Tafuta

Wanawake wa Afrika wakiwezeshwa wanaweza. Wanawake wa Afrika wakiwezeshwa wanaweza. 

Pato la msingi la muda mfupiTBI)linaweza saidia kujikwamua kwa wanawake!

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Maifa(UNDP)Machi 4,2012 inaangazia siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa Machi 8,ambapo imependekeza mkakati wa pato la msingi la muda mfupi(TBI kuwa likitolewa kwa mamilioni ya wanawake katika nchi zinazoendelea linaweza kuwa tija dhidi ya umaskini na hasa kwa wanawake wenye umri wa kufanyakazi kuanzia miaka 15-64 katika nchi zinazoendelea.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Ripoti mpya iliyotolewa tarehe 4 Machi 2021 naShirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) linasema kuwa Pato la msingi la muda mfupi (TBI) likitolewa kwa mamilioni ya wanawake katika nchi zinazoendelea duniani linaweza kuzuia kuongezeka kwa umaskini na kupanuka kwa pengo la usawa wa kijinsia wakati huu wa janga la corona au COVID-19. Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanawake wameathirika zaidi na janga la COVID-19  kuliko wanaume, kwa kupoteza mapato na kuondoka kwenye soko la ajira kwa kiwango kikubwa na baadaye  kugeukia sehemu kubwa ya kazi za malezi au kutoa huduma. Kwa mantiki hiyo ripoti imetoa wito kwa nchi katika kuanzishwa mara moja kwa pato la msingi la muda kwa misingi ya kijinsia kwa ajili ya wanawake maskini na wasiojiweza katika nchi zinazoendelea, huku ikisisitiza kwamba hatua hiyo ya dharura ni muhimu ili kuhakikisha wanawake walioathirika kiuchumi na janga hilo wanaweza kumudu maisha wakati huu wa hanga la corona.

Faida za uwekezaji kwa wanawake ni kusaidia jamii nzima

Akisisitiza zaidi kuhusu suala  hilo, Mtawala Mkuu wa UNDP  Bwana Achim Steiner amesema: “serikali zinaweza kuchukua hatua sasa hivi kuelekeza asilimia 0.7 ya pato lake la taifa ,GDP kila mwezi kwa wanawake wanaokabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi na kijamii, kwa sababu pato la msingi la kila mwezi litahakikisha wanaweza kuishi wakati huu mgumu. Na faida za uwekezaji huo hazitowasaidia wanawake tu na familia zao, kumudu janga hili bali pia zitawawezesha wanawake hao kufanya maamuzi huru kuhusu fedha na chaguo la maisha yao”.

Siku ya wanawake duniani tarehe 8 Machi

Ripoti hiyo iliyotolewa kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa tarehe 8 Machi, imependekeza mkakati huo kwa wanawake wenye umri wa kufanyakazi kuanzia miaka 15 hadi 64 katika nchi zinazoendelea. Ripoti inabainisha kuongeza kuwa kwanza unaweza kutoa usalama na uhakika wa kipato kwa muda mfupi kwa  wanawake milioni 613 wenye umri wa kufanyakazi ambao sasa wanaishi katika umasikini huku wakitengeneza njia ya uwekezaji kwa siku zijazo, na pili utapunguza madhila kwa wanake hadi bilioni 2 katika nchi zinazoendelea Kwa mujibu wa ripoti faida nyingine kubwa ya TBI ni kwamba itapunguza pengo baina ya wanawake na wanaume wanaoishi katika umasikini kwa kuwapa wanawake uhuru wa kiuchumi na kuleta uwiano katika kudhibiti rasilimali ndani ya familia.

Bado pengo la usawa wa kijinsia linaendelea kuwa kubwa

Bwana Raquel Lagunas mkurugenzi wa timu wa masuala ya jinsia kwenye shirika la UNDP ameema: “Pengo la usawa wa kijinsia linaendelea kupitia kutokuwepo uwiano wa kipato na mgawanyo wa kazi, na ingawa TBI sio suluhiso la  moja kwa moja, lakini itawasaidia wanawake kuongeza haki ya chaguo wakati huu wa COVID-19”. Ameongeza kuwa TBI inatoa fursa ya utulivu wa kiuchumi kwa wanawake ili waweze kupanga maisha yao kwa ajili ya matakwa yao, mahitaji yao na kushiriki kikamilifu katika jamii zao.

04 March 2021, 17:55