Tafuta

Vatican News
2020.07.06 Mtunzi maarufu Ennio Morricone 2020.07.06 Mtunzi maarufu Ennio Morricone  (Vatican Media)

Mtunzi mkubwa Ennio Morricon amefariki akiwa na miaka 91

Alikuwa amelazwa katika Kliniki moja Roma.Alikuwa amepokea Medali ya Dhahabu ya Kipapa kunako mwaka 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mwanamuziki na mtunzi Ennio Morricone na mmoja wa waandishi maarufu wa sauti nzuri zenye historia ya sinema amefariki mjini Roma akiwa na umri wa miaka 91. Alikuwa amelazwa katika kliniki ya Waroma kwa sababu ya kuanguka. Mauti yamemfikia alfajiri ya tarehe 6 Julai 2020 akiwa amezungukwa kwa faraja ya amani, kwa mujibu wa msemaji wa familia rafiki yake na wakili, Giorgio Assumma. Katika taarifa yake amesema “Mwalimu huyo alikuwa na fahamu lukuki hadi mwisho na heshima kubwa. Ameweza kumuaga mkewe mpendwa Maria ambaye alimsindikiza katika jitihada zake zote wakati wa maisha yake ya kibinadamu na taaluma yake  na alikuwa karibu naye hadi pumzi yake kuzimika.  Mazishi yatafanyika kwa faragaha kulingana na matashi na unyenyekevu ambao umekuwa ukichochea vitendo vya uwepo wake”. Amesisitiza msemaji huyo.

Muziki na imani

Wakati wa maisha yake ya kutengeneza filam ya Sergio Leone, ameweza kutunga zaidi  ya sauti 500 ikiwa ni pamoja na zile ziitwazo “Nuovo Cinema Paradiso” yaani ‘Cinema mpya ya mbingu’ na “Mission”.  Aliweza kutunga hata muziki mkubwa wa Pop ya Italia kwa miaka ya 60 kama vile “Se telefonando” yaaani ‘ikiwa ningepiga simu’ na “Sapore di sale” yaani ‘ladha ya chumvi’. Ametunukiwa Oscar ya kazi yake kunako  2007 na  The Hateful Eight” ya  Quentin Tarantino kunako mwaka 2016 na kunako mwaka 2019 alipokea  medali ya Dhahabu ya Kipapa kutoka kwa Papa Francisko kutokana na jitihada zake za kisanii na ambazo zimejikita katika mambo yenye asili ya kidini. Miezi michache baadaye, alikuwa ametoa kwaheri ya kuonana kwa maana ya kustaafu shughuli hizo kwa  kushangaza umati na alikuwa amekubali lakini kuongoza tamasha katika Ukumbi wa Papa  Paul VI, mjini Vatican kunako 2020. “Nisingeweza kusema hapana “ kwa mujibu wa maneno yake.

06 July 2020, 12:29