Tafuta

Félicien Kabuga amekamatwa nchini Ufaransa aliyetafutwa tangu miaka 26 iliyopita kufuatia na tuhuma za ushiriki wa kufadhili mauaji ya kimbari nchini Rwanda kunako 1994. Félicien Kabuga amekamatwa nchini Ufaransa aliyetafutwa tangu miaka 26 iliyopita kufuatia na tuhuma za ushiriki wa kufadhili mauaji ya kimbari nchini Rwanda kunako 1994.  

Rwanda:Mfadhili wa mauaji ya kimbari Kabuga akamatwa!

Félicien Kabuga amekatwa nchini Ufaransa ambaye alitafutwa kwa miaka sasa 26 kwa kushutumiwa kunako mwaka 1997 na Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Rwanda iliyoko nchini Tanzania.Mfanyabiashara huyo wa Kihutu anatuhumiwa kufadhili wanamgambo waliofanya mauaji kwa watu wapatao 800elfu kati ya Watutsi na Wahutu kwa siku mia moja mwaka 1994.

Félicien Kabuga amekatwa nchini Ufaransa ambaye alitafutwa kwa miaka sasa 26 kwakushutumiwa kunako mwaka 1997 na Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) kwa makosa saba ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari, na uchochezi katika mauaji ya kimbari kunako 1994 nchini Rwanda. Mwendesha mashtaka wa umma wa Umoja wa (UN) ameomba kuhamishiwa Uholanzi anayedaiwa kufadhili mauaji ya kimbari wa Rwanda Félicien Kabuga, aliyekamatwa siku ya Jumamosi tarehe 16 Mei 2020 nchini Ufaransa baada ya miaka karibu 26 ya kutoroka, Kabuga anatarajiwa kuhamishiwa katika Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Rwanda nchini Tanzania, lakini kutokana na mlipuko wa janga, mwendesha mashtaka anaomba uhamishaji wake katika Mahakama ya (AIA). Wizara ya Sheria ya Ufaransa ilitangaza kwa taarifa huku ikielezea kwamba Kabuga, kwa sasa mwenye umri wa miaka 84, ameishi chini ya kitambulisho cha bandia katika ghorofa moha huko Asnieres-sur-Seine, karibu na jiji la Paris. Mfanyabiashara wa Kihutu, anatuhumiwa kufadhili wanamgambo ambao walifanya mauaji watao 800,000 kati ya Watutsi na Wahutu kwa siku mia moja mwaka 1994.

Naye Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi Michelle Bachelet tarehe 19 Mei 2020  mjini Geneva Uswisi alikaribisha kukamatwa kwa  Felicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuongoza mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda yalitotekelezwa mwana 1994. Bi Bachelet amesema, “kukamatwa kwa Félicien Kabuga, miaka 26 baada ya mauaji ya kimbari, kunasisitiza ufikiaji mrefu wa uwajibikaji kwa makosa ya kimataifa. Hakuna ambaye anafanya makosa ya kimataifa anatakiwa kufikiri kuwa kupita kwa wakati wanaweza kukwepa mkono wa haki na kwamba hawatawajibishwa.”

Kabuga alikuwa ameshtumiwa mnamo mwaka 1997 na Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) kwa makosa saba  ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari, ushiriki katika mauaji ya kimbari, na pia uchochezi wa moja kwa moja na wa umma wa kutekeleza mauaji ya kimbari , yote haya yakiwa na uhusiano na uhalifu uliofanywa dhidi ya watutsi nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa shutuma, Kabuga pamoja na wengine, wanatuhumiwa kutumia Kituo cha redio cha Radio Television Libre des Mille Collines (RTLM) kuchochea zaidi chuki kati ya watu wa kabila la wahutu na watutsi nchini Rwanda. Kabuga pia anatuhumiwa yeye pamoja na wengine, kuanzisha uchangishaji fedha za kufadhili kundi la wanamgambo wa Interahamwe ambalo liliongoza mauaji dhidi ya watutsi, katika kipindi ambacho watu wa kabila la wahutu ambao waliyapinga mauaji, nao waliuawa.

“Tunapoendelea hii leo kuona hatari ya habari za uongo, chuki ya rangi na ukabila na uchochezi wa vurugu vikisambazwa kwa ukubwa, kesi ya Kabuga na matokeo ya propaganda yaliyotangazwa na Radio Television Libre des Mille Collines, ni ukumbusho wa lugha kama hiyo inakoweza kutupeleka, nani kwa nini kupambana navyo ni muhimu.” Amesema Kamishna Mkuu wa haki za binadamu za Umoja wa Mataifa. Aidha Bi Bachelet amepongeza ueledi wa mwendesha mashitaka Serge Brammertz na timu yake pamoja na mamlaka za Ufaransa, na juhudi za mamlaka za kutekeleza sheria katika nchi nyingine ambao kwa pamoja walifanikisha kukamatwa kwa Kabuga nchini Ufaransa tarehe 16 Mei 2020.

21 May 2020, 14:20