Tafuta

Ulimwengu uliojaeruhiwa na janga la virusi vya  corona au covid-19 Ulimwengu uliojaeruhiwa na janga la virusi vya corona au covid-19 

Ulimwengu#coronavirus:Mtazamo wa dunia katika dharura ya kiafya!

Ugonjwa wa virusi vya corona au covid-19 ni changamoto ya kisayansi,lakini pia ni mtihani kwa wote.Lazima tuchukue hatua kwa ajili ya maslahi na mshikamano wa ulimwengu na ubinadamu wetu wa kushirikishana.Ni maneno ya mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya duniani (WHO), Dk.Tedros Adhanom Ghebreyesus tarehe Mosi Julai katika mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari huko Geneva

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Katika harakati ya kutaka kurudia hali halisi ya shughuli za kijamii na zaidi sekta mbali mbali za kiuchumi ambao zimelala kwa kipindi sasa, mashirika ya ndege nchini Marekani yameanza kulegeza vikwazo na viurizi kwenye ndege, wakati rekodi mpya za janga nchini Marekani kesi mpya ni  52,000 katika masaa 24. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeonya kwamba hali bado inazidi kuwa mbaya ulimwenguni. Katika wiki moja, kumekuwa na idadi zaidi ya kesi mpya za maambukizi 160,000 kila siku. Huko New York, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limechukua  hatua za  makubaliano ya azimio la kusimamisha machafuko ulimwenguni kote na kuhimiza mapambano dhidi ya virusi.

Mojawapo ya somo  kuhusu janga ni kwamba, bila kujali hali ambayo nchi najikuta nayo  inaweza kubadilishwa. Hajachelewa sana. Ni maneno ya mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya duniani (WHO), Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus tarehe Mosi Julai katika mkutano wake wa kawaida kwa waandishi wa habari huko Geneva ambapo  mkuu huyo ameonyesha nchini Italia na Uhispania kama mifano ya uwezo wa kubadilisha  hali.

Kunako mwezi  Machi amekumbusha mkuu huyo kuwa Italia na Uhispania ndizo zilikuwa kituo kikuu cha janga la Covid-19. Mwisho wa janga hilo, Uhispania ilirekodi kesi karibu 10,000 kwa siku na Italia zaidi ya kesi 6,500. Lakini nchi zote mbili ziliweza kwenda mbele kwa udhibiti na mchanganyiko wa uongozi, unyenyekevu, ushiriki kikamilifu wote katika jamii na utekelezaji wa njia ya ulimwengu. Katika nchi zote mbli walikabiliwa na hali ya kutisha, lakini wakaigeuza, amebainisha  Dk Tedros.

Mkutano wa pili wa utafiti na uvumbuzi umehitimisha tarehe Mosi Julai ulikuwa umeandaliwa na  Shirika hilo, baada ya ule wa mwezi  Februari, ambao unakusanya pamoja wanasayansi zaidi ya 1000 kutoka ulimwenguni kote ili kutazama namna ya maendeleo yaliyofikia hadi sasa, kujadili uwezekano mpya wa utafiti na kujaribu kujaza mapungufu ya maarifa katika virusi kwa kufafanua vipaumbele vya utafiti kwa nusu ya pili yam waka 2020 na zaidi. Ugonjwa huu ni changamoto ya kisayansi, lakini pia ni mtihani kwa wote. Lazima tuchukue hatua kwa ajili ya maslahi ya mshikamano wa ulimwengu na ubinadamu wetu wa kushirikishana, amehitimisha.

Karibia  watu 100 wamekufa nchini Myanmar katika mgodi wa madini: Miili ya karibu wachimba migodi 100 wa madini ya jade wameotolewa kutoka kwenye tope baada ya maporomoko ya ardhi kutokea kaskazini ya Myanmar tarehe 2 Julai 2020, katika mojawapo ya ajali mbaya kabisa kuwahi kuikumba sekta hiyo yenye hatari kubwa. Mkasa huo umetokea baada ya mvua kubwa kunyesha karibu na mpaka wa China katika jimbo la Kachin. Idara ya Zima Moto ya Myanmar imesema wachimba migodi hao walifunikwa na wimbi la tope na mpaka sasa miili ya watu 113 imepatikana. Polisi ya eneo hilo imesema waathiriwa hawakujali onyo la kutofanya kazi katika migodi hiyo wakati wa mvua. Shughuli ya utafutaji na kuokoa imesitishwa kwa muda kwa sababu ya mvua kubwa. Watu hufariki kila mwaka wakati wakifanya kazi katika sekta hiyo yenye faida kubwa, lakini isiyodhibitiwa ipasavyo ya madini ya jade.

02 July 2020, 10:10