Tafuta

2020.05.21 Kuna upungufu mkubwa wa chanjo ya polio ya mdomo nchini Libia ambayo mtoto upewa mara baada ya  kuzaliwa na katika umri wa miezi tisa 2020.05.21 Kuna upungufu mkubwa wa chanjo ya polio ya mdomo nchini Libia ambayo mtoto upewa mara baada ya kuzaliwa na katika umri wa miezi tisa 

UNICEF/WHO:Zaidi ya watoto 250elfu nchini Libia wako hatarini na magonjwa!

Maisha na afya ya zaidi ya watoto 250.000 chini ya mwaka mmoja nchini Libya wako katika hatari ya magonjwa yanayoweza kuzuiwa na chanjo kutokana na uhaba mkubwa wa akiba. Kuna upungufu mkubwa wa chanjo ya polio ya mdomo nchini Libia ambayo mtoto upewa mara baada ya kuzaliwa na katika umri wa miezi tisa.Ni kwa mujibu wa sauti ya nguvu ya pamoja ya shrika la watoto Unicef na lile la Afya duniani,Who.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Shirika ya Umoja wa Mataifa la watoto UNICEF  na la Afya Ulimwenguni WHO wanatoa tahadhari kwa sauti moja kuhusiana na  uhaba mkubwa wa chanjo nchini Libya, ambao unaangazia watoto zaidi ya 250,000 walio katika hatari kubwa. Hali inazidi kuwa mbaya na mzozo unaoendelea wa kutumia silaha, janga la COVID-19, huduma za kiafya zilizokatizwa, kuzimwa mara kwa mara umeme, ukosefu wa maji ya kunywa na kufungwa kwa shule na nafasi zilizo nzuri kwa watoto.

Katika miezi miwili iliyopita, ufikiaji wa huduma za chanjo za kawaida umekatishwa kwa sababu ya matokeo ya kufungwa kutokana na ugonjwa huu wa COVID-19, ambao umesababisha hatari ya kuongezeka kwa milipuko ya ugonjwa wa  surua na polio. Kuna uhaba mkubwa wa chanjo ambayo inalinda dhidi ya magonjwa sita kama vile (diphtheria, tetanus, kikohozi cha koo, aina ya mafua ya Haemophilus b na hepatitis B).

Vile vile kuna upungufu mkubwa wa chanjo ya polio ya mdomo, ambayo mtoto upewa mara baada ya  kuzaliwa na katika umri wa miezi tisa. Watoto ambao wako katika maeneo ambayo ni vigumu kufikia na katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro ndiyo wako katika hatari kubwa kwa sababu wanaweza kuwa wamekosa dozi chache za chanjo. WHO na UNICEF pia wanahofia kwamba wahamiaji wengi, wakimbizi au watoto waliorundikana ndani wanaweza wasipate dozi ya chanjo msingi katika nchi zao au wamekosa dozi muhimu nchini Libya.

Amri za ununuzi wa chanjo muhimu zimechelewa kwa sababu ya muda mrefu wa michakato ya idhini ya serikali. Programu ya kupanuliwa nchini Libya (EPI) ilisitishwa kwa sababu ya kupungua vifaa  mwaka 2019. Pamoja na msururu uliogawanywa wa usambazaji katika ulimwengu na vikwazo vinavyohusiana na janga la COVID-19, nchi hiyo inaweza kukabiliwa na upungufu mkubwa akiba kwa mwaka wa pili mfululizo

Naye Mwakilishi maalum wa UNICEF Abdel-Rahman Ghandour amethibitisha kuwa “Chanjo ni moja wapo ya uingiliaji bora wa afya ya umma na wakati chanjo za kawaida zisipofanyikai, uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya milipuko, magonjwa mengine yanayoweza kuepukika na waathiriwa zaidi miongoni mwao ni watoto.

Shirika la Afya ulimwenguni WHO limehamasisha kwa ufanisi kuendeleza Programu ya  EPI wakati wa janga la COVID-19  na viongozi wa afya. Amethibitisha hayo Bi Elizabeth Hoff, mwakilishi wa WHO nchini Libya. “Hata kama tumeshinda kizuizi hiki, ikiwa hifadhi ya chanjo itamalizika tutalazimika kukutana na zile hali nzito zaidi. Hii itahatarisha maisha ya mamia ya maelfu ya watoto nchini Libya. WHO inaungana na UNICEF kwa kutoa msaada wake kamili kwa serikali ya Libya ili kushughulikia changamoto hii muhimu”.

21 May 2020, 15:36