Tafuta

Vatican News
Chanjo dhidi ya COVID-19  imefika nchini  Ivory Coast Chanjo dhidi ya COVID-19 imefika nchini Ivory Coast  (ANSA)

Toeni haki milki ili nchi kusini mwa dunia ziwe na haki ya kutengeneza chanjo!

Washiriki wa bodi ya WTO wanapaswa kufikiria kutoa misamaha muhimu katika masuala ya haki miliki ili kila mtu awe na haki ya utengenezaji. Wameonya juu ya vitisho katika vita dhidi ya janga la corona kama vile mapungufu kwa nchi katika kujikwamua na kuzuka kwa aina mpya za virusi vya corona au Covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jopo la wataalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ambao wamehimiza ushirikiano mkubwa katika fursa za kupata chanjo za COVID-19 ulimwenguni kote, huku wakiweka wazi hali halisi ya mgawanyiko, pengo la usawa na maslahi ya kitaifa na ya kikanda katika chanjo hizo. Ni ombi kuelekeza kwa shirika la biashara duniani (WTO) . Jopo la wataalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa tarehe Mosi Machi  2021 wametoa ombi  kwa wajumbe wa shirika la biashara duniani (WTO) kufikiria kuondoa masharti katika utengenezaji chanjo dhidi ya corona au COVID-19 kwa lengo la kutoa ulinzi kwa wale walio maskini kabisa duniani. Wataalam hao wametoa ombi hilo kwenye mkutano wa WTO unaoendelea mjini Geneva Uswis ukijadili masuala ya haki miliki. Katika ombi alao wamehimiza ushirikiano mkubwa katika fursa za kupata chanjo za COVID-19 ulimwenguni kote, huku wakiweka wazi hali halisi ya mgawanyiko, pengo la usawa, na maslahi ya kitaifa na ya kikanda katika chanjo hizo.

Jopo hili aidha wameongeza kusema  kuwa “Mabilioni ya watu hususan katika mataifa Kusini mwa dunia wanauwezekano mkubwa wa kuondolewa katika faida za chanjo dhidi ya COVID-19 hadi mwaka 2024 na hii si haki. Tunaziomba nchi zilizoendelea kukomesha utaifa na ubinafsi katika chanjo ambavyo vimekuwa vikichochea mgawanyiko na kuathiri juhudi za kujikwamua na janga hili ulimwenguni kote”. Mwezi Machi Shirika la biashara duniani, WTO linawaleta pamoja wataalam wa baraza la makubaliano kuhusu masuala ya biashara yanayohusiana na haki miliki kujadili changamoto mbalimbali zinazohusiana na suala la haki miliki. Kundi hilo la wataalam wa haki za binadamu limesema mkakati wa kimataifa wa chanjo COVAX, ni hatua muhimu kuelekea utaratibu maalum wa kusambaza chanjo duniani kote.

Kwa wataalam hao “washiriki wa bodi ya WTO wanapaswa kufikiria kutoa misamaha muhimu katika masuala ya haki miliki ili kila mtu awe na haki ya utengenezaji.” Wameonya juu ya vitisho katika vita dhidi ya janga la corona kama vile mapungufu kwa nchi katika kujikwamua na kuzuka kwa aina mpya za virusi vya corona. Changamoto hizi zimekuja baada ya juhudi za wanasayansi, mataifa na asasi za kijamii kupata chanjo. Shirika la afya duniani WHO linakadiria kwamba asilimia 95 ya chanjo hizo zinatolewa katika nchi 10 tajiri. Na jopo hilo la wataalam linasema “Hili ni dhihirisho la kushindwa kutoa ushirikiano ambao unaathiri haki ya maendeleo kwa kila mtu na kwa watu wote.” Wameongeza kuwa kwa mtazamo wao ingawa mkakati wa COVAX unaoongozwa na shirika la afya duniani WHO ni hatua muhimu kuelekea uratibu wa kusambaza chanjo mataigfa hayajihusishi ipasavyo na vya kutosha katika lengo hilo. COVAX inapanga kusambaza angalau dozi bilioni 2 za chanjo dhidi ya COVID-19 kote duniani. Kwa mujibu wa wataalam hao “ubinafsi katika chanjo utaweka hataribi mchakato wa kufikia lengo la madendeleo endelevu namba 3 na pia kuathiri uwezo wa nchi kutafsiri lengo hilo katika njia ambazo zinasaidia mahitaji yao ya maendeleo na mbinu za kukabiliana na janga hilo.”

Wataalam hao wanaamini kwamba wajumbe hao tisa wa bodi, makubaliano yanaweza na yanapaswa kusaidia kulinda afya ya umma katika kiwango cha kimataifa na kuhamasisha wanachama wote kujitosheleza na kutokuwa kikwazo cha fursa ya dawa na chanjo za COVID-19. Wataalam hao pia wamesema janga la COVID-19 ni changamoto ya kimataifa ambayo inaweza kutatuliwa tu kwa kupitia juhudi na hatua za pamoja. wamesisitiza kwamba "maneno matupu na ukosefu halisi wa kujitolea kwa ufikiaji wa chanjo kwa wote na usawa haviwezi kuokoa maisha au kulinda walio hatarini zaidi”. Wito mwingine kwa nchi ni kujitolea zaidi kwa ushirikiano wa maana, kama jukumu na sio chaguo, kuzuia ucheleweshaji wa usambazaji wa chanjo kwa watu walio katika mazingira magumu ulimwenguni, na sio kuwaacha nyuma.”

02 March 2021, 14:14