Tafuta

CONGO-DRC CONGO-DRC 

Congo Drc:hakimu ambaye alikuwa akichunguza kifo cha Attanasio ameuawa !

Shambulio hilo lilifanyika katika barabara hiyo hiyo ambapo balozi wa Italia, na Afisa wake na dereva wa msafara waliuawa mnamo tarehe 22 Februari12021.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Damu zaidi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Drc bado inamwagika. William Assani, hakimu wa jeshi ambaye alikuwa akichunguza shambulio ambalo balozi wa Italia Bwana Luca Attanasio, Afisa wake Vittorio Iacovacci na dereva wa Congo Mustafa Milambo waliofariki mnamo tarehe 22 Februari 2021 iliyopita, ameuawa katika shambulio kwenye barabara hiyo hiyo, ambayo inaunganisha Rutshuru huko Goma. Shirika la habari la kimisionari Fides limeripoti, huko likitoa mfano wa vyanzo habari za kimisonari vya huko.

Hata hivyo vyanzo vya habari za ndani vinatangaza kwamba hakimu alikuwa akirudi kutoka kwenye mkutano huko Goma, kama sehemu ya uchunguzi juu ya usalama wa eneo hilo na hasa juu ya mauaji ya balozi wa Italia na wenzake wawili”, linaandika shirika la Fides, likinukuu vyanzo vya wamisionari wanaotoa huduma huko  Kivu Kaskazini, ambapo Goma ni mji mkuu wake. Katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari za kimisionari Fides, Kituo cha Mafunzo ya Amani, Demokrasia na Haki za Binadamu (Cepadho) kinathibitisha kupata mshtuko mkubwa kuuawa kwa Meja William Assani, hakimu wa Mahakama ya Kijeshi ya Rutshuru, ambaye amebaki mwathirika karibu na Katale, kwenye mhimili wa barabara ya Rutshuru - Goma, alikokuwa akitokea. Uhalifu huu ulifanywa na watu wasiojulikana wenye silaha, ambao inawezekana si Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, taarifa inabainisha.  Hata hivyo katika harakati za kutafuta walihusika na mpango wa mauaji hayo ukiendelea, serikali ilikuwa imesema kuwa itafanya kila njia kugundua ni nani ambaye yuko nyumba ya uhalifu huo.

Kulaani tendo hili lililotekeza na kutaka haki kwa ajili ya waathiria ndiyo Chama cha Amani ya Kristo kimataifa (Pax Christi International) kimethinitisha kufuatia na kifo cha aliyekuwa balozi wa Italia Bwana Luca Attanasio, Afisa wake na Vittorio Iacovacci na dreva Mustapha Milambo, wa Shirika la Mpango na Chakula,waliouwawa tarehe 22 Februari huko Goma, Congo DRC. Chama hili cha Amani ya Kristo Kimataifa (Pax Christi International) na wanachama wake katika eneo la Maziwa Makuu wanalaani vikali kitendo hiki cha kudharaulika na kuitaka serikali mahalia  iwafikishe wenye hatia mahakamani. Chombo hiki aidha  kimebainisha kuwa  kila wiki kuna mashambulio na upotezaji wa maisha ya watu wasio na hatia nchini humo ,  na kwamba ni janga la ujanja ambalo limevamia eneo lote la Congo katika miaka thelathini iliyopita na ambalo kwa sasa halimwachi mtu yeyote. Kiukweli iwe  katika vijiji na katika miji kuna mauaji, utekaji nyara, wizi wa kutumia silaha na vitendo vingine vya vurugu, wakati huo huo vikundi vyenye silaha pia vispora mali za idadi ya watu kila wakati, na kusababisha wahanga wengi, ripoti hiyo inasisitiza.

05 March 2021, 15:59