Tafuta

Dk Ghebreyesus Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani ameshitushwa na baadhi ya wanasayansi ambao wanadai kutaka kufanya majaribio ya chanjo ya covid-19.Anasema fikira za kikoloni ziishe katika karne ya 21. Dk Ghebreyesus Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani ameshitushwa na baadhi ya wanasayansi ambao wanadai kutaka kufanya majaribio ya chanjo ya covid-19.Anasema fikira za kikoloni ziishe katika karne ya 21. 

WHO#coronavirus:Dk.Ghebreyesus anasema fikra za kikoloni ziishe!

Fikra za kikoloni za kujaribu chanjo ya COVID-19 barani Afrika zikome kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya duniani,kutokana na kauli za baadhi ya wanasayansi kutaka kufanya majaribio ya chanjo ya kwanza ya virusi vya corona barani Afrika.Ni jambo la kushangaza sana kauli kama hizo zitokazo kwa wanasayansi kwa karne ya 21,lakini hatutaruhusu amesema.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Dk. Tedros Ghebreyesus amesema juu ya kushtushwa sana na kauli za wiki iliyopita kutoka kwa baadhi ya wanasayansi wakipendekeza kuwa majaribio ya kwanza ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 yafanyikie Afrika.

Dk, Tedros akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva, Uswisi siku ya Jumatatu trehe 6 Aprili 2020 amesema: “Kusema ukweli nilishtushwa sana . Nikasema wakati huu ambapo tunataka mshikamano, kauli za kibaguzi kama hizo haziwezi kusaidia na ni kinyume na mshikamano”.

“Afrika haiwezi na katu haitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo yoyote. Tutafuata kanuni zote kujaribu chanjo au dawa yoyote duniani kote,  kwa kutumia kanuni hiyo hiyo,  iwe ni Ulaya au Afrika au kwingineko, tutafuata kanuni hiyo na kama kuna umuhimu wa majaribio kwingineko kutibu binadamu, vivyo hivyo kwa usawa. Na  fikra za kikoloni sasa zikome na shirika la Afya duniani (WHO katu haitaachia kitendo hicho kifanyike Afrika au kwingineko.”

Ni jambo la kushangaza sana kauli kama hizo za kufanya majaribio ya chanjo ya COVID-19 Afrika zinatokana kwa wanasayansi katika karne hii ya 21 na  hivyo wamelaani vikali na kusema watahakikisha kwamba suala hili halitendeki. Badala yake amesema taratibu sahihi za majaribio ya chanjo zitafuatwa na binadamu watatendewa kama binadamu kwa kuwa watu wote ni binadamu.

07 April 2020, 15:18