Tafuta

Ripoti mpya kuhusu njaa ulimwenguni Ripoti mpya kuhusu njaa ulimwenguni 

Umoja wa Mataifa:Hali ya chakula na lishe duniani ni mbaya!

Umoja wa Mataifa unasema kuwa kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani inaendelea kuongezeka. Kwa mujibu wa ripoti mpya ya hali ya uhakika wa chakula na lishe duniani iliyotolewa Jumatatu tarehe 13 Julai 2020 na Who/Fao/Ifad/Unicef/Pam kuwa ni mbaya na kukatisha tamaa japokuwa kuna matumaini ili kuifikia lengo namba 2 ya maendeleo endelevu ifikapo 2030.

Na Sr. Angela Rweza;-Vatican.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya hali ya uhakika wa chakula na lishe duniani iliyotolewa Jumatatu tarehe 13 Julai 2020 na Umoja wa Mataifa inasema kuwa kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani inaendelea kuongezeka. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya pamoja ya mwaka 2020 iliyotolewa mjini Roma, Italia na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya chakula na kilimo FAO na la afya duniani WHO, inasema ingawa hali ni mbaya na ya kukatisha tamaa lakini bado kuna matumaini ya kufikia lengo namba mbili la maendeleo endelevu au SDGs la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030 endapo hatua madhubuti zitachukuliwa sasa, la sivyo lengo halitafanikiwa mwaka 2030 na mamilioni zaidi ya watu watatumbukia kwenye njaa na umasikini.

Watu karibu milioni 700 wamekabiliana na ukosefu wa chakula

Mkurugenzi mkuu msaidizi na mchumi mkuu wa FAO Maximo Toredo akifafanua hali halisi ya uhakika wa chakula duniani amesema “Mwaka 2019 kumekuwa na watu karibu milioni 700 waliokabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula sawa na mtu 1 kati ya 10 na hii inamaanisha kwamba hatupigi hatua katika kupunguza lishe duni dumiani. Tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyumma tonaongezeko dogo badala ya idadi kushuka.” Hilo limeungwa mkono na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye ameonya kwamba mwaka huu hali itakuwa mbaya zaidi kutokana na janga la corona "Janga la COVID-19 linafanya hali kuwa mbaya zaidi, watu wengi watatumbukia katika njaa mwaka huu, hatuwezi kuruhusu hili kutokea. Ripoti iko wazi endapo mwenendo wa sasa utaendelea hatutaweza kutimiza lengo la maendeleo namba 2 la kutokomeza njaa ifikapo 2030. Mabadiliko yanapaswa kuanza sasa.”

Lengo namba 2 kufikia malengo ya maendeleo 2030 liko mbali

Tathimini ya awali ya ripoti hiyo inasema  janga la COVID-19 linaongeza kati ya watu milioni 83 na milioni 132 kwenye jumla ya watu wenye lishe duniani duniani kwa mwaka 2020. Bwana Toredo anasema huu ni mtihani kubwa: “Hii inamaanisha kwamba hatua zozote zilizopigwa kwa mfano katika kupunguza umasikini kwa miaka 10 iliyopita zimepunguzwa na suala la lishe dunia ambalo limekuwa likiongezeka katika miaka iliyopita hali itakuwa mbaya zaidi kwa ongezeko kubwa la watu wenye njaa na maana yake ni kwamba itakuwa  vigumu zaidi kufikia lengo namba 2.” Ripoti imependekeza kwamba ili kufikia lengo namba mbili mwaka 2030 ni lazima gharama ya lishe bora dunini zipungue ili kuwezesha watu wengi zaidi kuweze kumudu lakini pia kuwe na mikakati thabiti ya kupunguza idadi ya watu wasio na uhakika wa chakula kwa kuwajengea uwezo wazalishaji na wasambazaji wa chakula duniani.

14 July 2020, 13:18