Tafuta

IVORY COAST IVORY COAST 

Pwani ya Pembe:Wanawake ni wahudumu wa amani

Tumekuja kuwa karibu na wanawake wa Pwani ya Pembe ili kuwaonyesha msaada wetu,mshikamano wetuna kutia moyo kwetu kwa kuwaambia kuwa sasa ni wakati wa kusimama kidete;nchi,taifa linawahitaji wao.Wanawake wanawakilisha upendo,ni wabeba maisha,wako kila mahali katika jamii na ni jukumu lao leo hii kusimama kidete na kusema hapana kuwa na vurugu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Bi Joséphine Charlotte Mayuma Kala, Mwakilishi maalum wa rais  wa Tume ya Umoja wa Afrika akiwa nchini Pwani ya Pembe katika hotuba yake kwenye mkutano ulioongozwa na mada “Wanawake katika majadiliano ya upatanishi” amesema kwaba "umetaka mkusanyiko huu mkubwa ili kuonesha kuwa wanawake ni nguvu na ambayo inaweza kuwa wahudumu wa amani. Na wote wanaweza kuwa wajumbe wa amani katika mazingira yao”.

Mwakilishi maalum wa urais wa Umoja wa Afrika amesema hayo katika nchi ambayo inajiandaa na uchaguzi wa Ris wa Nchi ya Pwani ya Pembe Jumamosi tarehe 31 Oktoba 2020 mahali ambapo kwa siku hizi nchi nzima imeongezea matendo ya kuhamasisha amani na kwa maana hiy  wanawake hawakutaka kubaki pembeni katika katika kutafuta mawazo hayo. Kwa mujibu wao na katika muktadha huo, waliunga mkono Umoja wa Afrika na UNESCO katika siku ya utambuzi wa amani iliyofanyika tarehe 27 Oktoba 2020.

Washiriki walisukumwa na ujumbe mbalimbali kushiriki kikamilifu katika mchakato wa amani huko  Pwani ya Pembe ni pamoja na kutoka kvyama vya wapatanishi wanawake wa Umoja wa Afrika (Femwise) ambao walishirikisha pia uzoefu wa nchi zao. Akiendelea na hotuba yake mwakilishi huyo amesema “Tumekuja kuwa karibu na wanawake wa Pembe ya Afrika ili kuwaonyesha msaada wetu, mshikamano wetu na kutia moyo kwetu kwa kuwaambia kuwa sasa ni wakati wa kusimama kidete; nchi, taifa linawahitaji wao. Wanawake wanawakilisha upendo, ni wabeba maisha, wako kila mahali katika jamii na ni jukumu lao leo hii kusimama kidete na kusema hapana kuwa na vurugu”. Bi Marie Louise Baricako  ni wa kutoka  Burundi, anbaye pia ni mjumbe wa ‘Femwise Africa’.

Mkutano huo ulikuwa ni mmoja ya wakati mzuri wa nguvu na wa muungano kati ya wanawake wa asili zote kuanzia kisiasa, kikabila na kidini wa Pwani ya Pembe, ambao walifika idadi kubwa (zaidi ya wanawake 500). Wakati mwingine muhimu ambao uliashiria mkutano huo ni kuanzisha msafara wa amani ambao umekatisha kwa siku tatu jiji la Abidjan.

30 October 2020, 13:34