Tafuta

Vatican News
Msaada mkubwa nchini Yemen unahitajika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2014 na sasa janga la corona Msaada mkubwa nchini Yemen unahitajika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2014 na sasa janga la corona 

Yemen:Msaada mkubwa unahitajika kwa watu dhidi ya vita na corona nchini Yemen!

Unicef inatoa wito kuwa wasisahau waathirika zaidi hasa katika nchi zenye vita kama vile Yeme.Migororo ya kisilaha kuendelea kwa mashambulizi ya kigaidi na mauji katika nchi ya Burkina Faso,Libya, Misri na Somalia na majanga ya asili kama dhoruba nchini Guatemala na El Salvador.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Dola bilioni mbili na nusu ni kiasi cha pesa zilizotengwa ili kusaidia nchi ya Yemen, katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2014 na sasa pia nchi imeathiriwa na  virusi vya corona. Umefanyika mkutano wa wafadhili, kati ya  Saudia Arabia na Umoja wa Mataifa kwa njia ya video ikiwa ni kutaka kujaribu kukusanya msaada huu kwa kile kinachoweza kuwa  kama operesheni kubwa ya kibinadamu duniani.

Inakadiriwa kuwa ni milioni 12 za watu wanaohitaji msaada lakini pesa iliyotolewa mara nyingi hailingani na kile kinachotengwa. Kwa mfano, Umoja wa Matiafa uliomba zaidi ya dola bilioni 3 mwaka huu, lakini ni asilimia 15% tu ya takwimu hiyo iliyothibitishwa wiki iliyopita. Shida za ndani ya nchi za wafadhili katika kushughulikia janga la Covid-19 na kuporomoka kwa bei ya mafuta tayari zimekata programu nyingine za kibinadamu na kuna uwezekano wa kufunga programu 30 kati ya 41 za Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa msemaji wa Unicef nchini Italia na Yemen Andrea Iacomini, akizungumza na Vatican News, amebainisha kuwa janga la virusi vya corona kwa miezi mitatu au minne sasa, nusu milioni ya watu wanateseka na utapiamlo wa kutisha. Nchini Yemen ni nchi ambayo watoto 8,600  wameuwawa na kujeruhiwa, na zaidi ya watoto 3,000 wamefundishwa kushika silaha. Na tatizo kubwa lipo wakati wa dharura ya kibinadamu ambapo inaishia kusahuliwa na Jumuiya za kimataifa, na ni vigumu kuzungumza, pia vigumu kufanya msaada uweze kuwafikia watu hao. Aidha amesema kile kilichotokea katika miaka ya kwanza ya vita nchini Siria, ndiyo sasa matokeo ya vita huko Yemen ambayo kwa sasa hayana utofauti na ile ya Siria.

BURKINA FASO: inakaridiwa karibu watu 50 wamekufa katika mashambulizi ya makundi ya kijihadi, Ijumaa na Jumamosi iliyopita. Na kati ya watu 30 walio uwawa walishambuliwa wakiwa katika soko.

LIBIA: Karibu raia watano waliuawa na wengine 12 kujeruhiwa Jumapili 31 Mei 2020 kwa makombola dhidi ya mji mkuu Tripoli, Libya. Jambo hilo lilichangiwa na serikali ya umoja wa kitaifa na vikosi vya Jenerali Haftar ambaye kwa miezi hii amekuwa akijaribu kuitwaa  Tripoli.

MISRI: Jeshi lilitangaza kuwa lilimewaua watuhumiwa 19 wa kijihadi katika operesheni zilizolengwa kama sehemu ya hatua yake dhidi ya wanajeshi wa Isis kaskazini mwa Sinai.

SOMALIA: Karibu raia 10 waliuawa na bomu dhidi ya basi ndogo karibu na mji wa Mogadishu. Shambulio hilo halijatolewa maelezo, lakini inawezekana kuwa operesheni ya wanajeshi wa Shebab, ambao hufanya mashambulizi mara kwa mara ndani na karibu na mji mkuu wa Somalia, na mara nyingi wakiwaua raia.

SALVADOR :Dhoruba ya  kitropiki Amanda ikiwa ni ya kwanza katika  msimu kwenye baharí ya Pasifiki, ilitoa kipigo huko Guatemala na El Salvador, na kuwauwa watu wasiopungua 10 katika nchi ambayo wametangaza hata dharura.

 

01 June 2020, 11:39