Tafuta

Tarehe 2 Novemba ya kila mwaka ni Siku ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji sheria ya uhalifu dhidi ya wanahabari. Tarehe 2 Novemba ya kila mwaka ni Siku ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji sheria ya uhalifu dhidi ya wanahabari. 

Tarehe 2Nov ni Siku ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji sheria ya uhalifu dhidi ya wanahabari!

Ripoti ya UNESCO iliyotolewa tarehe 2 Novemba huko Paris,Ufaransa ikiwa ni katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji wa sheria ya uhalifu dhidi ya wanahabari,inasema kuwa ngawa idadi ya wanahabari waliouawa ulimwenguni imepungua,lakinbado wengi sana wanalipa bei ya mwisho kwa kuripoti kwao.Bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatari zinazoongezeka zinazowakabili wafanyakazi wa vyombo vya habari.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Takwimu mpya zilizochapishwa na UNESCO kabla ya Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Kutokujali kwa Makosa dhidi ya Wanahabari, ifnyakayo kila tarehe 2 Novemba, zinaonyesha kupungua kwa asilimia 14% kwa mauaji ya waandishi wa habari mnamo 2018-2019 ikilinganishwa na kipindi cha miaka miwili iliyopita. Takwimu hizo mpya zimewekwa katika Ripoti ya Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO kuhusu Usalama wa Wanahabari na Hatari ya Kutokujali, na pia zinaonyesha kuwa kiwango cha kutokujali kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa habari bado ni kubwa mno na karibu kesi tisa kati ya kumi zimesalia bila kuadhibiwa.

Ingawa idadi ya wanahabari waliouawa ulimwenguni imepungua,, taarifa inasisitza kuwa bado wengi sana wanalipa bei ya mwisho kwa kuripoti kwao. Tunabaki kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya hatari zinazoongezeka zinazowakabili wafanyikazi wa vyombo vya habari nje ya mazingira ya mizozo, na kuendelea kuadhibitiwa kwa mashambulio haya,” amesema hayo Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay. “Ili kuhifadhi haki ya kimsingi ya uhuru wa kujieleza na kuhakikisha ufikiaji wa umma wa habari za kuaminika, waandishi wa habari lazima waweze kutekeleza kazi zao katika hali ya uhudru na salama wakati wale wanaofanya uhalifu dhidi yao lazima wafikishwe mahakamani”, amesisistiza. Kulingana na ripoti hiyo, mnamo 2018-2019, UNESCO ilibainisha jumla ya mauaji 156 ya waandishi wa habari ulimwenguni. Hamsini na saba kati yao yalitokea mnamo 2019, jumla ya chini kabisa kwa mwaka katika miaka kumi.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake alioutoa tarehe 2 Novemba  mjini New York Marekani kuhusu siku  ya  kimataifa ya kutokomeza ukwepaji wa sheria ya uhalifu dhidi ya wanahabari, amesema katika siku ya mwaka huu, dunia vikiwemo vyombo vya habari, juu ya changamoto nyingine, vimekabiliwa na changamoto mpya kabisa ambayo ni COVID-19.  Bwana Guterres amesema, janga la COVID-19 limeonesha hatari mpya kwa waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari, hata idadi ya mashambulio juu ya usalama wao wa mwili yameongezeka. Kulikuwa na mashambulio yasiyopungua 21 kwa waandishi wa habari walioshughulikia maandamano katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2020 ambayo ni sawa na idadi ya mashambulio kama hayo katika mwaka mzima wa 2017. Pia kumekuwa na vikwazo vya ziada kwa kazi ya waandishi wa habari, pamoja na vitisho vya mashtaka, kukamatwa, kufungwa, kunyimwa upatikanaji wa uandishi wa habari na kushindwa kuchunguza na kushtaki uhalifu dhidi yao.

Akisisitiza zaidi, Katibu Mkuu amesema  “Wanahabari wanapolengwa, jamii kwa ujumla inalipia gharama. Ikiwa hatutawalinda waandishi wa habari, uwezo wetu wa kukaa na habari na kufanya maamuzi yanayotegemea ushahidi utakuwa umezuiliwa sana. Wakati waandishi wa habari hawawezi kufanya kazi zao kwa usalama, tunapoteza ulinzi muhimu dhidi ya janga la habari potofu na habari mbaya ambazo zimeenea mtandaoni.” Amenukuliwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.   Aidha Bwana Guterres amesema habari zinazoegemea ukweli na uchambuzi hutegemea ulinzi na usalama wa waandishi wa habari wanaofanya ripoti huru, iliyojikita katika kanuni ya msingi: "uandishi wa habari bila woga au upendeleo".  Wakati ulimwengu unapambana na janga la COVID-19, narudia wito wangu wa kuwa na vyombo vya habari huru ambavyo vinaweza kuchukua jukumu muhimu katika amani, haki, maendeleo endelevu na haki za binadamu.

02 November 2020, 16:09