Tafuta

Nembo ya chanjo ya Biontech na Pfizer ambayo wataalam wanasema kutibu covid kwa asilimia 90 Nembo ya chanjo ya Biontech na Pfizer ambayo wataalam wanasema kutibu covid kwa asilimia 90 

Covid:Pfizer na BioNTech ni chanjo ya covid kwa 90%

Kampuni ya Marekani na ile ya Ujerumani imethibitisha matumaini ya chanjo ambayo imeonesha asilimia 90 kutibu Covid.Shirika la Afya duniani WHO limepokea taarifa kwa tumaini ikiwa pamoja na Kamati Umoja wa Ulaya na rais mteule wa Marekani Biden,lakini wote wanashauri kuwa lazima kuendelea kujilinda kwa kutumia barakoa na kutunza umbali.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuna matumaini katika mapambano dhidi ya virusi vya corona baada ya kampuni ya madawa yenye makao yake mjini Mainz, Ujerumani ya Biontech, kusema kuwa chanjo yake inatoa zaidi ya asilimia 90 ya kinga dhidi ya COVID-19.  Pia imesema kuwa Biontech na mshirika wake wa Marekani kampuni ya madawa ya Pfizer zinapanga kutuma ombi la kupewa idhini kutoka kwa Idara ya Chakula na Madawa nchini Marekani (FDA) kuanzia wiki ijayo. Kampuni za Pfizer na BioNtech, ndio watangenezaji wa kwanza wa dawa kutoa data zinazoonyesha mafanikio kutokana na majaribio ya kiwango kikubwa ya chanjo ya virusi vya corona. Kampuni hizo zinasema kufikia sasa hakuna mashaka yoyote kuhusiana na usalama wa chanjo hiyo. Huu ni ushindi mkubwa dhidi ya janga la virusi va corona ambalo limesababisha vifo zaidi ya milioni moja kote duniani, kuuathiri uchumi wa dunia na kuyabadilisha kabisa maisha ya kawaida.

WHO inasema ni habari inayotia moyo shukrani kwa wanasayansi na makampuni: Ni habari ya kutia moyo, anatoa maoni mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Bwana Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye ameshukuru kupitia ujumbe mfupi wa Twitter “wanasayansi na washirika wote ulimwenguni ambao wanaunda zana mpya bora na salama kushinda Covid-1.9 Ulimwengu unajaribu ubunifu na ushirikiano wa kisayansi ambao haujawahi kutokea ili kumaliza janga hilo amehitimisha mkurugenzi wa WHO.

Hata hivyo wakati hatua za kutafuta chanjo , Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa viwango vya  njaa na ukimbizi ambavyo tayari vilikuwa vimevunja rekodi kabla ya mlipuko wa wa ugonjwa wa Corona au COVID-19,  vitazidi kuongezeka wakati huu ambapo wahamiaji na wategemezi wa fedha kutoka nje wanataabika kutafuta kazi ili kusaidia familia zao. Ripoti hiyo ya kwanza ya aina yake imetolewa mjini  Roma Italia tarehe na Geneva Uswisi, 10 Novemba  na mashirika ya Umoja wa Mataifa, la uhamiaji, (IOM) na lile la mpango wa chakula duniani, WFP.

Katika taarifa yao, kwa mfano inaonesha jinsi janga la Corona limeongeza ukosefu wa chakula na kuwaweka hatarini zaidi wahamiaji, walio kwenye mizozo na majanga pamoja na familia zinazotegemea upokeaji wa fedha kutoka kwa jamaa.  Mashirika hayo yameonya kuwa madhara ya kiuchumi na kijamii kutokana na janga la Corona yanaweza kuwa makubwa na hivyo kutoa wito kwa dunia kuchukua hatua haraka ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu yanayoongezeka na kushughulikia athari za kiuchumi na kijamii bila kusahau wale walio hataraini zaidi.

10 November 2020, 15:45