Tafuta

20202.11.26 Angola wanawake katika mji mji mkuu Luanda 20202.11.26 Angola wanawake katika mji mji mkuu Luanda 

Siku ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ambayo ni changamoto kubwa duniani

Janga la COVID-19 limedhihirisha zaidi suala la ukatili dhidi ya wanawake kama dharura ya ulimwengu inayohitaji hatua za haraka katika ngazi zote,katika nafasi zote na watu wote na kwamba anguko la kijamii na kiuchumi kutoka kwa janga hili kunawasukuma wanawake na wasichana katika umaskinimna hatari ya unyanyasaji dhidi yao inaongezeka.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake inayoadhimishwa kila Novemba 25, ya kila mwaka ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kwani ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni changamoto ya haki za binadamu ulimwenguni. Bwana Guterres amesema janga la COVID-19 limedhihirisha zaidi suala hili la ukatili dhidi ya wanawake kama dharura ya ulimwengu inayohitaji hatua za haraka katika ngazi zote, katika nafasi zote na watu wote na kwamba anguko la kijamii na kiuchumi kutoka kwa janga hili kunawasukuma wanawake na wasichana katika umaskini, na hatari ya unyanyasaji dhidi yao inaongezeka.  Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, “mwezi Aprili mwaka huu, nilihimiza jamii ya kimataifa ifanye kazi kumaliza janga la kivuli cha unyanyasaji wa kijinsia mara moja na daima. Narudia tena na kuzindua tena ombi hilo leo.”  Aidha Bwana Guterres amesisitiza kuwa, jamii ya ulimwengu inahitaji kusikia sauti na uzoefu wa wanawake na wasichana na kuzingatia mahitaji yao, hasa manusura na wale ambao wanakabiliwa na aina nyingi na mtambuka za ubaguzi.

Katibu Mkuu wa UN amesema “Lazima pia tupatie kipaumbele uongozi wa wanawake katika kutafuta suluhisho na kushirikisha wanaume katika mapambano.”.  Vilevile Bwana Guterres amesema hatua lazima ihusishe ufadhili wa kutabirika na rahisi kwa mashirika ya haki za wanawake, ambao mara nyingi ndio huchukua hatua ya kwanza wakati wa mizozo n ani muhimu kwamba huduma kwa manusura wa ghasia zibaki wazi, na rasilimali na hatua za kutosha kusaidia majibu ya kiafya, kijamii na haki. “Hatua hizi hazipaswi kuzingatia tu kuingilia kati mara tu unyanyasaji wa wanawake unapotokea. Wanapaswa kufanya kazi kuzuia unyanyasaji kutokea kwanza, ikiwa ni pamoja na kushughulikia kanuni za kijamii na ukosefu wa usawa wa nguvu, na polisi na mifumo ya kisheria inahitaji kuongeza uwajibikaji kwa wahalifu na kumaliza kulindwa kwa watenda uovu.” Amesisitiza Guterres.  Bwana Guterres amehitimisha kwa kusema katika siku hii ya kimataifa, "tuongeze juhudi zetu za kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia milele."

Hata hivyo katika kuangazia harakati za kukabili ukatili dhidi ya wanawake, tunakwenda nchini India ambako harakati za mfuko wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa, IFAD, umesaidia wakazi wa eneo la Maharashtra kuondokana na tabia ykutaka wajawazito kutoa mimba za watoto wa kike. Nchini India, wanawake wa jamii ya Maharashra wakigonga kifaa maalum kuashiria tukio maalum la sherehe. Nalo si lingine bali ni uzao wa mtoto, lakini leo tukio hili ni la ajabu zaidi kwa kuwa sherehe ni ya kukaribisha kuzaliwa mtoto wa kike. Rupaki Pandurand Pawar ni mama mzazi. "Naitwa Rupali Pandurand Pawar. Naishi Velgaon, Karjat na nina umri wa miaka 30. Ujauzito wangu wa pili nimejingua mtoto wa kike. Nilifurahi sana, halikadhalika familia yangu. Kijijini kwetu, serikali ya kijini inafurahia uzao wa mtoto wa kike.”

Awali sherehe kama hizi zilikuwa ni za uzao wa mtoto wa kiume na si wa kike. Tukio hilo  limeandaliwa na mradi wa Tejaswini unaofadhiliwa na IFAD na serikali ya India. Mradi umejengea uwezo zaidi ya wanawake milioni moja kwa kuwajengea uwezo kifedha na kitamaduni.  Licha ya sheria za kupiga marufuku uchunguzi wa ujauzito ili kuepusha utoaji mimba za watoto wa kike, bado sehemu nyingi nchini India kuwa na mtoto wa kike inaonekana ni jambo la kukatisha tamaa. Sasa mradi unataka kuhamasisha jamii kuona watoto wa kike sawa na wa kiume kama asemavyo Shraddha Joshi, Mkurugenzi kutoka IFAD. “Sherehe kama za watoto wa kike ni muhimu sana kwetu. Zinatusaidia kwa njia nyingi. Mosi kuzuia uchaguzi wa jinsia, unaongeza kiwango cha uwiano wa jinsia. Mtazamo wa jamii nzima unabadilika. Zamani mtoto wa kike alikuwa mzigo sasa anafurahiwa.” IFAD inasema juhudi za pamoja kupitia mradi kama huu umeleta mafanikio makubwa na kuongeza idadi ya watoto wa kike wanaozaliwa.  Kadri Rupali anavyopokea zawadi kutoka rafiki zake, anapata matumaini kuwa hata binti yake atakuwa anapata heshima sawa kama mtoto wake wa kiume.

25 November 2020, 17:14