Tafuta

Barani Afrika na maambukizi ya Covid Barani Afrika na maambukizi ya Covid 

Kuna ongezeko la maambukizi ya Covid-19 barani Afrika!

Shirika la afya la Umoja Ulimwenguni (WHO),linasema kuwa kwa hali ya sasa,mifumo bora ya afya inahitajika zaidi kuliko wakati wowote ule ili kudhibiti uwezekano wowote wa kuenea kwa maambukizi ya virusi na hasa mnyambuliko mpya wa virusi vya Corona.Hali mpya imeanza kongezeaka zaidi barani Afrka katika awamu ya pili kuliko awamu ya kwanza.

Na Sr. Angela Rwezaula,-Vatican.

Mkurugenzi wa  Shirika la Afya duniani (WHO) kwa kanda ya Afrika Dk. Matshidiso Moeti amesema “wastani wa wagonjwa wapya 25,223 waliripotiwa kila siku kati ya tarehe 28 Desemba 2020 na tarehe 10 Januari 2021 barani Afrika,” ikiwa ni ongezeko la asilimia 39 ikilinganishwa na wagonjwa 18,104 waliokuwa wakiripotiwa kila siku kwenye wiki mbili za mwezi Julai mwaka 2020, kipindi ambacho idadi ya wagonjwa ilikuwa juu zaidi barani Afrika. Na hii ni kutokana na mnyumbuliko mpya wa virusi vinavyosabaisha Corona au Covid-19, barani Afrika  ambao umeanza kuenea wakati huu ambapo idadi ya wagonjwa wa virusi wa Corona imefikia milioni 3 na ile ya wagonjwa wapya kila siku ikizidi ile iliyokuwepo wakati wa awamu ya kwanza ya gonjwa hilo.  Shirika la afya la Umoja Ulimwenguni (WHO), linasema kuwa kwa hali ya sasa, mifumo bora ya afya inahitajika zaidi kuliko wakati wowote ule ili kudhibiti uwezekano wowote wa kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo ambayo yanaweza kudidimiza zaidi mifumo ya afya ambayo tayari imezidiwa uwezo.

Mkurugenzi wa  Shirika la Afya duniani wa WHO kanda ya Afrika Dk. Matshidiso Moeti amesema “wastani wa wagonjwa wapya 25,223 waliripotiwa kila siku kati ya tarehe 28 Desemba 2020 na tarehe 10 Januari 2021 barani Afrika,” ikiwa ni ongezeko la asilimia 39 ikilinganishwa na wagonjwa 18,104 waliokuwa wakiripotiwa kila siku kwenye wiki mbili za mwezi Julai mwaka 2020, kipindi ambacho idadi ya wagonjwa ilikuwa juu zaidi barani Afrika. Mnyumbuliko mpya wa virusi vya Corona, 501Y.V2 umeripotiwa nchini Afrika Kusini, ukitajwa kubainika zaidi kwa wagonjwa wapya wakati huu wa awamu ya pili ya maambukizi ya Corona.  Ingawa virusi hivyo vinasambaa kwa urahisi zaidi na tayari vimebainika Botswana, Gambia na Zambia, bado hatari yake si kubwa sana kama aina ya awali, SARS-CoV-2 japokuwa si hatari lakini lazima  kuchukue hatua wanasisitiza

Dk. Moeti akizungumza kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao amesema uchunguzi zaidi unafanyika kuelewa madhara ya mnyumbuliko huo mpya. “Hata kama mnyumbuliko huo mpya madhara yake si makubwa kama ya awali, bado virusi hivyo vinaweza kusambaa rahisi na kudhoofisha mifumo yetu ya afya hospitalini ambako tayari huduma zimezidiwa uwezo. Hili ni kumbusho kwamba virusi hivi bado vipo na ni tishio na kwamba vita dhidi yake bado havijaisha,” amesema Dk Moeti. Ni kwa mantiki hiyo Mkurugenzi huyo wa WHO kanda ya Afrika ametoa wito kwa nchi za Afrika kuongeza uwezo wao wa uchunguzi dhidi ya virusi hivyo na kusambaratisha mnyumbuliko mpya wa COVID-19 punde tu unapobainika kwenye nchi zao.

Tuelewe vyema 501Y.V2: Akifafanua zaidi amesema ili kudhibiti ni lazima kutambua vyema aina yake, mnyumbuliko na tabia zake na kwamba “tusibweteke. Lazima tuwe macho kwa kuweka mikakati bora ya afya ya umma itakayosaidia kudhibiti kuenea kwa virusi hivi, kwa kuzingatia hatua zile tulizotumia na kudhibiti wakati wa awamu ya kwanza ya kuenea kwa COVID-19 kama vile  kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka michangamano na mikusanyiko na kuvaa barakoa kwenye maeneo yenye watu wengi.”

15 January 2021, 16:00