Tafuta

Vatican News
Kila tarehe 20 Mei ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya nyuki kwa kuangazia elimu ya asili na ufugaji wa nyuki. Kila tarehe 20 Mei ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya nyuki kwa kuangazia elimu ya asili na ufugaji wa nyuki.  (AFP or licensors)

Coronavirus#Siku ya kimataifa ya nyuki:umuhimu wa elimu ya asili na ufugaji wa nyuki!

Kila tarehe 20 Mei ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya nyuki kwa lengo la kuelimisha juu ya asili na ufugaji wa nyuki.Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa,FAO linatumia siku hii kuangazia athari za janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 katika uzalishaji na biashara ya zao hilo.

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linatumia siku hii kuangazia athari za janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 katika uzalishaji na biashara ya zao la asali. FAO kupitia wadau  wake inasema inatambua kuwa “janga la sasa la COVID-19 limekuwa na athari dhahiri katika sekta ya ufugaji nyuki, huku likiathiri uzalishaji, masoko na matokeo yake ni kuathiriwa kwa maisha ya wafugaji wa nyuki.”

FAO katika  tukio la siku hii tarehe 20 Mei 2020 kwa njia ya video mkutano wao utaangazia  mada ya  ufugaji nyuki katika kusaidia jamii za vijijini na kuboresha upatikanaji wa chakula na lishe hasa wakati huu wa sasa wa janga la Corona au covi 19. Kwa kupitia mada ya “Jishirikishe” FAO inaangazia umuhimu wa elimu ya asili inayohusiana na ufugaji wa nyuki na matumizi ya bidhaa na huduma zitokanazo na nyuki na umuhimu wake katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Kwa mfano, uzalishaji wa nyuki na mifano bora inayotumiwa na wafugaji wa nyuki katika kusaidia kujipatia kipato na kuhakikisha wanakuwa na bidhaa zenye ubora. Vile vile, Siku hii pia inaruhusu kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa wadudu na ndege wachavushaji na tishio wanalokumbana nalo katika mchango wao wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

FAO inasema kuwa nyuki, ambao ni wachavushaji wakuu miongoni mwa wengine kama vile popo na ndege, hivi sasa wako hatarini kutokana na shughuli za binadamu. “Uhai wa wadudu wachavushaji unategemea bayonuia ya dunia. Takribani asilimia 90 ya mimea yenye maua hutegemea kwa kiasi kikubwa uchavushaji sambamba na zaidi ya asilimia 75 ya mazao ya chakula n asilimia 35 ya ardhi ya kilimo,” imesema FAO.

Ni kwa nini Umoja wa Mataifa uliazimia kuweka siku hii? Ni kwa mara ya tatu siku hii ya kimataifa inaadhimishwa hasa Umoja wa mataifa katika kukumbuka nafasi msingi ya nyuki katika kuweka usawa wa asili ya dunia.  Lakini ni kwa nini Umoja wa Mataifa uliazimia kuwa kila tarehe 20 Mei ya kila mwaka ifanyike siku hii? Nyuki ni wadudu msingi kwa maisha ya sayari yetu, kwa kuwa bila nyuki, mimea, maua na mazao ya kilimo ambayo sisi wenyewe tunakula yanaweza kutoweka! Aidha Nyuki  kiukweli ni kati ya wahusika wakuu wa mchakato wa uchavushaji, hiyo ikiwa pia ni usafirishaji wa poleni kutoka ua moja kwenda kwa ua jingine ambalo uruhusu mimea kuzaliana. Kwa hakika Nyuki ni wakulima wa sayari.

Chaguo la kukumbuka kwa siku nzima juu ya  nyuki na kinga yao imekuwa muhimu tangu takwimu zilipoonesha wasiwasi mkubwa kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na mustakabali wa wadudu hawa. Kwa mujibu wa tafiti nyuki hupotea kutoka maeneo mengi ya sayari.Sababu zake? Jibu daima ni  lile lile yaani ni mwanadamu! Hii ni kwamba kupunguzwa kwa makazi yao na uchafuzi wa mazingira umezidi kuathiri sana maisha na uzazi wa wadudu hawa, ambao wamekaribia kutoweka tangu barani Asia pia wanazidi kupungua kwa  haraka hata Bara la Amerika na Ulaya, pamoja na Italia, ambapo nyuki pamoja na uchavushaji wake huzalisha zaidi aina 30 za asali tofauti.

 

20 May 2020, 13:54