Tafuta

Vatican News
Mtazamo wa hali halisi katika dunia ya sasa iliyokumbwa na covid-19 Mtazamo wa hali halisi katika dunia ya sasa iliyokumbwa na covid-19 

Dunia#coronavirus:mtazamo katika hali halisi ulimwenguni!

Kwa baadhi ya chi za duniani,Ulaya na kwingineko,Jumatatu 4 Mei 2020,imeona kuanza na hatua ya pili ya shughuli katika harakati za kuondokana na janga la covid-19 ambalo limedhoofisha kila sekta ya maisha ya mwanadamu au kwa maneno mengine rahisi kupigisha magoti mwanadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika umoja wa Nchi za Ulaya tarehe 4 Mei 20, nchini Italia, katika hatua ya pili kwa ufunguzi shughuli mbalimbali katika wakati huu wa janga covid-19 wameanza na viwanda. Nchini Uhispania wamefungua shughuli za biashara, wakati huo huo nchini Ujerumani wamefungua baadhi ya shule. Nchini Hungary na Slovenia, wamefungua Bar na sehemu za Hotel(lakini siyo katika mji wa Budapest).Poland wamefungua nyumba za kulala na vituo vya masoko hata baadhi ya nyumba za makumbusho.

Nchini Israeli wakiwa bado na umakini wa dharura na vizuizi wamefungua baadhi ya shule na wafanyakazi wa kipalestina wanaweza kwa upya kuingia nchini Israeli katika nafasi zao za kazi. Nchini Iran nako wamefungua misikiti katika badhi ya mikoa. Algeria waweza kufunga tena kwa upya maduka kutokana na ukosefu  tahadahari na kuheshimu hatua za usalama. Wakati huo huo nchini Senegal na Japan wameongezea muda tena wa kuendelea na dharura ili kupunguza maambukizi ya vovid-19.  Kwa mujibu wa taarifa za serikali ya Japan  Jumatatu 4 Mei 2020 imeongeza kipindi cha hali ya dharura kwa muda wa takriban mwezi mmoja, kufuatia janga la virusi vya Corona wakati nchi hiyo ikiendelea kuripoti mamia ya visa vya maambukizi mapya kila siku.

Taarifa kutoka jijini Bruxelles wameanza kampeni duniani kwa ajili ya ukusanyaji wa fedha za utafiti wa chanjo dhidi ya virusi vya corona. Muungano wa viongozi wa dunia wamefanya mkutano kwa njia ya video wa kuchangisha mabilioni ya dola kufadhili shughuli za utafiti wa chanjo ya kukabiliana na virusi vya Corona pamoja na utengenezaji wa tiba mpya na upimaji wenye uhakika zaidi.

Na kwa mujibu wa Shirika la watoto duniani, UNICEF imetoa  tahadhari juu ya hatari la ukosefu wa chanjo kwa milioni ya watoto katika nchi za Mashariki na Afrika Kaskazini, dhidi ugonjwa wa Polio na  surua, kutokana na janga la virusi vya corona au Covid-19 ambayo inazuia kufanya kampeni ya chanjo. Nchini Canada, madaktari wamealikwa kuwa na  jitihada katika nyumba za wazee baada ya tuhuma za  kukuta hali mbaya ya wagonjwa kwa sababu ya ukosefu wa wahudumu na mifumo ya usalama katika vituo vya kutunzia wagonjwa. Kwa mujibu wa chuo kikuu cha Johns Hopkins takriban watu milioni 3.5 wameambukizwa virusi hivyo duniani na zaidi ya 247,000 wamefariki kutokana na virusi hivyo vya covid-19.

KOREA ZOTE MBILI: imethibtishwa milipuko ya risasi katika mipaka kati ya Korea Kaskazini na kisini kwa mujibu wa Kiongozi wa Kidiplomasia wa Marekani

VENEZUELA:Serikali imethibitisha juu kugundua jana jaribio la kuvamia kupita njia ya baharini magaidi kutoka nchini Colombia kutaka kufanya mapinduzi dhidi ya Nicolas Maduro. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Caracas, magaidi nane wameuawa, wawili walikamatwa na silaha pia.

MYANMAR:wakimbizi ishiri wa Rohingya waliokuwa wamezuiwa katikati ya bahari kwa baadhi ya wiki sasa wameruhusiwa kutua kwenye kisiwa cha utata na cha mafuriko katika Ghuba ya Bengal.

MISRI:Wanajeshi wa Misiri wamewauwa watu 18 wanaoshukiwa kuwa majihad katika Kisiwa cha Sinai ya Kaskazini Mashariki siku mbili baada ya mashambulizi makali dhidi ya jeshi la kulipiza kisasi la Isis .

UZBEKISTAN: kubomoka kwa bwawa kumesababisha mafuriko kwa maelfu ya nyumba na maeneo ya kilimo nchini Uzbekistan na Kazakhstan, na kusababisha watu 100,000 kukimbia kutafuta mahali pa kujiokoa.

IRAN: Tehran yaonya kuwa kuongeza muda wa kizuizi cha Umoja wa Mataifa juu ya uuzaji wa silaha Iran kama ombi la Washington litaua kabisa makubaliano ya kimataifa juu ya mpango wa nyuklia wa Iran.

04 May 2020, 15:31