Tafuta

Wahamiaji wanazidi kuzama kwenye bahari ya Mediteranea wakati wa safari zao za kubahatisha Wahamiaji wanazidi kuzama kwenye bahari ya Mediteranea wakati wa safari zao za kubahatisha 

ULIMWENGU:Ni matatizo juu ya matatizo katika Dunia!

Matazo ya silaha,ukimbizi,mlipuko ya magonjwa,umaskini,maandamano,ukosefu wa haki za mwanadamu,njaa,ukame,mafuriko,dhoruba na mengine mengi ndiyo matatizo ambayo yanazidi kumulika nchi mbalimbali ulimwenguni.Wahamiaji 74 wamefariki dunia baada ya meli yao kuzama nje ya pwani ya Libia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa, wahamiaji wapatao 74 wamefariki dunia baada ya meli waliokuwamo ndani yake kuzama hapo  nje ya pwani ya Libia. Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema boti hiyo ilikuwa imebeba zaidi ya watu 120, kati yao wanawake na watoto. Limeongeza kuwa manusura 47 wameweza kuokolewa na miili 31 tayari imeopolewa. IOM imeeleza kuwa tangu mwezi Oktoba hii ni takriban ajali ya tisa kutokea katika bahari ya Mediterania. Na katika siku mbili zilizopita, watu wasiopungua 19, pamoja na watoto wawili, walizama baada ya boti mbili kuzama katikati mwa Mediterania. Maelfu ya wahamiaji wengine hukamatwa na walinzi wa pwani ya Libya, wanaoungwa mkono na Italia na Umoja wa Ulaya. Baada ya kukamatwa wahamiaji hao hurudishwa Libia na kuwekwa katika vizuizi vyevye hali mbaya

Ehiopia:watu karibia 11,000 wanakimbia mapigano yanayoendelea kaskazini mwa Tigrey

 Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema tarehe 12 Novemba 2020  raia wengi wameuawa katika kile ilichokitaja kuwa ni mauaji ya watu wengi, kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia. Mashahidi wamesema mauaji hayo yamefanywa na vikosi vinavyounga mkono chama tawala cha eneo hilo, Tigray People's Liberation Front (TPLF) katika mapambano yake dhidi ya serikali kuu ya shirikisho, Na zaidi ya watu 11,000 wamekimbilia nchi za jirani kama Sudan. Shirika hilo limethibitisha katika ripoti yake kwamba mashambulizi haya pia yanahusika na tukio la  mamia ya watu waliuliwa kwa kuchomwa visu au kukatwa atwa hadi kufa katika mji wa Mai-Kadra jimbo la Tigray usiku wa Novemba 9. Ni tukio la kwanza la vifo vingi kuripotiwa katika mzozo huo ulioanza wiki moja iliyopita kati ya chama cha (TPLF).Umoja wa Mataifa unaomba kuweza kuingiza huduma za kibinadamu katika eno la Tigray ili kuhakikisha usalam wa raia ambao wanakimbia mapigano hayo.

UNICEF/OMS/CDC:kuna ongezeko karibia asilimia 50% la vifo ulimwenguni kutokana na surua tangu 2016

Shirika la Afya Duniani WHO limesema idadi ya watoto waliopata ugonjwa wa surua mwaka jana ilikuwa ya juu zaidi katika miaka 23. Utafiti uliochapishwa jana, umesema idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo ilifika watu 207,500 ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 tangu mwaka 2016. Wataalamu wanasema ongezeko hilo limetokana na kupungua kwa kiwango cha kuwapatia watoto chanjo. Watoto lazima wapate dozi mbili za chanjo ya surua ili kuwaepusha kupata ugonjwa huo wa kuambukiza. Ili kuzuia milipuko ya ugonjwa wa surua, shirika la WHO linakadiria lazima asilimia 95 ya watu wapatiwe chanjo.

Burkina Faso: Mauaji ya wanajeshi katika kichaka

Wanajeshi kumi na wanne wameuawa katika shambulio la kuvizia kaskazini mwa nchi ya Burkina kwenye mpaka na Mali na Niger, moja ya mkoa ulioathiriwa sana na ukatili wa vikundi vya kijihadi. Ni moja ya mashambulio mabaya zaidi kwa jeshi katika miaka mitano na katikati ya kampeni ya uchaguzi wa urais na wabunge mnamo tarehe 22 Novemba 2020.

Angola:Maandamano yasiyo na ruhusa kusababisha ghasia

Polisi wamefyatua risasi na kutumia mabomu ya machozi dhidi ya vijana wakiandamana Jumatano trehe 12 Novemba 2020  dhidi ya umaskini huko Luanda katika mji mkuu wa chi. Maandamano hayo, yaliungwa mkono na Unita, chama kikuu cha upinzani, lakini ambayo yalikuwa yamepigwa marufuku na serikali za mitaa.

13 November 2020, 17:28