Tafuta

Vatican News
NIGERIA-CHAD-Kikosi  cha ulinzi na usalama nchini Nigeria kaskazini katika operesheni NIGERIA-CHAD-Kikosi cha ulinzi na usalama nchini Nigeria kaskazini katika operesheni  (AFP or licensors)

Nigeria:Kundi la kijihadi lateka nyara raia wa Kaskazini mwa nchi ya Nigeria!

Majihadi katika wilaya za kaskazini mwa Nigeria hatua kwa hatua wamezidi kuchukua udhibiti wa idadi kubwa ya watu na kuwateka nyara katika mkoa wa Ziwa la Chad.Kitisho kingine kiliwekwa vizingiti na jeshi mnamo Jumanne wiki hii,lakini wakati wa kundoka wanajihadi hao kujumiusha na wanamgambo wa kutumia silaha walichoma moto vituo vya umma na hospitali iliyofunguliwa hivi karibuni.

Na Sr. Angela Rwezaula Rwezaula -Vatican

Wanamgambo wenye itikadi kali wamewateka nyara mamia ya watu kwenye mji wa kaskazini mashariki ya Nigeria, ambako raia walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kukimbia makazi yao.  Hawa Wanamgambo wa kundi liitwalo ISWAP walivamia eneo la Kukawa kwenye mkoa wa ziwa Chad na kuwakamata watu baada ya kuishi kwenye kambi za wasio na makazi kwa miaka miwili ba sasa waliuwa wakielekea kwao. Kwa miaka kadhaa sasa Nigeria imekuwa ikilengwa na wapiganaji hawa wa wa ISWAP kwa mashambulizi ya mara kwa mara na utekaji nyara wa raia ikiwa ni moja ya mbinu zinazotumiwa na makundi ya itakadi kali. Mwaka 2018 kundi hilo liliwateka zaidi ya wanafunzi wa kike 100 kutoka kwenye mabweni yao tukio ambalo lilirejesha kumbukumbu ya tukio kama hilo la kutekwa wanafunzi wa kike 300 kwenye mji wa Chibok katika jimbo la Borno.

Utekaji nyara  na mauaji nchini Nigeria unazidi

Itakumbuka pia mwezi Desemba mwaka 2019, wanachama wa kundi la Boko Haram  walishambulia Maiduguri katika mkoa wa Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Wakati watu wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa, raia 11 walilipotiwa  kutekwa nyara wakati wa shambulizi hilo. Kwenye usiku wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, kundi hilo  hilo lilivamia na kupelekea vifo vya watu 6 na kutekwa nyara kwa watu watatu katika kijiji cha Bomo Kwaaagilim. Watu 36,000 wameuawa tangu 2009 kaskazini magharibi mwa Nigeria kufutia na ghasia na kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo limekuwepo nchini Nigeria tangu miaka ya 2000.

20 August 2020, 11:56