Tafuta

Wanawake wakitengeneza madawati ya shule Wanawake wakitengeneza madawati ya shule 

Siku ya Kimataifa ya Kulipa Sawa:Hakuna mtu anayepaswa kuachwa nyuma!

Katika kuhamasisha ufahamu kwenye ulimwengu wa uchumi juu ya mada ya usawa wa malipo pia kwa kuzingatia kipindi baada ya covid-19,Umoja wa Mataifa umeanzisha kwa mara ya kwanza Siku ya Kimataifa ya Kulipa Sawa,ambayo itafanyika kila tarehe 18 Septembata ya kila mwaka na unasisitiza umuhimu wa kufanikisha usawa wa mshahara kama uthibitisho wa haki ya binadamu,dhidi ya aina zote za ubaguzi,hasa dhidi ya wanawake na wasichana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Inachukuliwa kuwa kawaida kwamba mshahara wa thamani sawa unapaswa kulipwa kwa kazi sawa, lakini sivyo ilivyo. Wanawake, kwa mfano, ulimwenguni kote wanalipwa kiwango cha chini kuliko wanaume kwa malipo karibu asilimia 20. Kwa ngazi ya Ulimwengu, mshahara wa wanawake hufikia asilimia 77 tu ya wanaume na tofauti hiyo hudumu kwa maisha yote hadi kufikia idadi inayoongezeka kila kuchaao ya wanawake wastaafu ambao ni maskini. Ukosefu huu wa usawa kati ya mshahara wa wastani wa wanaume na wanawake unaendelea kuonekana katika nchi zote na katika sekta zote, kazi ya wanawake bado haijathaminiwa na wengi wao wako katika nyadhifa tofauti na zile za wanaume licha ya kuwa na kazi sawa. Kwa njia hii, ujuzi sawa karibu haufanani kamwe na usawa wa sifa.

Kwa kuongezea, wanawake wako chini katika uwakilishi wa majukumu ya kufanya maamuzi na katika sekta kama vile sayansi na teknolojia. Kwa namna ya pekee  katika nchi zenye kipato cha juu, wanawake hufanya kazi hasa katika sekta za afya, elimu, masoko ya jumla na rejareja, wakati katika nchi za kipato cha chini na cha kati wameajiriwa sana katika sekta ya kilimo. Kwa upande wa wanawake weusi, wahamiaji au mama tu, pengo hili ni kubwa zaidi. Uzazi katika sehemu ya kazi unachukuliwa kuwa ulemavu sana hadi kwamba unasukuma wanawake katika uchumi usio rasmi, katika kazi ya mara moja au ya muda tu. Hata kama kuna sheria karibu kila mahali ulimwenguni ambayo hutoa likizo ya uzazi, inakadiriwa kuwa ni asilimia 28 tu ya wanawake wanaofanya kazi na kuweza kufaidika na likizo ya uzazi wa kulipwa.

Pamoja na maendeleo hadi sasa yaliyotimizwa lakini bado kuna pengo ambalo linapaswa kuzibwa la ukosefu wa usawa kijinsia ambao umekua polepole na kwa kiwango hiki inakadiriwa kuwa itachukua labda miaka 257 kuziba pengo kati ya wanaume na wanawake katika ulimwengu wa kazi. Katika kuhamasisha ufahamu katika ulimwengu wa uchumi juu ya mada hii pia kwa kuzingatia kuanza kwa upya kipindi baada ya covid-19, Umoja wa Mataifa  umeanzisha kwa mara ya kwanza Siku ya Kimataifa ya Kulipa Sawa, ambayo inaadhimishwa kila ifikapo  tarehe 18 Septemba ya kila mwaka kwa kusisitiza umuhimu wa kufanikisha usawa wa mshahara kama uthibitisho wa haki ya binadamu, dhidi ya aina zote za ubaguzi, hasa dhidi ya wanawake na wasichana.

Kulingana na kwamba wanawake  wanaendelea kupata kazi zenye mshahara mdogo na wenye ujuzi mdogo kuliko wanaume, na ukosefu wa usalama mkubwa wa kazi, na wanawakilishwa chini katika majukumu ya kufanya maamuzi ni kinyume na kanuni ya msingi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo hakuna mtu anayepaswa kuachwa nyuma. Kwa maana hii ni umuhimu wa kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake na wasichana wote ifikapo mwaka 2030.

Licha ya kuhamasisha ukuaji wa uchumi, Malengo ya Maendeleo Endelevu yanalenga kuhakikisha kuwa wanawake na wanaume, vijana na watu wenye ulemavu, wanafanya kazi kwa heshima na malipo sawa kwa kazi ya thamani sawa.  Kwa  kuzingatia Siku ya Kimataifa, Umoja wa Mataifa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wametoa wito kwa Nchi Wanachama na asasi za kiraia, pamoja na mashirika ya wanawake, pamoja na wafanyabiashara na mashirika ya wafanyakazi na waajiri, kuhamasisha  malipo sawa kwa kazi ya thamani sawa na uhuru wa kiuchumi wa wanawake. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ( UN), ni muhimu wakati huu wa janga na baada ya janga la covid-19 kuhamasisha wahusika wote katika soko la ajira ili kuchukua hatua zinazohitajika kuhakikisha kuwa malipo sawa ni kiini cha juhudi za kufufua uchumi.

18 September 2020, 17:26