Tafuta

Vatican News
Nchini Malawi walekea kuondoa adhabu ya kifo katika ktiba ya nchi Nchini Malawi walekea kuondoa adhabu ya kifo katika ktiba ya nchi 

Malawi:Nchini Malawi yaelekea mchakato wa kuondoa adhabu ya kifo

Tarehe 28 Aprili 2021,Mahakama ya Katiba ya Malawi ilitangaza adhabu ya kifo kuwa kinyume cha katiba.Kufutia na hilo,Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambayo imekuwa bega kwa bega katika kuwasindikiza inakaribisha kwa shangwe uamuzi huo kuelekea mchakato wa kuondoa adhabu ya kifo nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inakaribisha na kuridhika sana na uamuzi wa Mahakama ya Katiba Malawi ambapo mnamo tarehe 28 Aprili 2021 imetangaza adhabu ya kifo kuwa kinyume cha katiba. Kwa mujibu wao wanabainisha kuwa kwa hakika ni kitendo cha uamuzi wenye msimamo katika mchakato wa kukomesha adhabu hiyo katika nchi hii ya kusini mwa Afrika, 

Mchango wa  Jumuiya ya Mtakatifu Egidio

Katika miezi ya hivi karibuni, hati ya mapendekezo iliwasilishwa kwa serikali, iliyoandaliwa na mchango wa uamuzi wa Jumuiya ya  Mtakatifu Egidio kupitia wakili wao  Alexious Kamangila, kwa ushirikiano na wawakilishi wa chama cha Rudisha na Muungano wa Ulimwengu Dhidi ya Adhabu ya kifo. Hati hii pia ilifurahiwa na kuungwa mkono na Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na ilikuwa ya uamuzi.  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ni kwamba kitendo hiki katika nchi ambayo wao wamo ndani humo kwa miaka mingi wakiwa na  mipango kadhaa kwa ajili ya idadi ya watu, ni sehemu ya kujitoa kwa Jumuiya hiyo katika kusitisha na kukomesha adhabu ya kifo, iliyopelekwa mbele tangu 2005 , pamoja na hiyo kwa ajili ya ubinadamu wa watu walio katika magereza.

Ushirikiano wa asasi za kiraia na harakati nyingine

Hii ni shughuli ambayo ni pamoja na mwamko muhimu wa asasi za kiraia pia juu ya suala la haki ya ukarabati. Miongoni mwa wasindikizwaji wa kwanza kwenye mchakato wa safari ya kampeni nchini Malawi ni mwanaharakati Vera Chirwa, ambaye mara kadhaa alishiriki katika mikutano ya kimataifa ya Mawaziri wa Sheria, iliyohamasishwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio juu ya mada ya kukomeshwa kwa adhabu ya kifo. Katika miaka hii mingi, vitendo kadhaa kwa ajili ya kupendelea marekebisho ya mfumo wa gereza pia vimetekelezwa kwa wakati ambao ufahamu umekua juu ya masuala haya kupitia maadhimisho ya kila mwaka kwenye Miji kwa ajili ya Maisha, miji dhidi ya adhabu ya kifo, harakati ambayo imepata wafuasi wa miji 2,300 ulimwenguni. Kuhusiana na nchi ya Malawi, kwa sasa unasubiriwa kwa hamu uthibitisho wa Bunge la uamuzi wa Mahakama ya Katiba.

30 April 2021, 12:59