Tafuta

Vatican News
Vurugu zaidi nchini Malawi zimeongezeka kutokana na mtazamio wa kurudia kupiga kura za uchaguzi wa Rais. Vurugu zaidi nchini Malawi zimeongezeka kutokana na mtazamio wa kurudia kupiga kura za uchaguzi wa Rais.  (AFP or licensors)

MALAWI:Vongozi wa kidini walaani mauaji maana kila maisha ni matakatifu!

Familia moja huko Lilongwe nchini Malawi imepata shambulio na kusababisha vifo vya watu 4, waliochomwa wakiwa hai.Familia hiyo ilikuwa inaishi katika majengo yaliyotumiwa na chama cha Muungano wa harakati za mabadiliko (UTM), na ndiyo chanzo cha shambulio hilo.Kwa mujibu wa Tume ya kidini ya masuala ya umma inalaani kitendo hicho na kwamba kila maisha ni matakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican  

Kwa mujibu wa  tume ya maswala ya umma (PAC), kiungo  ambacho kinajumuisha pamoja na jumuiya zote za dini nchini Malawi kimebainisha kuwa “ kila maisha ni matakatifu”, mara baada ya shambulio la  familia moja  huko Lilongwe ambayo ilisababisha vifo vya watu 4, waliochomwa wakiwa hai. Familia hiyo ilikuwa inaishi katika majengo yaliyotumiwa na chama cha  Muungano wa harakati za mabadiliko (UTM), na ndiyo chanzo cha shambulio hilo. Muungano wa harakati za Mabadiliko (UTM) ni chama cha Makamu Rais Saulios Chilima, ambaye lakini amevunja ushirikiano na Rais Peter Mutharika na kuomba rufaa tarehe 3 Februari 2020.

Kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya maswala ya umma (PAC) iliyosainiwa na Mwenyekiti wake na Katibu wa Mawasiliano, Askofu Gilford Emmanuel Matonga wa Jumuiya ya Kiinjili  wanabainisha “Tukio hilo linapaswa kulaaniwa kwa masharti makali, kwa kuwa linakiuka haki za binadamu na linalenga kutishia na kuleta mgongano wa kidemokrasia wa maoni na kutuliza sauti mbadala”.

Aidha Wajumbe wa tume ya maswala ya umma (PAC) wametahadharisha kwamba vitendo vya ukatili, uwoga na vya uonevu vinaonyesha hisia za kukata tamaa kwa watu, kwani Malawi inajiandaa kwa uchaguzi mpya wa rais. Kwa sababu hiyo, viongozi wa dini wanaomba uchunguzi mzito ufanyike. Vile vile tume hiyo inataka kuongeza sauti yake kwa ombi la upelelezi wa haraka na usio na usawa katika vitendo vya ukatili wa kisiasa bila kujali mtu.

Ikumbuke kuwa Tume ya maasuala ya Umma (PAC) ilianzishwa kunako 1992 wakati wa mabadiliko ya kisiasa ya nchi hiyo kutoka mfumo wa chama kimoja kwenda vyama vingi. Tume ya PAC inaomba kufanyike mazungumzo ya wazi na ya pamoja katika usimamizi wa mabishano ya kisiasa,  utaratibu ambao una msaada kamili wa watu wote nchini Malawi ambao wanapenda amani. “Tunawaomba pia raia wote waheshimu sheria na waepuke aina yoyote ya dhuluma za kisiasa”. Vurugu zaidi zimeongezeka kutokana na mtazamio wa kurudia kupiga kura tarehe 19 Mei mara baada ya Mahakama kuu kubatilisha uchaguzi uliopita.

19 May 2020, 12:07