Tafuta

Uchaguzi Mkuu Tanzaia 2020 Uchaguzi Mkuu Tanzaia 2020 

28 Oktoba ni Uchaguzi Mkuu Tanzania.Kumekucha!

Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 Watanzania wanapiga kura kumchagua rais mpya,wabunge pamoja na madiwani.Tangu asubuhi vituo vimefurika kila mmoja kuonesha wajibu wake kama raia mwema na anayependa nchi yake kwa kumchagua kiongozi anayempenda hasa mwenye sifa zinazostahili kwa dhati kusimamia uongozi katika jamii kwa ajili ya ustawi wa wote.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Jumatano 28 Oktoba 2020 Watanzania wanapiga kura kumchagua rais mpya, wabunge pamoja na madiwani. Vituo vya upigaji kura vimefunguliwa tangu asubuhi mapema na milolongo mirefu ya wapiga kura imeshuhudiwa katika vituo mbalimbali . Rais J. P Magufuli wa chama cha Mapinduzi CCM anayewania muhula wa pili, anakabiliana na mshindani wake wa karibu Tundu Lissu wa Chadema, lakini pia hata washindani wengine katika nchi.  Hii ni kuonesha demokrasia ya vyama vingi ambavyo vina jaribu kutoa sera zao katika jamii.

Kanisa Katoliki la Tanzania  na viongozi wake na zaidi kupitia Rais wake skofu Mkuu Gervas Nyaisonga, wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, mapema katika maandalizi ya uchaguzi huo alitoa mwaliki wa amani kwa waamini wote wa Tanzania, na hasa kwa kutumia fursa hiyo kama sehemu muhimu ya kutoa mchango na kwamba ni kipindi muhimu kw sababu uchaguzi unatoa mwelekeo wa kufuata. Kwa maana hiyo wapiga kula lazima kudumisha amani kwani Tanzania imekuwa ya kijivunia amani. Amani ni tunu msingi na lazima kuilinda ili isivurugwe.

Jumla ya wagombea 15 wanawania wadhifa huo wa urais kwenye uchaguzi wa leo. Hata hivyo kiongozi ambaye bado yuko madarakani Bwana Magufuli amewatolea wito Watanzania kudumisha amani kwenye uchaguzi huo. Ni uchaguzi mkuu wa sita tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini humo mwaka 1992. Hapo jana wakaazi wa visiwani Zanzibar walianza kupiga kura lakini awamu ya jana ilikuwa inahusisha makundi maalum. Upigaji kura unatarajiwa kumalizika saa kumi na mbili jioni.

Mungu ibariki Tanzania, Afrika na Ulimwengu!

28 October 2020, 15:01