Tafuta

Vatican News
Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona duniani tangu vilipoanza kusambaa kutokea China mapema mwaka huu imefikia milioni na watu 96,000 wamekwisha aga Dunia. Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona duniani tangu vilipoanza kusambaa kutokea China mapema mwaka huu imefikia milioni na watu 96,000 wamekwisha aga Dunia. 

Ulimwenguni#coronavirus:Hali hali halisi ya matukio katika sayari yetu!

Hadi sasa watu 96,000 duniani wamekufa na milioni 1,5 ni maambukizi rasmi yaliyotangazwa.Barani Afrika chini ya jangwa la Sahara amefariki kwa mara ya kwanza mtu wa miaka 25.Uchumi duniani utaanguka sana baada ya 1929.Serikali zinatakiwa kuchukua hatua zaidi za kusaidia makampuni ya kibiashara ili kuepusha athari kwa uchumi na kufanya iwe vigumu kuufufua baada ya janga hili kumalizika.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Katika harakati za mapambano ya Covid-19 madakatari watafiti wanaendelea na mchakato wa kutafuta chanjo au dawa kwa ajili ya mapambano ya virusi vya corona. Nchini India imefunguliwa mchaato wa wa kiafya kwa ajili ya  madawa  yao ya  kienyeji kwa maana nchi hiyo ni mzalishaji mkubwa wa madawa yote kwa ujumla. Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa taifa hili amesema wako wameanza kutoa zawadi zao kwa mataifa yaliyo karibu  ili kuwasaidia kukabiliana na janga la corona. Nchi hizo za madwa kwa zilizo karibu ambazo ni Bhutan, Bangladesh, Afghanistan, Nepal, Myanmar, Seychelles, Mauritius na badhi ya Nchi za Kiafrika. Wamefunga hata usafirishaji wa manadwa ya kuzuia Covid-19 huko Marekani, Uingereza, Brazili, Uhispanaia, Ujerumani, na Italia. Hdi sas anchini India kuna maambukizi ya virusi kwa watu 5734 na vifo vya watu 166. Siku mbili zilizopita wakabidhi tan 10 za madawa nchini Sri Lanka.

Siria:Vizuizi vya Amerika na  Umoja wa Ulaya EU vinazuia mapambano dhidi ya coronavirus. Inakosekana Oksijeni na vitanda katika vyumba vya uangalifu mkubwa (ICU), muhimu katika kesi ya kuenea kwa virusi. Hivi ndivyo Nabil Antaki, daktari wa Kikristo na mtaalam wa gastroenterology, alivyoambia  shirika la habari k AsiaNews, akiwa mstari wa mbele katika harakati za kuwasaidia mamia ya maelfu ya wahathiriwa wa vita ambavyo kwa miaka sasa vimeenea katika nchi hiyo. Yeye pia ni mwanachama mlei wa Shirika la Watawa wa Kiume wa Marist na ni mmoja wa madaktari wachache ambao wameamua kukaa jijini, licha ya vurugu za mzozo huo mkubwa mabao hauna mwisho. Hatua za adhabu, ameoongeza, zinaathiri idadi ya watu wote na zinaweza kuzidisha janga  la virusi vya corona japokuwa havina mtazamo wowote wa kuweza kukomesha vita.

Covid-19: hadi sasa watu 96,00 duniani wamekufa, na milioni 1,5 ni maambukizi rasmi yalitotangazwa. Barani Africa chini ya jangwa la Sahara, amefariki kwa mara ya kwanza mtu mwenye miaka 25. Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi hivyo duniani tangu vilipoanza kusambaa kutokea China mapema mwaka huu imefikia milioni na watu 96,000 wamekwisha aga Dunia. Katika ulimwengu mzima, janga hili litasababisha udhaifu  na mdodoto mkubwa baada ya 1929 kwa kila sekta, kuanzia kijamii na hadi kiuhumi. Katika Umoja wa Mataifa UN, katibu mkuu anaomba kuwa  umoja wa baraza la usalama. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Bwana Antonio Guterres, usimamizi baada ya mgogoro utakuwa  sababu ya kuwa Umoja wa Mataifa ulioungana.

Yemen yatangaza kesi ya kwanza ya virusi vya corona:Mpango wa kusitisha mapigano uliopendekezwa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen umeanza kutekelezwa na kutoa nafasi ya kumalizika kwa mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano. Hata hivyo wakati nchi ikitangaza kesi ya kwanza ya virusi vya corona, vikundi vya waasi wa Houth usiku walikataa pendekezo la kusitisha mapigano yaliyotolewa  na Saudi Arabia wakiifikiria ni njia zao za  ujanja.

Umoja wa Ulaya UE umepata muafaka kati ya mawaziri 27 wa uchumi. Umoja wa Ulaya  EU uko tayari kwa mpango wa euro  bilioni 500 ,  fedha za matumizi ya huduma ya afya na kutaka kukuza uchumi baada ya janga. Katika mpango wao hakuna kiitwacho Eurobonds. Muafaka huo umepatika katika Mataifa hayo yenye nguvu duniani tarehe 9 Aprili  mjini Brussels, ambapo kwa pamoja walikuwa watafute jawabu kuhusu janga la kibinaadamu na kiuchumi linalotokana na mlipuko wa virusi vya corona, wakati idadi ya vifo nchini Marekani na Ulaya vinazidi kuongezeka kwa kiasi kikubwa.  Ikumbukwe hadi sasa nchi zilizoathiriwa vibaya sana ni Italia na Uhispania barani Ulaya.

Katika jiji lililofungwa shughuli zote la New York, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (IFM) limekutana Alhamisi 9 Aprili 2020 kujadili janga hilo kwa mara ya kwanza. Kwa mujibu wao  janga la kimataifa la virusi vya corona linasababisha mgogoro wa kiuchumi tofauti kabisa na wowote uliowahi kutokea katika karne iliyopita na utahitaji juhudi kubwa kabisa ili kurejesha hali ya kawaida. Naye  Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva ameonya kuwa ukuaji wa uchumi duniani utaanguka kabisa katika mwaka huu wa 2020 huku nchi 170 kati ya nchi wanachama 180 wa IMF zikishuhudia kupungua kiwango cha mapato ya wastani. Aidha Bi Georgieva katika hotuba yake kwa njia ya video kutokana na vizuizi vilivyowekwa vya  COVID-19 amebinisha kuwa  nchi tayari zimechukua hatua za kiasi cha jumla cha dola trilioni 8, lakini mkuu amezitaka serikali kuchukua hatua zaidi za kusaidia makampuni ya kibiashara ili kuepusha athari kwa uchumi na kufanya iwe vigumu kuufufua baada ya janga hili kumalizika.

Chad:Jeshi nchini Chad limepoteza wanajeshi 52 wakati wa mapambano tarehe 31 Machi 2020  dhidi ya majeshi ya Boko Haram, yaliyomalizika tarehe 9 Aprili 2020. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya serikali, wapiganaji 1000 wajihadist wameuawa.

10 April 2020, 13:04