Tafuta

Zindzi Mandela amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59 Zindzi Mandela amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59 

Balozi Zindziswa Mandela, Binti yake Mzee Mandela, Amefariki dunia!

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika ya Kusini, Jumatatu tarehe 13 Julai 2020 ametangaza kwamba, Balozi Zindziswa Mandela, Binti yake Mzee Nelson Mandela na Winnie Madikizela-Mandela, amefariki dunia huko Johannesburg, akiwa ni umri wa miaka 59. Rais Cyril Ramaphosa hakutaja sababu ziliyopelekea kifo cha Balozi Zindziswa Mandela, aliyekuwa anafanya kazi zake nchini Denmark. RIP.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Johannesburg, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika ya Kusini, Jumatatu tarehe 13 Julai 2020 ametangaza kwamba, Balozi Zindziswa Mandela, Binti yake Mzee Nelson Mandela na Winnie Madikizela-Mandela, amefariki dunia huko Johannesburg, akiwa ni umri wa miaka 59. Rais Cyril Ramaphosa hakutaja sababu ziliyopelekea kifo cha Balozi Zindziswa Mandela, aliyekuwa anafanya kazi zake nchini Denmark hadi mauti ilipomfika. Katika kipindi hiki alikuwa nchini Afrika ya Kusini, akisubiri kupangiwa kituo kipya cha kazi huko Liberia, lakini, mauti ikamfika kabla hata ya Serikali haijatekeleza mpango huu.

Balozi Zindziswa Mandela, alizaliwa tarehe 23 Desemba 1960, kwenye kitongoji cha Soweto, Johannesburg. Akiwa na umri wa miezi 18 tu, Baba yake, yaani Mzee Nelson Mandela akahukumiwa kifungo cha maisha na kupelekwa kwenye Kisiwa cha Robben. Balozi Zindziswa Mandela, kama alivyokuwa Baba na Mama yake, hata yeye pia alikuwa ni mwanaharakati, aliyejipambanua tangu awali, akiwa na umri wa miaka 12 alipomwandikia barua Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo, akitaka Jumuiya ya Kimataifa itoe ulinzi kwa mama yake, ambaye maisha yake yalikuwa yako hatarini. Alibahatika kujiendeleza kwa masomo na hatimaye, kutunukiwa Shahada ya Uzamili mambo ya Sheria kutoka katika Chuo Kikuu Cape Town, Afrika ya Kusini. Kwenye Miaka 1985 alisimama kidete kutetea utu, heshima na haki msingi za binadamu dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi. Alikuwa ni malenga mzuri sana wa mashairi yaliyokuwa yanabubujika kutoka katika historia ya maisha ya familia yake.

Balozi Mandela
15 July 2020, 09:56