Tafuta

Ajali ya Treni huko Kigwe-Bahi, Dodoma, Tanzania imesababisha vifo vya watu 3 na wengine 66 kujeruhiwa na kwa sasa wanaendelea na matibabu kwenye Hospitali za Bahi na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Ajali ya Treni huko Kigwe-Bahi, Dodoma, Tanzania imesababisha vifo vya watu 3 na wengine 66 kujeruhiwa na kwa sasa wanaendelea na matibabu kwenye Hospitali za Bahi na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. 

Ajali ya Treni Dodoma: Watu 3 Wamefariki Dunia; Majeruhi ni 66 Wanatibiwa!

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jumapili tarehe 3 Januari 2021 amewatembelea na kuwafariji majeruhi 66 waliopata ajali ya Treni kati ya Kigwe na Bahi na kusababisha watu watatu kupoteza maisha yao. Hawa ni mtoto mmoja na watu wazima wawili. Uchunguzi wa chanzo cha ajali hii unaendelea kufanyika na Shirika la Reli Tanzania, TRC litaendelea kutoa taarifa rasmi.

Shirika la Reli Tanzania, TRC., - Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Jumapili tarehe 3 Januari 2021 amewatembelea majeruhi 66 waliopata ajali ya Treni na kusababisha watu watatu kupoteza maisha yao. Hawa ni mtoto mmoja na watu wazima wawili. Treni iliyohusika na ajali ni B17 na kichwa cha Treni ni chenye namba 9004. Mabehewa 6 ndiyo yaliyopata ajali. Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Unasikitika Kutangaza tukio la Ajali lilitokea Maeneo ya Kigwe-Bahi umbali wa Kilomita 508 Kutokea Dar Es Alaam na Kilomita 58 Kutokea Dodoma, Treni hiyo ilikuwa inatokea jijini Dar Es Salaam ikielekea Mikoa ya Tabora, Katavi (Mpanda), Kigoma na Mwanza ikiwa na Abiria wapatao 720. Treni hii iliwasili Dodoma majira ya saa 9:15 alasiri na Kuondoka Dodoma majira ya Saa 11:40 Jioni. Treni hii iliwasili katika kituo cha Kigwe majira ya saa 12:25 Jioni na Kuondoka saa 12:27 Jioni.

Treni hii ilikuwa na Behewa 12 na kati yake Behewa 6 ndizo zilipata ajali Usajili wake ni kama ifuatavyo:

TCB 3603 ya kwanza kutoka kwenye kichwa cha Treni

TCB 3612 ya Pili kutoka kwenye kichwa cha Treni

TCB 3652 ya tatu kutoka kwenye kichwa cha Treni

TCB 3650 ya Nne kutoka kwenye Kichwa cha Treni

TCB 3619 ya Tano kutoka kwenye Kichwa cha Treni

Na ya Mwisho ni yenye Usajili wa Na. RCB 4526.

Mpaka Jumapili tarehe 3 Januari 2021 Majeruhi ni 66 na waliopoteza maisha ni watatu (3), akiwemo mtoto mmoja (1) na watu wazima wawili (2). Majeruhi wamekwisha chukuliwa eneo la Tukio na wanaendelea na matibabu katika Hospitali za Bahi na hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Uchunguzi wa Chanzo cha ajali unaendelea kufanyika na Shirika litaendelea kutoa Taarifa. Uongozi wa Shirika la Reli unatoa Pole kwa Abiria wote waliofikwa na ajali, Majeruhi na Ndugu na Jamaa waliopoteza Wapendwa wao.

03 January 2021, 11:52