezi Oktoba 2021 inatarajia kufanya mkutano wa kimataifa wa Utalii na Masoko huko Jijini Arusha.

Ni mkutano utakaowakutanisha wataalam wabobezi kutoka makampuni makubwa duniani yanayojishughulisha na kutangaza vivutio vya utalii sehemu mbalimbali za dunia. Wataalam hao kwa nyakati tofauti wamechangia katika mkutano wa Utalii Kanda ya Afrika. Mkutano huo utakuwa ni wa siku tatu, utakaotoa fursa kwa wadau kujadili mbinu na mikakati ya kukuza na kuimarisha sekta ya utalii baada ya sekta hii kuchechemea kutokana na maafa makubwa yaliyosababishwa na Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19.

Utalii Tanzania
19 June 2021, 09:10