Tafuta

Vatican News
2018.08.18 Nembo ya Umoja wa Mataifa 2018.08.18 Nembo ya Umoja wa Mataifa  

Miaka 75 ya UN:Tujenge kwa upya jamii na uchumi endelevu!

Lazima tuijenge tena jamii endelevu na yenye uchumi endelevu zaidi na umoja .Ndiyo mwaliko wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bwana Antonio Guterres, aliotoa kwa kukazia kufanya mabadiliko katika fursa ya kumbu kumbu kuundwa ya Miaka 75 tangu kuundwa Umoja wa Mataifa ulitiwasaini huko San Francisco kunako tarehe 26 Juni 1945.

Tarehe 26 Juni imetimia miaka 75 ya mkataba wa kuundwa  Umoja  wa  mataifa, uliotiwa  saini  na  mataifa  50. Wakati wawakilishi wa  mataifa hayo wakitia  saini  mkataba  huo  wa kuundwa  kwa  Umoja  wa  mataifa  tarehe 26 Juni 1945 mjini San Francisco, wawakilishi  hao  walikuwa wamo  katika athari  za  vita  Kuu ya  Pili ya Dunia. Lakini pamoja na hayo yote kulikuwa  na  haja  ya  kupatikana  utaratibu wa  mkataba  utakaokuwa  na  ujumuisho wa  jumla duniani, ambao ni Mkataba  wa  Umoja  wa  mataifa.  “Katika dunia ambayo imeghubikwa na misukosuko na majanga kama virusi vya Corona au COVID-19, mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi , ongezeko la pengo la usawa na watu kutotendewa haki kwa misingi ya rangi, kuhodhi masuala ya anga na hatari ya uzalishaji wa nyuklia, changamoto yetu ya pamoja kama jumuiya ya kimataifa ni kuyakabiliana na  haya” amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres tarehe 25 Juni  wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari kabla ya maadhimisho ya miaka 75 ya kupitishwa kwa katiba ya Umoja wa Mataifa ilitimimia kilele chake tarehe 26 Juni.

Bwana Guteress ameongeza kusema  kuwa “Hakuna hata mmoja wetu anayeweza kutabiri nini kitakachofuata, tuko katikati ya ukungu na kila tuwezapo Umoja wa Mataifa umepenyeza katika ukungu huo na kuchukua hatua. Familia ya Umoja wa Mataifa imejikusanya ili kuokoa maisha, kudhibiti maambukizi ya virusi na kupunguza athari za kiuchumi.” Bwana Guterres amesisitiza kwamba hatuwezi kumudu kurejea katika hali ya zamani na kujenga mfumo ambao utachochea mgogoro “Lazima tujijenge vyema kwa kuwa na jamii na uchumi endelevu, jumuishi na wenye usawa wa kijinsia. Hakuna sababu kwa mfano kwa nchi yeyote kujumuisha makaa ya mawe katika mikakati yake ya kujikwamua na COVID-19”. Huu ni wakati wa kuwekeza katika rasilimali za nishati ambayo haichafui mazingira, yenye kuunda ajira zenye hadhi na kuokoa fedha. Umoja wa Mataifa umedhamiria kuongoza katika nishati endelevu.”

Katibu Mkuu pia alitumia nafasi hiyo kuwasilisha uzinduzi wa ripoti ya muongozo wa hatua za Umoja wa Mataifa za kukabiliana na COVID-19 ambao siyo tu umeorodhesha hatua zilizochukuliwa na Umoja huo katika miezi mitatu iliyopita, lakini pia unatoa mtazamo wa kuelekea kujikwamua vyema. Kuhusu utendaji wa shirika wakati wa miaka hii 75 tangu kupitisha kwa katiba ya Umoja wa Mataifa, Bwana Guterres ameonyesha kwamba “Tumejaribu kusaidia kuunganisha ulimwengu kuwa na ushirika mzuri kwa ajili ya kutatua changamoto za dunia na kwa ajili ya faida ya wote.” Na baadaye  akaorodhesha kazi za kila siku za Umoja wa Mataifa duniani kote na kueleza kwamba amesikiliza majibu ya utafiti wa UN75 ambapo watu zaidi ya 230,000 kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa walishiriki. Utafiti huo ulijikita katika vipaumbele vitatu vya msingi: huduma za afya kwa wote, kuimarisha mshikamano baina ya watu na mataifa na kuufikiria upya uchumi dhidi ya usawa.

Katibu Mkuu aidha amesema “wakati tukisherehekea siku ya katiba ya UN na kuganga yajayo ni lazima tufikirie upya jinsi gani mataifa yanashirikiana.” Amesema miongoni mwa mahitaji muhimu ni haja ya kuwa na ushirikiano wa kimataifa ambao unahusiana  kuyaleta pamoja mashirika ya kikanda ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, taasisi za kimataifa za fedha na mashirika mengine, jumuishi, mchango mkubwa wa asasi za kijamii, makampuni ya biashara, miji, dini na vijana, na utendaji ambao unafanyakazi kama nyenzo ya mwongozo wa kimataifa mahali popote utakapohitajika. Bwana Guterres ameongeza kuwa “Tatizo siyo kwamba ushirikiano wa kimataifa hauko tayari kwa changamoto zinazoikabili dunia. Tatizo ni kwamba ushirikiano wa sasa unapungukiwa na kiwango, matamanio na nguvu. Amekiri kwamba kuna ugumu wa kufikia mabadiliko yenye maana ya mfumo wa utawala wa dunia “bila ushiriki wa mataifa yenye nguvu duniani na ngoja niweke  wazi kwamba uhusiano leo hii haujawahi kuwa mbovu kuliko wakati mwingine wowote.”

Akijibu swali  kuhusu nani ndio wababe hao katika kubomoa ushirikiano; Bwana Guterres amebainisha  kwamba wawili ni mataifa makubwa yenye nyuklia  na uchumi mkubwa Urusi na Marekani wakishika nafasi ya kwanza na taifa hilo la Amerika Kaskazini na China katika nafasi ya pili. Kwa maana hiy  akaongeza kusema “Kaka kuna uhusiano ambazo sasa hivi ziko vibaya na hazifanyi kazi bila shaka ni hizo na tunaona wazi athari zake katika wakati ambao tunahitaji kuchagiza ulimwengu wote ili kulishinda janga la COVID-19, kuyashinda mabadiliko ya tabianchi, kurejesha utulivu angani na kuhakikisha uzalishaji wa nyuklia hatuna tishio jipya ambalo linaweza kuwepukika.”  Hata hivyo alikuwa na matumaini kwamba kutakuwa na “Mwamko mpya wakati tutatambua udhaifu wetu wa pamoja na mwamko huu utafanyika wakati sababu zinazotugawanyaleo hii, badala yake kuwalazimisha watu kuelewa kwamba migawanyiko ni hatari kwa kila mtu kuanzia kwao wenyewe. Na hatimaye huo ndiyo mlango wa kutoka kwenye ukungu unaotughubika na katikati yetu bado inatuonyesha mlango huo.”

26 June 2020, 16:03