Tafuta

Vatican News
Ukanda wa Afrika Magharibi ambamo nchi nyingi zinakabiliwa na changamoto za vita,wakimbizi na wakimbizi wa ndani ziko hatarini katika hatari ya maambukizi ya covid-19. Ukanda wa Afrika Magharibi ambamo nchi nyingi zinakabiliwa na changamoto za vita,wakimbizi na wakimbizi wa ndani ziko hatarini katika hatari ya maambukizi ya covid-19.   (AFP or licensors)

Shirika la kuhudumia wakimbizi katika harakati za kuokoa wakimbi ukanda wa Afrika Magharibi&Kati!

Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema nchi 21 za ukanda wa Afrika Magharibi ambazo nyingi zinakabiliwa na changamoto za vita,wakimbizi na wakimbizi wa ndani zinahitaji msaada ili kukabiliana na janga jipya la covid-19 linaloendelea kuyumbisha dunia kwa sasa.

Kutokana na changamoto mpya iliyozuka ya virusi vya COVID-19 Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linafanya kila juhudi kuhakikisha linanusuru maisha ya mamilioni ya watu ukanda wa Afrika Magharibi na Kati yaliyo hatarini. Shirika hilo linasema nchi 21 za kanda hiyo ambazo nyingi zinakabiliwa na changamoto za vita, wakimbizi na wakimbizi wa ndani zinahitaji msaada ili kukabiliana na janga jipya linaloitikisa dunia hivi sasa.

Kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi linasema COVID-19 imeongeza changamoto katika ukanda ambao tayari ni moja ya mgogoro mkubwa kabisa wa kibinadamu duniani ukihusisha zaidi ya watu milioni moja ambao wamelazimika kutawanywa. Janga hili la corona kwa mujibu wa UNHCR limesababisha mipaka kufungwa na kuongeza shinikizo katika mifumo ya afya ambayo inayumba na uchumi dhaifu. Moja ya vitu vinavyofanywa na shirika hilo la wakimbizi ni kuongeza msaada wa serikali kuweza kushughulikia hali ya kibinadamu inayozidi kuzorota. “Kipaumbele chetu ni kuhakikisha fursa ya usalama na kujaribu kupunguza athari za mlipuko wa janga hili la corona” limesema shirika hilo.

Hadi sasa nchi zote 21 za ukanda huo zimeripoti jumla ya wagonjwa 5000 wa COVID-19 na vifo Zaidi ya 100. David ni mmoja wa viongozi wa jamii zinazowahifadhi wakimbizi katika makazi ya wakimbizi ya Adagom anasema “Hivi sasa tunapaswa kuwa waangalifu sana kuhusu COVID-19. Janga hili ni Dhahiri, na kwa hakika wametuwekea hadi ndoo hapa kwa ajili ya kunawa mikono na kuwa makini , pia hatupaswi kutoka nje , tunapaswa kusalia ndani kwenye maeneo ya kambi hadi pale mtakapoambiwa kwamba janga hili limekwisha.”

Na eneo hilo la Afrika Magharibi na Kati “ni moja ya eneo la Afrika lenye idadi kubwa ya waliotawanywa likiwa na jumla ya wakimbizi wa ndani milioni 5.6, wakimbizi milioni 1.3, watu waliorejea makwao milioni 1.4 ambao bado wanahitaji msaada na watu milioni 1.6 ambao hawana utaifa.” UNHCR inasema kwa mfano Nigeria inahifadhi wakimbizi 57,000 na shirika hilo linashirikiana kwa karibu na serikali na mamlaka ili kuimarisha fursa za huduma za afya , maji, usafi na vituo vya kujisafi hasa katika juhudi za kuwalinda wakimbizi na jamii zinazowahifadhi. Na kwa upande wa Niger UNHCR imetoa mafunzo kwa wasanii na mafunzo cherahani ili kutengeneza barakoa kwa ajili ya wakimbizi na watu wa jamii zinazowahifadhi.

Mali na Burkina Faso:Kama hiyo haitoshi nchini Mali uchaguzi wa wabunge kwa sasa unaendelea kusumbuliwa na ghasia za kijihadi ambazo zimezuia kupiga kura katika baadhi ya maeneo. Wakati huo huo, kwa mujibu wa taarifa kutoka na  Right Watch zinasema kuwa nchini Burkina Faso wameuwawa rai 31 na vyombo vya usalama. Operesheni hizo zilianza Aprili 9. Iliyowasilishwa rasmi kama uingiliaji wa kupambana na ugaidi, Right Watch inashutumu vikosi vya usalama vya kulenga watu wa jamii ya Saule nusu wachungaji ambao kwa mujibu wa wataalam, vikundi vya Kiisilamu viko vinawafundisha. Kwa mujibu wa Right Watch wanaomba serikali kufanya uchunguzi huru.

20 April 2020, 17:29