Tafuta

Vatican News
Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini umetiwa sahini Mkataba wa amani kati ya na wawakilishi wa serikali ya Sudan na wale wa makundi makuu yenye silaha nchini humo. Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini umetiwa sahini Mkataba wa amani kati ya na wawakilishi wa serikali ya Sudan na wale wa makundi makuu yenye silaha nchini humo. 

Sudan:Mkataba kati ya serikali na waasi.Ni hatua ya mbele kuelekea katika amani

Muungano wa makundi yanayotetea mapinduzi nchini Sudan,ambao unajumuisha makundi manne yenye silaha ni miongoni mwa makundi ambayo yako yamkubali kusaini mkataba wa kihistoria nchini Sudan.Askofu wa Khartoum anasema ni hatua muhimu ya kuelekea katika amani.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Mkataba wa amani umetiwa sahihi mwishoni mwa mwezi Agosti yaani Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini ambapo mazungumzo yaliendelea kufanyika katika miezi ya hivi karibuni na wawakilishi wa serikali ya Sudan na wale wa makundi makuu yenye silaha nchini humo. Mkataba huo unalenga kumaliza vita baada ya miaka kumi na saba vya wenyewe kwa wenyewe. Muungano wa makundi yanayotetea mapinduzi nchini Sudan, ambao unajumuisha makundi manne yenye silaha ni miongoni mwa makundi ambayo yamekubali hatimaye kusaini mkataba huo wa kihistoria nchini Sudan.

Kwa mujibu wa Askofu mkuu Michael Didi Adgum Mangoria, wa Jimbo Kuu Katoliki la Khartoum, Sudan amebainisha kuwa hiyo ni hatua muhimu katika kuelekea kwenye njia ya amani mbele kwa makundi makuu yenye silaha huko Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile. Na mikataba kwa hakika ina maleno yafuatayo: kuwa mwisho wa vita vilivyodumu miaka kumi na saba na kuweza kurudi makwao mamilioni ya watu waliolundika kwa sababu ya vita; utoaji wa uhuru wa kiutawala kwa majimbo ya Darfur Magharibi, ya Kordofan Kusini na Blue Nile; ujumuishwaji wa vikosi vya kijeshi la waasi wa zamani ndani ya jeshi la Sudan ndani ya kipindi cha miezi 39 na udhibiti wa ardhi zilizotumiwa na jamuiya za makabila. Ni makubaliano yaliyotiwa saini jijini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, katika nchi ambayo ilichangia mazungumzo ya amani. Lakini pamoja na hayo vikundi viwili vya waasi vilikataa hati hiyo na havikujiunga na mkataba huo. Kwa sababu hiyo, Askofu Didi anawasihi viongozi wa kisiasa kujumuisha pande zote zinazohusika ambazo zimebaki kutengwa, ili kuwezesha mkataba uwe kamili.

Kwa mujibu wake Askofu mkuu anasema “ili Mkataba wa amani uwe   kamili ni wakati wale wote walio na silaha wanakubali na hakuna mtu aliyeachwa nyuma”. Lakini, hata hivyo askofu mkuu wa Khartoum ameonyesha furaha yake kwa kusitisha mapigano na kumalizika kwa uhasama, huku akionesha hitaji la amani ya kudumu, kwa sababu anasema mwisho wa mzozo hauwezi kulinganishwa na upatanisho wa kweli na kwa maana hiyo ni wakati umefika kwa pande zote zinazohusika kutoa maoni yao. Wito wa kiongozi huyo pia umeungwa mkono na Mwakilishi Mkuu wa Jumuiya ya Ulaya ya Masuala ya Kigeni Bwana Josep Borrell ambaye, kwa barua rasmi, amefafanua makubaliano hayo kama hatua muhimu kwa mabadiliko ya kidemokrasia na kiuchumi ya Sudan hivyo anawaalika vikundi vyote vilivyohusika ili kujiunga na juhudi za amani kwa ajili ya faida ya jamuiya ya raia wote.

04 September 2020, 13:54