Tafuta

Wazamiaji kutoka Jeshi la Majini nchini Indonesia wanaendelea kutafuta "Visanduku vyeusi" vitakavyosaidia kubaini chanzo cha ajali kilichopelekea watu 62 kupoteza maisha baada ya ndege kukosa mwelekeo na kuzama baharini. Wazamiaji kutoka Jeshi la Majini nchini Indonesia wanaendelea kutafuta "Visanduku vyeusi" vitakavyosaidia kubaini chanzo cha ajali kilichopelekea watu 62 kupoteza maisha baada ya ndege kukosa mwelekeo na kuzama baharini. 

Ajali ya Ndege Indonesia, Abiria 62 Wafariki Dunia! Majonzi Makubwa!

Ndege hii aina ya SJ 182 ilikuwa na wafanyakazi 12 na abiria 50, wakiwamo na watoto 10. Indonesia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameanza kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hii ambayo imesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Wasiwasi mkubwa ni kuhusu usalama wa aina hii ya ndege ambayo imekuwa ikifanya safari zake kwa muda wa miaka 27 sasa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Wazamiaji kutoka Jeshi la Majini nchini Indonesia wanaendelea kutafuta “visanduku vyeusi” (Black boxes), ili kupata habari zaidi kuhusu kilichopelekea kuanguka na hatimaye, kuzama kwa Ndege ya Shirika la Sriwijaya Air, iliyopata ajali hivi karibuni na kusababisha watu 62 kupoteza maisha, muda mfupi tu, tangu iliporuka kutoka katika Kiwanja cha Ndege cha Jakarta nchini Indonesia. Juhudi hizi zinakwenda sanjari na kutafuta miili ya watu waliopata ajali katika ndege hii iliyokuwa inafanya safari yake kuelekea mjini Pontianak, kwenye Kisiwa cha Borneo, kilometa 749 kutoka Jakarta. Hii ni ajali ya pili kutokea nchini Indonesia katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Itakumbukwa kwamba, kunako mwaka 2018 Shirika la Lion Air Boing 737 MAX ilipoteza mwelekeo na hatimaye, kutumbukia baharini, ikiwa na abiria 189, wakati wa safari yake kutoka Kiwanja cha ndege cha Soekarno-Hatta.

Taarifa rasmi zinaonesha kwamba, Jumatatu tarehe 11 Januari 2021 baadhi ya miili ya abiria waliopata ajali hivi karibuni imeanza kuonekana ikielea juu ya bahari. Operesheni hii inawajumuisha watu 2, 600 wanaotumia meli 53 pamoja na msaada wa ndege ili kutafuta miili ya watu waliopata ajali na kutumbukia baharini. Ndege hii aina ya SJ 182 ilikuwa na wafanyakazi 12 na abiria 50, wakiwamo na watoto 10. Serikali ya Indonesia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameanza kufanya uchunguzi wa kina, ili kubaini chanzo cha ajali hii ambayo imesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Wasiwasi mkubwa ni kuhusu usalama wa aina hii ya ndege ambayo imekuwa ikifanya safari zake kwa muda wa miaka 27 sasa. Uchunguzi utajikita zaidi katika ukarabati wa ndege hii, taarifa za injini, orodha ya manahodha wa ndege, mafunzo pamoja na taarifa za mwenendo wa ndege nchini Indonesia.

Ajali Indonesia
11 January 2021, 15:04