Tafuta

Ukame wa kukithiri nchini Angola kufuatia na ukosefu wa mvua. Ukame wa kukithiri nchini Angola kufuatia na ukosefu wa mvua. 

Angola imekumbwa na ukame mkubwa

Kwa mjibu wa Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) mjini Geneva,Uswisi Tomson Phiri amewaambia waandishi wa Habari kuwa hali ya hewa ya ukavu isiyo ya kawaida nchini Angola inakwamisha msimu wa mvua ambao mara nyingi huanzia mwezi Aprili hadi Novemba na kusababisha ukame wa kupindukiia, kwa maana hiyo na matokeo yake.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linaonya hivi karibuni kuwa kiwango cha njaa kinazidi kuongezeka nchini Angola wakati huu ambapo taifa hilo la kusini mwa Afrika linakumbwa na ukame ambao haujawahi kushuhudiwa kwa miongo minne katika majimbo ya kusini magharibi mwa nchi hiyo. Kwa mjibu wa Msemaji wa WFP mjini Geneva, Uswisi Tomson Phiri amewaambia waandishi wa Habari kuwa hali ya hewa ya ukavu isiyo ya kawaida inakwamisha msimu wa mvua, ambao mara nyingi huanzia mwezi Aprili hadi Novemba.

Kiongozi huyo amesema ukame umeshamiri nchini humo tangu mwezi Desemba mwaka jana na majimbo ya Cuanza Sul, Benguela, Huambo, Namibe na Huila kupata kiwango kidogo cha mvua na kwamba hali haitarajiwi kuwa bora hivi karibuni. Bwana Phiri amesema kadri kiwango cha maji kinavyopungua, mazao yaanathirika na kuna uwezekano wa kupoteza hadi asilimia 40 ya mazao sambamba na hatari ya wananchi kushindwa kuendelea kutunza mifugo yao na sasa familia zinahamahama kuelekea majimbo mengine na nchi jirani ya Namibia.

Kwa sasa shirika la Mpango na Chakula WFP linaratibu tathmini za uhakika wa upatikanaji wa chakula na lishe kwenye maeneo hayo ya kusini mwa Angola, tathmini ambayo itapatikana mwishoni mwa mwezi wa Mei. Shirika hilo limekuwa likisaidia serikali ya Angola kwenye maeneo ya mgao wa mlo shuleni, tathmini za hatari katika mwelekeo wa chakula na lishe na limesema litaendelea kufuatilia kwa karibu hali ilivyo na kutoa msaada wa kiufundi kwa kuzingatia mahitaji na mapengo yaliyopo.

29 March 2021, 13:39