Tafuta

Vatican News
2021.04.23 Papa atebelea kituo cha chanjo kilichomo katika ukumbi wa Paulo Vi katika fursa ya siku wa Somo wake 2021.04.23 Papa atebelea kituo cha chanjo kilichomo katika ukumbi wa Paulo Vi katika fursa ya siku wa Somo wake   (Vatican Media)

Rais Mattarella amtakia heri ya somo wa Papa

Rais Sergio Mattarella wa Jamhuri ya Italia,amemtumia Papa Francisko matashi mema kwa niaba ya watu wa Italia katika siku kuu ya Mtakatifu George somo wake.Anamshukuru kwa Barua yake ya kitume “Candor lucis aeternae”,katika maadhimisho ya miaka 700 tangu kifo cha mshairi Dante Alghieri”maarufu kwa utunzi wa 'Paradiso' yaani mbinguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya siku kuu ya somo wa Papa Francisko, tarehe 23 Aprili 2021, ambapo inaadhimisha siku kuu ya Mtakatifu George shahidi ambaye aliuawa huko Nocomedia kwa kutetea imani yake, Rais Sergio Mattarella wa Jamhuri ya Italia, amemtumia salamu za matashi mema zake: “ Baba mtakatifu, katika fursa ya Mtakatifu George, ninayo furaha ya kukufikishia kwa upendo salamu za furaha kwa niaba ya watu wote wa Italia, kuungana nawe kwa ajili ya matashi mema". Akikumbuka barua ya kitume ya Papa hivi Karibuni. Rais Mattarella ameandika: "Wiki chache zijazo, itakuwa ni fursa ya mwaka wa 700 tangu kifo cha Dante Alighieri. Baba Mtakatifu, kwa mara nyingine umeweza kuonesha tunu ya zawadi ya mtunzi huyo wa Firenze. Ninakushukuru kwa sababu ya kusindikiza mwaka huu muhimu kwa ajili ya Italia katika tafakari nzuri sana ambayo ipo kwenye Barua yako ya kitume  “Candor lucis aeternae”. 

Rais Mattarella kwa namna hiyo ameandika:"Ninapenda kuungana na matashi mema kwamba sura ya Dante Alighieri, “Dhana ya hali ya kibinadamu”, iweze kuangazia safari ya kila mtu na matumaini, hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho bado kinatiwa alama na janga na kusaidia kila mtu kusonga mbele kwa utulivu na ujasiri katika hija ya maisha. Ni kwa roho hii kwamba, katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Somo wako, ninasasisha maoni ya ukaribu wa Waitaliani wote na ya kwangu kwa ajili ya utume mkuu wa kitume wa Utakatifu Wako”. Amehitimisha Rais wa jamhuri ya Italia, kutakia matashi mema Baba Mtakatifu ambaye amefanya kumbu kumbu ya somo wake Mtakatifu George mfiadini.

 

23 April 2021, 16:45