Tafuta

Vatican News
Maamuzi ya wahudumu wa kibinadamu  ni magumu wanayochukua ili kwenda maeneo magumu zaidi na kuhatarisha maisha yao. Maamuzi ya wahudumu wa kibinadamu ni magumu wanayochukua ili kwenda maeneo magumu zaidi na kuhatarisha maisha yao.  (ANSA)

UN:Wahudumu wa kibinadamu wako mstari wa mbele kwa watu waathirika!

Siku ya Kibinadamu Ulimwenguni inadhimishwa kila tarehe 19 Agosti kwa kuwakumbuka wahudumu wengi wanaohatarisha maisha yao.Ilikuwa ni tarehe kama hiyo mnamo 2003,ofisi ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Baghdad nchini Iraq ilishambuliwa kwa bomu na kuwauwa watu 22.Tangu 2008 Umoja wa Mataifa ukatangaza siku hii kuwa ya kimataifa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Siku ya huduma za kibinadamu duniani huadhimishwa kila tarehe 19 mwezi Agosti kila mwaka tangu mwaka 2008 kukumbuka shambulizi dhidi ya jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Baghdad nchini Iraq tarehe 19 Agosti mwaka 2003. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 22 akiwemo mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq Sergio Vieira de Mello. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuadhimisha siku hii mwaka 2008 kupigia ili kuangazia ulinzi na usalama wa wafanyakazi wanaotoa huduma za kibinadamu sambamba na utu wao kwenye maeneo mengi yenye mizozo na pia yenye majanga ya asili na yasiyo ya asili kwa ujumla.

Wahudumu wa kibinadamu wako mstari wa mbele

Wahudumu wa kibinadamu anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres, wako mstari wa mbele katika sehemu mbali mbali zilizo na majanga mengi na migogoro. Wanatoa msaada kwa raia walioathiriwa na mikasa ili kukabiliana na janga. Wapo katika nchi zilizokumbwa na vita kama  vile Afghanistan, katika maeneo yanayotishiwa na ukosefu wa chakula kama vile ukanda wa Sahel. Wako karibu na watu wanaohitaji sana katika nchi zilizoharibiwa na mizozo na umaskini. Wapo wanawanaume na wanawake wahudumu wa kibinadamu, ni wengi na wanahatarisha maisha yao ili kuokoa wengine.

Migogoro inaendelea kuwa sababu ya uingiliaji kati wa misaada

Migogoro inaendelea kuwa sababu kuu ya uingiliaji wa msaada. Kwa mujibu wa tawakimu za Umoja wa Mataifa kwa  mwaka wa 2019, karibu watu milioni 132, katika nchi 42 ulimwenguni kote, wanaohitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi. Mojawapo ya nchi yenye shida kubwa ni ile ya Yemen. Katika nchi hiyo tu, angalau kuna watu milioni 24 wanahitaji msaada. Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  (DRC) kuna zaidi ya milioni 13 ambao wana hatari ya kufa kutokana na athari kubwa zinazohusiana na njaa. Sudan Kusini bado inatikiswa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyowaangamiza na nchini Afghanistan hali ya uhamiaji wa ndani inaongezewa na ukosefu wa usalama wa chakula. Huko Venezuela, mzozo wa kisiasa na kuanguka kwa uchumi pia kumesababisha uhamiaji wa watu wapata milioni tatu. Hali za majanga pia zinapatikana nchini Siria, Nigeria, Ethiopia na Somalia.

Wahudumu wa kibinadamu wanapaswa wahakikishiwe kuingia nchi zilizoathirika

Msaada wa kibinadamu umeainishwa kupitia safu kadhaa za kanuni msingi, miongoni mwake ni  ubinadamu, kutokuwa na usawa, kutokujali na uhuru. Kwa mujibu wa sheria ya kiutamaduni ya kimataifa,inathibitisha kuwa wahudumu wa kibinadamuni  lazima wahakikishiwe kuingia katika nchi zilizoathiriwa na mizozo ya kibinadamu, migogoro au majanga ya tabianchi ili kutoa misaada na huduma. Mbali na kutoa majibu ya dharura ya haraka wahudumu wa kibinadamu pia hutoa msaada wa kisaikolojia, kwa lengo la kujenga  na kurudisha miongoni mwa kiungo yale mahusiano ya jamumuiya zilizojeruhiwa sana.

Je maisha ya walio kwenye mizozo yangekuwaje bila kuwa na watoa misaada ya kibinadamu?

Moja ya maswali aliyohoji Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR,  Bwana Filippo Grandi wakati wa fursa ya siku kama hii kunako mwaka 2018 alisema: “Hebu fikiria maisha ya walio kwenye mizozo kuanzia barani Afrika, Asia, Ulaya hadi Amerika yangalikuwa vipi bila watoa misaada ya kibinadamu wanaoweka rehani uhai wao? Kwa kujibu alesema:  “mamuzi  yao watoa huduma ya kibinadamu ni magumu wanayochukua ili kwenda maeneo hayo magumu zaidi. Kila wakati ni wito wa kuafanya uamuzi kati ya uhai na kifo.”

19 August 2020, 11:28