Tafuta

Vatican News
2018.12.22 Mpango wa shule huko Rumbek nchini Sudan Kusini, unaoendeshwa na watawa Walasalliani (La Salle) 2018.12.22 Mpango wa shule huko Rumbek nchini Sudan Kusini, unaoendeshwa na watawa Walasalliani (La Salle) 

Siku ya Kimataifa ya Elimu:sehemu kubwa ya maudhurio ya masomo duniani imepotea sababu ya COVID-19

Katika mtazamo kwa ujumla wa Elimu ulimwenguni katika fursa ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Elimu tarehe 24 Januari,UNESCO imeangazia madhara ya Covid-19 yaliyokwamisha pakubwa Elimu.Tangu kuzuka kwa janga hilo zaidi ya wanafunzi milioni 800 wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuvurugiwa mpango wa elimu yao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni mwaka mmoja tayari umetimia  tangu kuzuka kwa janga la corona au COVID-19, ambapo kwa mtazamo wa madhara yake makubwa, zaidi ya wanafunzi milioni 800 ambao ni zaidi ya nusu ya wanafunzi wote duniani bado wanakabiliwa changamoto kubwa ya kuvurugwa kwa elimu yao, kuanzia kufungwa kwa shule katika nchi 31 hadi kupunguzwa au kusoma kwa muda mfupi katika nchi zingine 48 kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa tarehe 24 Januari 2021 kupitia ramani ya ufuatiliaji ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na utamaduni UNESCO.

Elimu ni haki ya binadamu, faida ya umma na jukumu la umma. Haki ya kupata elimu imewekwa katika kifungu cha 26 cha Azimio la Ulimwengu la Haki za Binadamu, ambapo elimu ya msingi lazima iwe bure na ya lazima kwa Mkutano wote wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Mtoto na Kijana, uliopitishwa mnamo 1989, unapita zaidi ya sharti hili kwa kuanzisha kwamba nchi lazima pia zifanye elimu ya juu kupatikana kwa wote. Mnamo mwaka wa 2015, wakati Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu ilipopitishwa, jamuiya ya kimataifa ilitambua elimu kama msingi, bila kwayo kufanikiwa kwa malengo yake yote 17 haingewezekana. Hasa, Lengo la Maendeleo Endelevu namba 4 linalenga kutoa elimu bora, yenye usawa na jumuishi, na fursa za kudumu za kujifunza kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Tukirudi katika takwimu zilizotolewa na UNESCO ambazo zimechapishwa katika siku ya kimataifa ya elimu katika ramani hiyo zinaonyesha kwamba, duniani kote shule zilifungwa kabisa kwa wastani wa miezi 3.5 sawa na wiki 14 tangu kuzuka kwa janga la COVID-19. Katika maeneo mengine takwimu zimeongezeka hadi miezi 5.5 sawa na wiki 22 ambazo ni theluthi mbili yam waka mzima wa masomo ukizingatia muda wa kawaida wa shule kufungwa.

Kwa mujibu wa twimu hizo za UNESCO kumekuwa na tiofauti kubwa za muda wa ufungaji shule baina ya kanda kuanzia miezi 5 (wiki 20) za wastani wa kufungwa shule kabisa nchi nzima Amerika ya Kusini na nchi za Caribbea hadi miezi 2.5 (Wiki 10) kwa nchi za Ulaya na mwezi mmoja tu kwa Ocenia. Tofauti hiyo imedhihiria pia wakati wa kuangalia muda wa kawaida wa ufungaji shule ambao unaanzia wastani wa miezi 7 (wiki 29) kwa nchi za Amerika ya Kusini na Caribbien  ikilinganishwa na wastani wa miezi 5.5 (wiki 22) kwa maeneo mengine duniani.

Hata hivyo tawimu hizo za ramani ya ufuatiliaji ya UNESCO zinaonyesha kuwa serikali zimejitahidi kupunguza ufungaji shule nchi nzima kutoka nchi 190 wakati wa kilele cha maambukizi ya COVIDF-19 mwezi Aprili 2020 na kufikia nchi 30 leo hii ambapo nchi nyingi zinaunga mkono kufunga sehemu tu ya masomo au kufunga kutokana na maeneo athirika zaidi katika kiala nchi. Hadi sasa shule zimefunguliwa kikamilifu katika nchi 101 tu duniani.

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO,  Audrey Azoulay akizungumzia suala la kufunga shule amesema: “Ufungaji shule wa muda mrefu na wa kujirudia unasababisha ongezeko la athari za kisaikolojia na kijamii kwa wanafunzi, unaongheza kupotea kwa muda wa kujifunza na hatari ya Watoto kuacha shule, na unaathiri kwa kiasi kikubwa jamii zisizpojiweza na zilizo hatarini zaidi. Hivyo ufungaji wa shule kabisa ni lazima uwe suluhu ya miwsho na kufungua shule hizo kwa usalama ndio kiwe kipaumbele.”

Twakimu hizo ambazo zimeandaliwa na kutolewa kitengo cha UNESCO cha ripoti ya kimataifa ya ufuatiliaji wa elimu zinaonyesha kwamba hata kabla ya janga la COVID-19 ni nchi 1 tu kati ya 5 ndio iliyoonyesha hatua kubwa katika usawa wa elimu kupitia mikakati ya ufadhili na kuna ushahidi kidogo sana wa kuwepo usawa katika mikakati ya kukabiliana na COVID-19. Kwa maana hiyo Azoulay amesema“Tunahitaji mkakati uliofadhiliwa wa kujikwamua ili kuweza kufungua shule kwa usalama, tukiwalenga wenye mahitaji zaidi na kuirejesha elimu katika mstari unaotakiwa kwa kizazi cha COVID-19. Leo katika siku ya kimataifa ya elimu natoa wito kwa nchi na washirika wetu kutoa kipaumbele kwa elimu , kwa faida ya dunia nzima katika kujikwamua na janga hili.”

Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa janga la COVID-19 litaongeza pengo la ufadhili wa elimu kwa theluthi moja na kugfikia dola bilioni 200 kwa mwaka katika nchi za kipato cha chini na cha kati ambalo ni saw ana asilimia 40 ya gharama zote za elimu. Na ili kuwezesha wanafunzi kurejea salama mashuleni UNESCO imetoa wito kwa walimu na waelimishaji milioni 100 kote duniani kupewa kipaumbele katika kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19.

01 February 2021, 12:25