Tafuta

Janga la kidunia ambalo ni baya limesababisha tayari milioni moja na elfu 80 kuambukizwa virusi hatari vya corona  duniani kote.Jithada binafsi na pamoja zinahitajika kujilinda. Janga la kidunia ambalo ni baya limesababisha tayari milioni moja na elfu 80 kuambukizwa virusi hatari vya corona duniani kote.Jithada binafsi na pamoja zinahitajika kujilinda. 

Cornavirus duniani#:hali ni ngumu katika mabara yote kwa kasi ya maambukizi !

Watu milioni moja na elfu 80 wameambukizwa virusi hatari vya corona duniani kote huku idadi ya waliokufa ikipanda na kufikia watu 57,474 kutokana na ugonjwa wa COVID-19.Mabara yote duniani zinasikika taarifa za majanga ya virusi,pia na habari nyingine.

Kwa mujibu wa Padre José Barranco mmisionari wa kikomboni nchini Equador anasema hali ni ngumu ya nchi kufuatia na maambukizi ya virusi vya corona. Katika mji wa Guayaquil wenye wakazi milioni 2,3, karibia zaidi ya watu 2,700 wana kesi za maambukizi ya covid-19 katika nchi yote na ambayo imelazimisha kuwa na dharurua mara mbili ya kiafya. Hii ni kutokana na kwamba mfumo wa afya tangu hapo hawali nni mbovu sana pili maiti kwa sasa wengine wakiwa katika masanduku  na wengine hawana wamerundikwa katika barabara huku wakisubiri kupelekwa katika makaburi.

Ni hali ngumu ya kupindukia, ambapo tarehe 4 Aprili hata Rais  Lenin Moreno  ametangaza kuwa karibia vifo 150 wanakuswanywa kila siku kutoka katika nyumba zao na katika maeneo ya umma, hata hivyo hatua za utekelezaji bado haitoshi. Vyumba vya kuhifadhia maiti zote zimejaa na katika nchi yote ametaarifu  Padre huyo ambaye ni  Mkurugenzi wa Radio Katoliki ya Quito, mji mkuu kuwa mamia ya makampuni ya kuzika wamekataa kutoa huduma yao kwa sababu hawahisi kuwa naa usalama yaani ukosefu wa zana muhimu za kutumia. Hali ya nchi ni ngumu sana lakini zaidi huko Guayaquil  ndiyo janga hasa la kutisha.

China:Siku ya maombolezo na kukaa dakika tatu kwa ukimya nchini China

Nchini nzima ya  China wamekumbuka kwa heshima zaidi ya waathirika 3,300 wa virusi vya corona na vifo vya watu wa kwanza 14 waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za kusadia katika mji wa Hubei. Wakati wa kutoa heshima hiyo hewani zilisikia milio ya honi za magari. Rais wa nchi Bwana Xi Jinping ameongoza afla hiyo huko Zhongnanhai jijini Beijing.

Marekani: Rais Trump ahimiza kufaa barakoa bila kulazimisha

Serikali ya Marekani  imetoa wito kwa raia wake kufunika pua na mdomo kwa kutumia barakoa wakiwa katika maeneo ya umma ili kujinga dhidi ya virusi vya Corona. Wito huo umekuja wakati kuna wasiwasi wa  virusi kuwakumba zaidi ya watu milioni moja duniani na ambavyo vinaweza kusambaa kupitia njia ya kawaida ya kupumua.

Rais Donald Trump amesema pendekezo la kuwahimiza raia wote milioni 330 wa Marekani kutumia barakoa pindi wakiwa maeneo ya wazi litakuwa la muda mfupi na lisilo la lazima. Afisa wa afya wa ngazi ya juu nchini Marekani Jerome Adams amesema uamuzi huo umefikiwa kwa sababu watu wengi walio na virusi vya corona hawaoneshi dalili na kugeuka kitisho cha kuwaambukiza wengine. Tangu kugundulika kwa virusi vya corona nchini China, wataalamu wa afya wamesema virusi hivyo husambaa kwa sehemu kubwa kupitia chafya na kikohozi.

Uingereza: Malkia Elizabeth atahutubia Jumapili 5 Aprili katika Baraza la  Umoja wa Mataifa

Tukio ambalo ni mara chache sana, taarifa zinabainisha kuwa Malkia wa Uingereza Elizabeth II atahutubia katika Baraza la Umoja wa Mataifa.  Wakati hu huohuko   tarehe 4 Aprili 2020 Chama kikuu cha upinzani cha Labour nchini Uingereza kinatangaza kiongozi wake mpya. Wanachama takribani laki tano, wanatumai kuwa huo utakuwa mwisho wa kipindi kibaya zaidi katika historia ya miaka 120 ya chama hicho.

Umoja wa Mataifa:  sitisheni vita

taarifa kutoka Umoja wa Mataifa inasema hali  mbaya inakuja kuwa mbaya zaidi hasa katika nchi zenye vita na vizozo na hivyo imerudia kutoa wito wa kusitisha moto ulimwenguni. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataida Bwana Antonio Guterres kuwa ni wakati wa kugeuza maneno kuwa vitendo na kusitisha uhasama. Ametoa kauli hiyo tarehe 3 Aprili 2020  siku kumi tangu alipotoa wito wa kimataifa wa kusitisha uhasama katika ripoti yake aliyoiwasilisha kwa njia ya video mjini New York Marekani. Ameshukuru kuhusiana na wito wake alioutoa na kusikika katika sehemu mbalimbali zenye mogogoro lakini anahisi kwamba sasa umewadia wakati wa wito huo wa maneno kuwa vitendo

Katika ujumbe wake amesema “Kuna pengo kubwa kati za maazimio na vitendo, kati ya kutafsiri maneno kuwa amani sehemu mahalia na katika Maisha ya watu. Kuna changamoto kubwa ya utekelezaji ukizingatia kwamba migogoro imedumu kwa muda mrefu, hali ya kutoaminiana imemea mizizi na shuku na shaka zikitawala. Tunafahamu kwamba mafanikio yoyote yanayopatikana ni tete na yanaweza kugeuka kirahisi na baadhi ya migogoro hata imeshika kasi zaidi. Tunahitaji hatua madhubuti za kidiplomasia ili kukabili changamoto hizi. Ili kunyamazisha silaha ni lazima tupaze sauti kwa ajili ya amani.”

Ugiriki/uhamiaji: watoto wadogo wasiosindikizwa 1600 wanatarajiwa kuokolewa siku sijazo.

Kwa mujibu wa Baraza la Umoja wa Ulaya (UE) limetangaza kuwa watoto wadogo karibia 1600 wasiosindikizwa , inawezekana wakaokolewa siku sijazo na kupokelewa huko Lussemburgo.

Niger: Mauji katika mapigano kati ya wanajeshi na wanamgambo wa silaha

Wanajeshi wanne na magaidi 63 wameuawa Alhamisi 2 Aprili 2020 wakati wa mapigano kati ya  kikosi cha kijeshi na wanamgambo  wenye sihala katika maeneo ya Tillabéri, mpakani na nchi ya Mali.

SENEGAL yaadhimisha miaka 65° ya uhuru

Siku ya Uhuru wa nchi ya Senegal inayodhimishwa kila tarehe 4 Aprili kila mwaka, kwa mwaka huu  imejikuta katika dharura ya covid-19, janga la kimataifa. Nchi ya Senegal iliweza kujikomboa na kujinyakulia uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kifaransa mnamo tarehe 4 Aprili 1960.

Dharura ya Covid-19 ni tishio kubwa duniani kote

Kwa hali halisi kiasi cha watu milioni moja na elfu 80 wameambukizwa virusi hatari vya corona  duniani kote huku idadi ya waliokufa ikipanda na kufikia watu 57,474 kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Italia ndiyo imerikodi idadi kubwa ya watu waliokufa ambayo imefikia 14,681 ikifuatiwa na nchi ya Uhispania, Marekani na Ufaransa. Wakati virusi hivyo vikiendelea kusambaa dunianikote kwa kasi, benki ya maendeleo barani Asia imeonya kuwa janga hili litasababisha hasara ya hata dola Trilioni 4.1 kwenye uchumi wa dunia kutokana na athari zake kwa mataifa tajiri. Kadhalika mpango wa chakula wa Umoja wa Mataifa WFP umesema janga la Corona linatishia kusababisha upungufu wa chakula kwa mamilioni ya watu hususani barani Afrika. Karibu nusu ya idadi ya watu duniani wameamriwa kubakia majumbani wakati mataifa yote ulimwenguni yanaongeza zaidi juhudi za kupambana na virusi vya corona vilivyo hatri ambavyo havina mpaka na wala vizingiti.

04 April 2020, 13:11