Unicef:bado mauaji ya watoto nchini Siria yanaendelea kutokana na mashambulizi
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Kulingana na ripoti kutoka ofisi za UNICEF, kuhusiana na nyanja hiyo msichana wa miaka 12 aliuawa Jumapili tarehe 31 Januari katika shambulio huko Azaz, kaskazini mwa eneo la vijijini la Aleppo. Watoto wengine wawili ni miongoni mwa makumi ya waliojeruhiwa, mmoja wao akiwa chini ya mwaka mmoja. Siku mbili zilizopita, watoto watatu walifariki katika mlipuko katika mji wa Afrin, pia kaskazini mwa eneo la vijijini la Aleppo. Amesema hayo Bwana Andrea Iacomini, msemaji wa UNICEF nchini Italia.
Kwa mujibu wa msemaji huoyo amesema “Mashambulio haya ya hivi karibuni, kwa huzuni yanatukumbusha kuwa vurugu zinaendelea nchini Sria na kwamba watoto wanaendelea kuwa katika hatari siku baada ya siku. Tangu mwanzo wa mwaka huu, watoto wasiopungua 22 wameuawa. Ni mauaji ya kusikitisha ambayo yamedumu muda mrefu miaka 10”.
Kwa mara nyingine, UNICEF inawakumbusha wahusika wote kwenye mzozo majukumu yao ya kulinda watoto wakati wote na kujiepusha na vurugu katika maeneo ya raia. Miaka kumi baada ya kuanza kwa mzozo, watoto wanaendelea kuathiriwa zaidi na uharibifu usiokuwa wa kawaida, makazi yao na vifo. Wamepoteza maisha, nyumba na utoto. Wakati umefika sasa wa ghasia nchini Siria kuisha, amehitimisa msemaji huyo.