Tafuta

Vatican News
Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu sayansi na utamaduni UNESCO linaonya juu ya habari za kugushi kuhusu COVID-19.Kuwa na mani  ya vyanzo vya habari rasmi.Usishirikishe habari isiyohakikishwa. Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu sayansi na utamaduni UNESCO linaonya juu ya habari za kugushi kuhusu COVID-19.Kuwa na mani ya vyanzo vya habari rasmi.Usishirikishe habari isiyohakikishwa. 

UNESCO na vituo vya Radio katika harakati za kupambana na uongo kuhusu COVID-19!

Katika harakati ya kupambana na ‘Fake News’ kuhusu covid-19 ujumbe kutoka UNESCO unahimiza kwamba katika kipindi chote cha mlipuko wa COVID-19 uwe na imani ya vyanzo vya habari rasmi na vyombo vya habari vya kuaminika tu.Usishirikishe katu habari isiyo hakikishwa.Wakati habari mbaya inaenea kwa watu wenye ushawishi,kuna hatari kwamba habari sahihi na za kuthibitishwa zinakuwa na athari ya kuwekwa kando na hazipokelewi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu sayansi na utamaduni UNESCO, katika hatua za kuchangia harakati za kuondoa habari mbaya za kugushi au za uongo “Fake News” kuhusu  COVID-19 na kukuza ile  tabia nzuri, limetoa  fursa ya safu kadhaa  za ujumbe wa sauti kwa lugha mbali mbali ambazo zinaweza kutumiwa kwa uhuru na vituo vyote vya redio ulimwenguni kote. UNESCO iko mstari wa mbele na inafanya rasilimali hizi zipatikane ili kusaidia kumaliza madhara yanayosababishwa na ‘info-demic’ yaani habari za kudhuru kwa maana nyingine kupambana na hiyo hatari ya kueneza habari za mbaya za kugushi  na ili kuchangia kwa kiasi kikubwa kutoa masuala ya habari za kisayansi zolizothibitiwa kuhusiana na virusi.

Ujumbe mfupi wa sauti (unaopatikana kwa lugha nyingi kama vile kingereza, Kifaransa, Kihispania, kiitaliano, Kiarabu, kiswahili na nyingine) ambazo zinatoa  habari muhimu juu ya hatua za kuzuia, habari potofu juu ya virusi na zinasisitiza umuhimu wa kutokuwa na ubaguzi na kuwa na mshikamano.

UJUMBE WA UNESCO

Habari mbaya za kughushi zipo kila mahalia: Hata hivyo kabla ya dharura, ya virusi vya Corona, UNESCO illikuwa tayari inahisi wasiwasi huo katika suala la kuzidi kuenea kwa kampeni za habari mbaya na hatari kubwa. “Na zaidi katika kipindi hiki kisicho kuwa uhakika mkubwa, woga na machafuko ardhini ni  kama yenye rotuba ya  kuzidi kukua  kwa milima ya  habari za kugushi”, amesema hayo mkuu wa Unesco Guy Berger, katika mahojiano na  Habari za Umoja wa Mataifa. “Wakati  habari mbaya imeeana na kuongezeka kwa watu wenye ushawishi, kuna hatari kwamba habari sahihi na za kuthibitishwa zinakuwa na athari ya kuwekwa kando na hazipokelewi” amesema Berger.

Kwa nini kueneza “fake news”: Kwa mujibu wa  Guay Berger amesema “ Kuna sababu nyingi za kueneza habari za uongo na miongoni mwake ni malengo ya wanasiasa, kujitangaza na kutafuta umakini kwa faida ya mtu mwenyewe binafsi. Wale ambao hucheza kwenye hisia, hofu, ujinga na ubaguzi, wanalenga kufafanua  kwa hakika katika hali ngumu na inayozidi kuongezeka kila wakati

Je inawezakana kufanya nini ili kuhakikisha kuwa habari za kweli, zenye manufaa na nguvu ya maisha ziweze kuja juu? Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu sayansi na utamaduni (UNESCO)  linazingatia uwazi na usambazaji wa takwimu kwa wakati na serikali. Uaminifu katika nyakati hizi za shida unategemea ufikiaji wa habari kutoka vyanzo rasmi, ambavyo hata hivyo haviwezi kuchukua nafasi ya uhuru wa waandishi wa habari. Kwa namna nyingine UNESCO inahimiza serikali kutoweka vizuizi vya uhuru wa kujieleza, lakini pia huku wakichangamana na vyombo vya habari kupambana  dhidi ya kutengua ukweli wakati huo wakiheshimu uhuru wa waandishi wa habari ambao ni huduma muhimu.

Kwa kuongezea, UNESCO iko mstari wa mbele na jitihada za kuzungusha idadi kubwa ya habari ya kuaminika kupitia mikondo yake ya habari kwa kushirikiana na  Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na kuongeza uhamasishaji juu ya roho muhimu ya umma, kupitia utumiaji wa hashtags kama vile: #ThinkBeforeSharing, #ThinkBeforeCaringing, na # ShareKnowledge. Kwa mujibu wa maelezo ya  UNESCO wanasema “uhuru wa kujieleza na haki ya kupata habari ni silaha bora dhidi ya utenguzi wa habari za uongo. Kumbuka kwa kipindi chote cha mlipuko wa COVID-19 kuwa na mani  ya vyanzo vya habari rasmi na vyombo vya habari vya kuaminika tu. Usishirikishe habari isiyohakikishwa”. Kwa maelezo zaidi wasiliana nao: resourcecenter-covid19@unesco.org(link sends e-mail);https://en.unesco.org/covid19/disinfodemic

09 May 2020, 11:03