Tafuta

Watanzania wametakiwa kujenga na kudumisha: Umoja, amani, uhuru na upendo, ili Tanzania iweze kuendelea kupeta katika medani mbalimbali za maisha! Watanzania wametakiwa kujenga na kudumisha: Umoja, amani, uhuru na upendo, ili Tanzania iweze kuendelea kupeta katika medani mbalimbali za maisha! 

Watanzania Dumisheni: Umoja, Uhuru, Amani na Upendo!

Serikali inaendelea na kazi na hivi karibuni tutaanza ujenzi wa ofisi mpya za kudumu za Wizara kwa sababu zilizopo zilikuwa za muda tu. Mkakati wa mwendelezo wa kuifanya Dodoma kuwa makao makuu unaendelea. “Serikali imejipanga vizuri kuwahudumia na hakuna kitakachoharibika Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao, yote yaliyopangwa yataendelezwa.”

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, - Dodoma, Tanzania.

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watazania waendeleze utamaduni wao uliodumu kwa muda mrefu wa kushikamana, kupendana na kushirikiana ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa ya amani na utulivu. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo hivi karibuni, baada ya sala ya Ijumaa katika msikiti wa Gaddaf jijini Dodoma. Waziri Mkuu alikuwa akiwasilisha salamu za Rais Samia kwa Watanzania. Amesema Mheshimiwa Rais Samia ana matumaini makubwa na Watanzania wote hivyo amewataka waendelee kuwa watulivu na washiriki katika shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

“Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ana matumaini makubwa kwa Watanzania wote, tuendelee kuliombea Taifa letu na kila mmoja ashiriki katika shughuli za maendeleo na hatua tunayotarajia itafikishwa na sisi wenyewe na tukizingatia haya tutafanikiwa sana.” “Serikali inaendelea na kazi na hivi karibuni tutaanza ujenzi wa ofisi mpya za kudumu za Wizara kwa sababu zilizopo zilikuwa za muda tu. Mkakati wa mwendelezo wa kuifanya Dodoma kuwa makao makuu unaendelea.” Amesema Serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha wananchi wanaendelea kuhudumiwa na kutumikiwa huko huko walipo. “Serikali ipo imara na imejipanga vizuri kuwahudumia na hakuna kitakachoharibika Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao, yote yaliyopangwa yataendelezwa.”

Akizungumzia kuhusu miradi mkubwa ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri kuhakikisha miradi yote inaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa. Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania wamuombee kwa Mwenyezi Mungu Rais pamoja na wasaidizi wake wote ili waendelee kutimiza majukumu yao ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yanatimia. “Tumeanza vizuri, tutaendelea vizuri na tutamaliza vizuri, wananchi tuendelee kumuombea rais wetu ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu aendeee kuwa na afya njema ili atekeleze malengo ya kuwatumikia Watanzania na hakuna kitakachoharibika.” Kadhalika Waziri Mkuu ameedelea kuwasisitiza wazazi na walezi nchini Tanzania kuhakikisha wanawajengea watoto wao msingi wa kufanya ibada kwa kuongozana nao kwenye nyumba za ibada kwa kuwa dini zina nafasi kubwa ya kuwakuza katika maadili mema.

08 April 2021, 16:33