Tafuta

Vatican News
Wanafunzi wa shule nchini Tanzania wanaombwa kufuatilia mafunzo yao kwa njia ya radio au televisheni wakati huu wa kipindi cha corona ambapo wamelazimika kukaa majumbani Wanafunzi wa shule nchini Tanzania wanaombwa kufuatilia mafunzo yao kwa njia ya radio au televisheni wakati huu wa kipindi cha corona ambapo wamelazimika kukaa majumbani 

Tanzania:Wanafunzi waombwa kujifunza kupitia redio na televisheni!

Wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO,wa kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kujifunza hata wakati wa huu wa waanafunzi kubaki nyumbani kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona,COVID-19,umeanza kutekelezwa hata nchini Tanzania,ambapo tarehe 20 Aprili Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,imezindua rasmi urushaji wa vipindi vya masomo kupitia Radio na televisheni.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kufuatia wito wa wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, wa kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kujifunza hata wakati wa huu ambapo watoto wametakiwa kubaki nyumbani kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, Nchini Tanzania, wameanza kutekelezwa ambapo tarehe 20 Aprili 2020 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imezindua rasmi urushaji wa vipindi vya masomo kupitia televisheni na Radio.

Uzinduzi wa urushaji wa vipindi hivyo vya masomo umefanyika Dodoma mji mkuu wa Tanzania na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo. Wakati wa uzinduzi huo amethibitisha kuwa vipindi hivyo vya masomo mbalimbali kwa ngazi ya elimu ya awali, elimu ya msingi na elimu ya Kidato cha  cha kwanza mpaka cha sita, vitasambazwa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini humo ili masomo yaweze kufikia wanafunzi wote nchi nzima. Lengo kubwa la kutoa vipindi hivi ni kuwaezesha wanafunzi waendelee kujifunza wakati huu ambapo wako nyumbani, katika kipindi hiki ambapo shule zao  zote zimefungwa.

Ni mfumo ambao umewezesha wanafunzi wengi katika mataifa yote ulimwenguni kuaniza Ulaya na kwingineko, kama ilivyo hatashughuli nyingine za kiofisi ambazo zinafanyika katika majumbani. Madarasa yako wazi lakini elimu inaendelezwa kwa kutumia teknolojia wakati huu wa kukabiliana na COVID-19. Aidha kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Elimu,  Akwilapo amesema wizara yake iliandaa vipindi hivyo kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania. Kuhusiana na lugha, amesema  urushwaji wa vipindi hivyo hauna maana ya kuwa mbadala wa masomo ya darasani mara baada ya shule hizi kufunguliwa baada ya janga hili kuwa limekwisha. Kwa hivyo amewasihi walimu wataendelea na mitaala yao kama inavyoelekezwa kwenye taratibu zao za kila siku sio kwamba wataruka mambo ambayo yatakuwa yamerushwa kwenye vipindi hivyo.

Kadhalika akifafafanua zaidi kuhusiana na wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wafanye mitihani amebainisha kuwa Baraza la mitihani la Tanzania limeandaa vipindi  kwa ajili ya maandalizi ya watahiniwa wa kidato cha sita nayo pia yatarushwa kwenye vyombo hivi. Vipindi hivi vitawawezesha watahiniwa hawa kufanya marudio ya mada mbalimbali ambazo wataalam wa baraza la mitihani wameona ni vizuri zikafanyiwe marejeo na kwa maana hiyo wamejizatiti katika mada ambazo zinakuwa na maswali magumu wakati wa kufanya mtihani. Kwa kuhitimisha amerudia msisitizo wake kuwa vipindi hivyo havitakuwa mbadala pindi shule zitakapofunguliwa na kwamba walimu wataendelea kufundisha kwa kufuata mitaala hata kama kuna matangazo ya radio na televisheni.

Kwa wanafunzi na watu wote endelea jifunza ugonjwa huu wa vurusi vya corona au COVID-19 na kuzingatia kwa makini yale yote yanayotolewa kueleimisha juu ya janga hili: Coronavirusi ni kundi kubwa la virusi ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa kuanzia homa ya kawaida kwenda kwa magonjwa mazito ya kupumua kama bronchitis, pneumonia au ugonjwa kaliwa kupumua kwa papo hapo (SARS). Virusi vya corona 2019 novel (COVID-19) husababisha maambukizo ya mfumo wa upumuo yaliyoanza mkoa wa Hubei (Wuhan), nchini China. Dalili za ugonjwa huu ni kama mafua au maambukizo ya kawaida ya mfumo wa upumuo, dalili huwa tangu za kadiri mpaka zilizo kali na zinaweza kuwa:homa, kohozi  na shida ya kupumua.

Magonjwa ya ziada ya virusi vua corona au covid-2019 ni pamoja na hali mbaya kama nimonia au kushindwa kwa figo kufanya kazi na wakati mwingine kusaaìbaisha vifo ambavyo vimeonekana na vinaendelea kutokea.Virusi vya corona vinasambazwa kwa kiasi kikubwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ukikaa karibu, kwa mfano, nyumbani, kazini au katika kituo cha afya na sehemu zenye mikusanyiko. Hata hivyo kukaa  karibu kunamaanisha kuwa ndani ya miguu sita (mita 2) na mtu kwa muda mrefu. Hii hutokea unapomtunza mtu, ukiwa mpenzi wa mtu, unapoishi na mtu, unapotembelea mtu au unapokuwa katika sehemu ya kusubiri huduma na watu wengine. Ikiwa umekaa karibu na mtu ambaye amepatikana kuwa na COVID-19: kaa nyumbani, punguza mawasiliano ya moja kwa moja na watu wengine, na upigie simu Idara ya Afya ya Elimu ya Magonjwa ya Mlipuko ambazo zimetolewa kutokana na kila taifa, mkoa, wilaya ili ujadili ikiwa unahitaji kumwona mtoa afya na jinsi utakavyochunguza dalili zako.

Kwa kuwa hakuna dawa ya chanjo inayopatikana kwa sasa ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona au covid-2019, lakini kuna vitendo vya kila siku ambavyo vinaweza kukusaidia kuzuia usambazaji wa vijidudu visivyoonekana kwa macho ambavyo husababisha magonjwa ya kupumua na kwa maana hiyo: Epuka kugusana/kuwa karibu na watu ambao ni wagonjwa; Epuka kugusa macho, pua na mdomo wako; Kaa nyumbani ikiwa unagonjwa; Funika kikohozi chako au kupiga chafya na tishu, kisha utupe tishu hizo kwenye takataka; Safisha na sanitisha vitu vya kugusiwa kila mara na nyuso ukitumiya dawa ya kawaida ya kupuliza, kusafisha nyumbani au kupanguza; Nawa mikono mara nyingi ukitumia sabuni na maji kwa angalau sekunde 20, hasa baada ya kwenda chooni; kabla ya kula; na baada ya kusafisha pua lako, kukohoa au kupiga chafya; Ikiwa sabuni na maji hayapatikani, tumia sabuni ya kuua viini iliyoundwa na bidhaa za kileo iliyo na angalau asilimia 60 ya kileo. Daima nawa mikono ukitumia sabuni na maji ikiwa mikono yako inaonekana kuwa chafu.

21 April 2020, 09:52