Tafuta

2019.02.06 Kituo cha Astalli ( mateo ricci) 2019.02.06 Kituo cha Astalli ( mateo ricci) 

Watu 6 wafariki katika fukwe za Libia:mikondo ya kibinadamu inahitajika!

Padre Camillo Ripamonti,Mwenyekiti wa Kituo cha Astalli ametiwa moyo na barua ya Papa Francisko na kubainisha juu ya hali halisi ya sasa kama vile maono ya kinabii ya Padre Arrupe ambaye miaka 40 iliyopita alianzisha Huduma ya Wajesuit kwa ajili ya Wakimbizi. Ulaya iko mbali na mabadiliko ya kimantiki.Wakati huo manusura wa Mediteranea wanaendelea lakini hata kifo cha mtoto wa miezi sita.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Siku moja baada ya siku nyingine ya kushangaza katika bahari ya  Mediterrania, Baba Mtakatifu Francisko ametuma barua ya kutia moyo Padre Thomas H. Smolich SI, mkurugenzi wa kimataifa wa Huduma ya Kijesuit kwa ajili ya Wakimbizi(JRS), kwenye tukio la kumbukumbu ya miaka 40 tangu kuanzisha kwa hali halisi ya huduma yao kwa wakimbizi.

Papa: familia ya wanadamu katika mtumbwi mmoja

Katika barua yake Papa anasema “wakati mnapyaisha na kuongeza juhudi za kweli katika kuhudumia mahitaji ya wenye shida mbambali na magumu ya wakimbizi na watu waokimbia makazi yao, ninaomba kwamba ninyi nyote mpate faraja na hekima kutoka katika maono na mfano wa mwanzilishi wenu,”. Amesema hayo wakati akirudia kueleza historia nzima ya kujitoa kwamba ni kuanzia na “watu wa mtumbwi" ambao walitoroka kutoka Vietnam mapema miaka ya themanini hadi changamoto za uhamiaji za siku zetu ambazo zinaonyesha jinsi familia nzima ya wanadamu iko kwenye mtumbwi mmoja”.

Mienendo ya mikasa

Wakati huo huo, katika masaa 24 yaliyopita, habari hiyo inaripoti mikasa mipya kutoka pwani ya Libia, ambapo inasemekana kuwa boti iliyo na wahamiaji wapatao 100 ilivunjika, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua sita, pamoja na mtoto wa miezi 6. Boti hiyo imeanguka karibu na  maili 30 kaskazini mwa Sabratha. Waokoaji kutoka katika shirika lisilo la kisekali (Open Arms) walifika katika eneo la ajali ya meli, hiyo wakakuta watu ndani ya maji, bila koti za okoa maisha, wakijaribu kujiokoa kwa kushikamana na chochote kilichoelea juu. Watu Sita kati yao hawakufanikiwa, pamoja na mtoto wa miezi sita kutoka nchini Guinea.

Utata juu ya kuzuiwa kwa NGOs

Walinzi wa Pwani ya Italia, baada ya kuthibitisha ukosefu wa uwezekano wa mataifa mengine katika mkoa huo, walituma mashua ya doria na wafanyakazi wa matibabu, lakini Shirika lisilo la kiserikali linajadili na mamlaka, kwa madai kuwa ndilo ukweli pekee uliobaki kufanya kazi katika Bahari ya Mediterania baada ya kusimama usimamizi wa boti nyingine za mashirika yasiyo ya kiselikali (ongs). Na jioni hiyo hiyo shughuli ya uokoaji ya shirika la Uhispania iliendelea. Meli hiyo tayari imesheheni wahamiaji 198 na  imekamilisha uokoaji wa mashua nyingine ikiwa na watu 65 ndani.

12 November 2020, 18:23