Tafuta

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador akihutubia hadhira wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Kizazi  cha Usawa Mexico,huko mji wa Mexico Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador akihutubia hadhira wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Kizazi cha Usawa Mexico,huko mji wa Mexico  

Huu ni wakati wa kubadili baadhi ya mila,desturi na kulainisha mifumo dume

Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake,masuala ya kijinsia na vijana ulimwenguni kote wameendelea kusonga mbele katika mchakato wa kufikia lengo la usawa,kuilainisha mifumo dume iliyokita mizizi,kubadili baadhi ya mila na desturi na kuhamisha madaraka na kuwapa wale ambao mara nyingi husahaulika na kunyamazishwa.Amesema hayo Katibu wa Umoja wa Mataifa katika Jukwaa la kizazi cha usawa lililofanyika mji wa Mexico.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres katika  hotuba yake kwenye kongamano la kizazi cha usawa lililoanza tarehe 26 Machi huko  mji mkuu wa Mexico kwa njia ya mtandao amesema: “wanaharakati wa kutetea haki za wanawake, masuala ya kijinsia na vijana ulimwenguni kote wameendelea kusogea mbele katika a mchakato wa kufikia lengo la usawa, kuilainisha mifumo dume iliyokita mizizi, kubadili baadhi ya mila na desturi na kuhamisha madaraka na kuwapa wale ambao mara nyingi husahaulika na kunyamazishwa, kumekuwepo na ushindi mkubwa lakini mchakato unakwenda polepole mno na huu ni wakati wa kubadili hilo.”

Bwana Guterres katika hotuba yake amesema kuwa usawa wa kijinsia ni suala la mamlaka na mamlaka yanasalia mikononi mwa wanaume.  katika maeneo mengi, wazo la usawa wa kijinsia limeshambuliwa. Sheria za ukandamizaji zimerudi, na unyanyasaji wa kutisha dhidi ya wanawake unaongezeka, mambo ambayo ninayalaani kabisa. Na sasa, mshituko wa janga la COVID-19 umehjarubu na kusambaratisha maisha ya mamilioni ya wanawake na wasichana na kuathiri hatua za mafanikio yetu mengi tuliyopata.”  Katibu mkuu akienda mbali zaidi  amesisitiza kwamba, “huu ni wakati wa kujikusanya na kujipanga tena kwa ajili ya kutimiza azma yetu kuunda ulimwengu ulio sawa, wa haki, na endelevu zaidi ambao watu wote wanaweza kutambua haki zao za binadamu bila ubaguzi na bila woga. Na kazi hii ni ya wanawake wote.”  

Bwana Antonio Guterres amesema "ni kwa kina mama wote kila mahali, ambao wanahangaika kujumuisha masuala ya kikazi na mzigo mkubwa unaoongezeka wa kutoa huduma, kwa wasichana kutoka jamii za asili na watoto wakimbizi, kwa mwanamke anayeishi na ulemavu au anayesa ka ajira katika masuala ya teknolojia na sayansi, kwa wanawake watetezi wa haki za binadamu na wengine wengi. Kazi hii ni kwa ajili ya wote na lazima ifanywe na wote wanawake na wanaume vilevile.”

Tunapojikwamua kutoka katika janga la COVID-19 Katibu Mkuu amesisitiza kwamba ni, lazima tuzingatia hatua tano muhimu: “Kwanza, linda haki sawa za wanawake na ufute sheria za kibaguzi.  Pili, hakikisha uwakilishi sawa kuanzia katika bodi za kampuni hadi mabunge na zaidi kupitia hatua maalum na nafasi za upendeleo. Tatu, ongeza ujumuishaji wa wanawake kiuchumi kupitia malipo sawa, ulinzi wa kazi, mikopo inayolengwa na uwekezaji katika uchumi wa huduma na hifadhi ya jamii.  Nne, mara moja weka mipango ya hatua za dharura kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.  Tano, toa nafasi kwa kipindi cha mpito cha kizazi kinachoendelea na kwa vijana ambao wanatetea ulimwengu ulio na haki zaidi na sawa”.

Katibu mkuu aidha ameweza kukumbusha yafuatayo kwamba: “wakati tutakapofika Paris mnamo Juni ijauo, tunataka kuona ahadi thabiti na uwekezaji mezani, na harakati imara za wadau mbalimbali kwa ajili ya usawa wa kijinsia. Utambuzi wa haki sawa za nusu ya idadi ya watu wote duniani ni mapigano ya haki za binadamu ambayo haijakamilika ya karne hii.” Kongamano hili la kizazi cha usawa limeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women kwa msaada mkubwa wa serikali za Mexico na Ufaransa ambako kutafanyika sehemu ya pili ya kongamano hili mwezi Juni mwaka huu.  Pia wadau wengine mbalimbali wamesaidia kuwezesha kongamano hilo.

31 March 2021, 14:04